Boyzmen Talks by Raphael JL.
TUTAFJIFUNZA KWA UJUMLA NAFASI YA MWANAUME
kwa muda wote tutakuwa
tunaangalia nafaso ya mwanaume katika jamii pana kama biblia inavyoonesha
Somo hili litatupa nafas ya kujitafakari na kuangalia namna
ambavyo mungu amempa mwanaume nafasi ya ajabu sana katika jamii
Kutokujua
nafasi yako haimaanishi nafasi yako haipo.
Utakuwa huru kuuliza na kuchangia pia
LEO NINAOMBA TU NITOE TAKWIMU ZA MSINGI KIDOGO KUHUSU WANAUME
takwimu hizi zitatusaidia mbele ya safari
ni vema tu kujua mambo mawili makubwa kuhusu
takwimu za wadada na wakaka ili usikae unashangaaa
Ø Idadi ya
wakaka na wadada hazitakuja kukaa zikalingana
Ø Farao aliua
wakiume wengi sana
Ø Herode
aliua wakiume wengi sana
Ø Takwimu
zinaonyesha watoto wa kiume chini ya umri wa miaka mitano wanakufa sana kuliko
wadada
Ø cha ajabu ni kwamba, ni rahisi sana kwa
mwanaume kuwa na wake zaidi ya mmoja na sio kinyume chake.
kwani sasahivi kuna
madhara gani kwamba mwanaume anaweza akaoa wanawake wengi na sio mwanamke?
tufahamu kuna vitu
vimeandikwa kwenye biblia sio kwamba mungu aliviruhusu ila kwa mazingra ya
wakati ule ilijifanya kama haoni au alipotezea sana.
LEO TUTAANZA RASMI SOMO LETU
Ø Kwanza
tufahamu kuwa adam ni jina la wote wawili.
Ø muungaaniko ambao hakuna mwanadamu anaweza
kuuvunja.
Ø Wote ni
wanadamu yaani wametoka mavumbini, wameumbwa. Ila eva likuwa ndani ya adamu
kama ambavyo adam alitoka tumboni kwa eva baada ya anguko.
Ø Kwahiyo
mwanume na mwanamke wameumbwa kuwa au kuishi pamoja. Sio mambo ya ushoga na
usagaji.
Ø baada ya adam wa kiume kuumbwa mungu alikuwa
ameshamuandalia tayari location ya kukaa na jukumu la kufanya. Ailime na
kuitunza bustani. Muhimu sana hii.
Ø ni jukumu la adam kuilima na kuitunza
bustani,kwa tafsiri hii ni jukumu la adam kufanya kazi na kuzalisha na kulinda
familia. Ni wajibu na jukumu lake.
Point: ukiona unagombania nafasi
yako ujue umeshatoka kwenye nafasi yako tayari maana kama nafasi ni yako huna
haja ya kuigombania. Kikubwa ni kupata ufahamu sahihi.
Mwanzo 2:16
“Bwana mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani
waweza kula”
Baada ya adam kupewa wajibu na jukumu la
kufanya kila siku katika ile bustani mungu alimpa wajibu mkubwa sana mwingine
katika familia. Alimpa amri na agizo. Na wajibu wake uikuwa kuwa kiongozi
kwasababu hiyo.
Agizo kwa adam:
Mwanzo
2:16-17
“Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani
waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana
siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
huu ni wajibu mkubwa
sana wa mwanaume kiroho.
Ni mwanaume aliyepewa agizo na amri. Ni yeye ndiye alitakiwa
kumfundisha eva. Na alifanya hivo, kwa kiwango gani sisi hatujui ila
tukijifunza kutoka kwenye kosa la eva tunaona mengi sana.
Haya
ninayosema hapa ni msingi wa kujua nafasi yako kama mwanaume.
ukiyajua haya
utamrahisishie sana mdada uliyemoa au utakaemuoa.
na yeye akiwa
amefundishwa namna hii basi ni kukua tu na kusonga mbele.
Tunaona mambo kadhaa makuu
sana:
1.tumeshaona adama amepewa kazi ya kuilima na kuitunza bustani. Peleka
wazo hili kwenye familia yako.
2.tunaona adamu amepewa agizo
la kiroho kama kionogozi, ajue kuwa ile bustani ina mipaka yake. Asile matunda
ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
3.bado mungu anaongea na yeye peke yake, hapo bado eva hajaja bado.
Mwanzo 2:18..
“Bwana Mungu akasema, si vema huyo
mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Ø Kwenye huu
msitari ni muhimu ukausoma vizuri sana. Ni Mungu ndiye aliyeona uhitaji wa adam
kuhitaji msaidizi. Ni mungu ndiye aliyesema atamfanyia msaidizi. Ni Mungu ndiye
aliyemfanyia msaidizi. Ni Mungu jamani.
Ø Hii ni
muhimu sana kuelewa kwani vinginevyo unaweza ukajikuta unajifanyia msaidizi
wako. Itakuwa hatari sana.
Ø Moja kati
ya maeneo nyeti kuyaelewa ni hili: msaidizi wa kufanana nae. Maana yake
anaekuja kumsaidia adam kwenye yale majukumu na wajibu aliopewa au tuseme
kwenye yale maono. Kusingekuwa na haja ya kuwa na msaidizi kama hana cha
kusaidia. Ni hatari kujitafutia msaidizi na hana cha kukusaidia mwisho wake
mtaanza kugombania nafasi kila mtu na ya mwingine.
Ø Pia ni vema
ukaona hapo hapo kuwa, usaidizi wa msaidizi huyu anaetoka kwa Mungu haijakaa
kuoneana au kumlalia au kumkandamiza au kudai haki sawa. Imekaa kikusudi.
Mwanaume ni kiongozi. Mwanamke ni msaidizi. Msaidizi anakuja kusaidia majukumu
na wajibu wa kiongozi.
Nikupe
mfano mzuri,
Neno
msaidizi hapo sio assistance bali ni neno makamu, bado kwa kingereza ni
helper...lakini lazima ujue kuwa mwanamke sio mwenye majukumu, majukumu ni ya
mwanaume. Kwamba mwanamke atakusaidia haimaanishi ni wajibu wake maana yeye
anabaki kuwa msaidizi. Ukiwa haupo anasimama kwenye nafasi yako, ukirudi
unaendelea na wajibu wako.
Ø Ndio maana
wakuu wa shule wenye akili wanaweza wakawa wanazunguka tu duniani kama
wamewawezesha vizuri mamakamu wao kusimamia wajibu wao. Makamu akiwa na bidii
halafu mkuu akawa na akili basi makamu ataonekana kama mkuu kwani mkuu anajua
huyo ni msadizi wake yaani mtu aneweza kufanya kazi zake zote kwa kumsaidia.
Ø Kwahiyo
kibiblia ni muhimu wewe kama wa kuime ujue kuwa wewe ndio wa kuilima na
kuitunza familia na wewe ndio mchungaji
kiongozi wa familia maana ulipewa agizo kwanza wewe kabla ya mwanamke. Muhimu
sana.
Mwanzo
2:19-20
“ Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na
kila ndege wa angani, akamletea adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai,
jina alilokiita adamu likawa ndilo jina lake.
20 adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani,
na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia adamu aliyefanana
naye.”
Ø Wazo la
kwanza la msaidizi wa adam halikufua dafu wala kufaa hata kidogo. Kuwapa tu
wanyama majina na kujichagulia mnyama mmoja haikufaa kitu. Ndio maana usimfanye
mwanamke kama mnyama maana hakuna mnyama aliyefaa kuwa msaidizi. Weka moyoni
Ø wazo la msaidizi lilipokuja kwa Mungu, mungu
alianza kulifanyia kazi na akaanza kwa kumeletea adam wanyama wa kila aina.
Utaona adam anaishia tu kuwapa majina na katika hao wanyama hakuwepo msaidizi
ambaye mungu alitaka ampe adam. Ndo maana nikasema, kama wanyama hawakuweza
kufaa kuwa msaidizi wa adam,basi wanaume wasiishi na wanawake kana kwamba
wanawake ni wanyama kwani wanyama hawakufaa kuwa wasaidizi. Nafasi ya mwanamke
ni ya juu kuliko mnyama.
Ø Si unajua
kuna mila na desturi ambazo zinamuona mwanamke kama si kitu,na kumbe ni
msaidizi aiseeeee
Ø kwahiyo mpaka msitari wa 20 tunaona swala la
msaidizi bado halijapata ufumbuzi wa kudumu.
Ø Usisahau
kuwa swala la msaidizi sio la adam
Ø Uhitaji
haukuonwa na adam bali ni mungu mwenyewe.
Ø na unaona pia kuwa, Mungu aliona kuwa si
vema...ni ama kusema haikumpendeza kumuona adam yuko peke yake tu na huku
anatakiwa kuwajibika kwa kuilima na kuitunza bustani.
Ø Vijana
wengi wa kiume na hasa kwenye kizazi hiki chetu wamekuwa maarufu sana kwa
kukwepa kuwajibika kwa visingizio kadhaa. Kumbuka msaidizi haji kukuchukulia
nafasi yako kama wanaume na kiongozi. Anakuja kukusaidia. Ni lazima ukubali
kuwajibika.
Mwanzo 2:21-22
“ Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika
ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea adamu ili aone
atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita adamu likawa ndilo jina lake.
20 adamu akawapa majina yao kila
mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini
hakuonekana wa kumsaidia adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea adamu usingizi mzito,
naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika adamu
Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa adamu.”
Ø Hili ni
jaribio la pili la mungu kumtafutia adam msaidizi. This time ni usingizi tu.
Maana lazima msaidizi afanane na adam yaani amfae katika yale majukumu yake.
Ø Kwahiyo
wote tunajua kuwa eva alitolewa kutoka kwenye ubavu wa adam ila kuna itu cha
ajabu sana kwenye jaribio hili la pili....
Ø Japo kwamba
swala la msaidizi halikutoka kwa adam lakini msaidizi alipoletwa na mungu adam
hakujiuliza mara mbilimbili,alijikuta anabubujika kwa mshangao akisema...huyu
sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu,ataitwa mwanamke kwa
mkuwa alitolewa katika mwanaume.
Ø Kumbe hapo
kipo kikubwa cha kujifunza. Akitoka kwa mungu hakika utamfurahia sana.
Ø Usisahau
pia kuwa ni adam ndo alitoa jina la mwanamke, maana alishakuwa na uwezo wa
kutoa majina kama alvyowapa wanyama wote waliokuwemo bustanini majina yao. Ila
utaoana kwa hakika kuwa jina la msaidizi lilikuwa na tofati kubwa sana.
Mwanzo
2:24
“ kwa hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja.”
Ø Kumbe,
kimsingi hapa tunaona mwanaume anaagizwa yeye kuachana na wazazi wake ili aambatane
na mumwe. Fahamu kuwa adam aliyasema haya lakini tunajua wote wawili hawana
wazazi wa kimwili.
Ø ni aibu kwa mkaka ambaye anataka kuoa na bado
anataka wazazi wake na hasa mama yake aendelee kukaa kwenye nfasi hata ya
kumuamulia mambo ya kufanya.
Ø ukisoma hiyo mistari utagundua kuwa mambo
yalikuwa sawa kabla ya anguko.
Ø Mpaka hapo
ni sura ya pili wa mwanzo ndo inaishia na msitari wa 25 na inaonyesha kulikuwa
hakuna aibu ingawa hawakuwa na nguo. Hapa lazima kuelewa jambo pia.
Ø walikuwa uchi kwa jinsi ya mwili lakini
walikuwa wamevikwa na uwepo wa mungu na ndo maana haikuwasumbua kwamba walikuwa uchi kimwili
but roho zao zilikuwa zimefunikwa na uwepo wa mungu.
Ø Ni wazi
kwamba adam na eva walikaa bustanini kabla mambo hayajaenda kombo kwa amni na
utulivu mkuu.
Ø Hii inatupa
kujifunza kama wanaume na viongozi kuwa ni uwepo wa Mungu tu unaoweza kutufanya
tuishi kwa usalama na amani.
Ø Kimsingi
ukisoma biblia utagundua kuwa ni jambo baya sana lilitokea pale adam
alipokubali kula lile tunda
Ø Mambo mengi
yanayoendelea kutoa hata leo kama usagaji na ushoga na maandamano ya haki sawa
na movement za wanawake kama beijing yalizaliwa na taarifa ya uharibifu baada
ya anguko
Ø Ndo maana utaona wadada wengi wa leo walidhani
wakiwa na pesa zaidi au kisomo zaidi basi wanaweza kukaa kwenye nfasi kama
mwanaume. Bila kujua kuwa mwanamke na mwanaume waliumbwa kutimiza kusudi wakiwa
kwenye nafasi zao na sio nje.
Ø Hatuwezi
kukataa kuwa zipo jamii zinazowakandamiza wanawake lakini utagundua kuwa jamii
hizo wanaofanya hivyo sio wanaume peke yao bali na wanawake walioharibika.
Kikubwa na kupata ufahamu sahihi ili tusiingiliane nafasi.
Ø Mwanaume
anaetambua nafasi yake ni rahisi sana kumsaidia mwanamke asiyejua nafasi yake
kwani mahusiano yenyewe sio ya kuonyeshana umwamba. Bali kujengana na kusaidiana
na kuimarishana.
Niseme kidogo kuhusu takwimu zisizo rasmi....
Ø Kwamba
wakaka ndio wamekuwa sababu kubwa sana ya mahusiano mengi yasiyoeleweka kwani
inaonekana kwamba wanaume wengi wanapoingia kwenye mahusiano basi sex huwa kitu
cha msukumo wa pekee sana.
Ø Inaonyesha
pia kuwa wanaume ndio wamekuwa kichocheo kikubwa kuwashawishi wadada waweze
kufanya sex kabla hawajaachana na wazazi wao. Kumbuka agizo ni kuwa watakuwa
mwili mmoja wakishaachana na wazazi wao.
Ø Pia
inaonyesha pia kuwa wanaume wamekuwa wakibadilikabadilka zaidi ya kinyonga
kwenye mahusiano.
Ø Wakaka wengi wanaamini huwezi kuwa na mdada mmoja
tu.
Ø Kwamba
wakaka wanaamini mahusiano ya bila sex kabla ya ndoa hayawezekani kwani wengi
wanaogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Ø Wakaka
wengi wanaogopa kuwaoa wadada wenye uwezo au kisomo kikubwa zaidi kuliko wao.
Ø Wakaka wengi hawapendi kuwa na wadada ambao
wanaonekana wanaulizauliza sana vitu.
Ø Hizi nyingi
na zaidi zinasababishwa sana na ufahamu, yaani kukosa ufahamu sahihi.
Ø Mfano,kuna mambo ya kujifunza wakati na baada
ya anguko.
Ukifuatilia
mchakato wa anguko utashangaa kidogo...
Ø Nyoka
alimfuata mwanamke. Lazima kutakuwa kuna sababu kwanini alipitia kwa mwanamke
na mojawapo huenda ikawa kwamba nyoka alijua adam ndo aliyesikia na kupewa lile
agizo la katazo.
Ø swali la kujiuliza ambalo halina jibu ni kuwa
adam alikuwa wapi wakati nyoka anazungumza na mwanamke? Maana hapa ndo tatizo
lilipo na linapoanzia na kuishia pia.
Mwanzo 3:1
Tunaweza tukawa na mengi ya kujifunza hapo....
“ basi nyoka
alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Akamwambia mwanamke, ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda ya miti
yote ya bustani?”
1.kama adam alikuwepo wakati nyoka
anazungumza kwanini alikaa kimya,kwanini asingejibu usahihi wa mambo au ni
kwakuwa aliyefuatwa kuulizwa ni mwanamke.?
2.kama nyoka alimfuata mwanamke na
kuzungumza nae basi huenda hakumfuata kimwili,labda aliingia ndani ya mawazo
yake na kuhojiana nae huu adam hajui kinachoendelea mpaka alipoona tunda
linachumwa na kula. Kama hivi ndivyo bai yule nyok hakuwa tu nyoka bali shetani
kabisaaa.
Ona hapa mwanzo 3:6
“mwanamke
alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa
kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na
mumewe, naye akala.”
Ø ..angalia
yale maneno ya mwisho...alitwaa katika matunda yake akala, na akampa na
mumewe,naye akala.....kwa haraka sana unawaza lazima walikuwa wote ila kuna
kosa adam atakuwa alilifanya hapo. Kama alikuwepo basi hakusimama katika nafasi
yake pindi nyoka ameanza hoja zake,ni kama alitakiwa kuingilia kati na kujibu
kwa usahihi.
Ø Ni kama
wewe upate mgeni nyumbani kwako...mke wako akamfungulia mlango..mgeni akasema
siingii naomba niulize hapa hapa...wewe ukaenda kujua ni nini kinaendelea
ukafika ukakuta swali la kwanza limeulizwa na mkeo anaijibu, ukakaa
kimya...mazungumzo yakaendelea mpaka mke wako akapokea tunda na kulila na wewe
uko kwa pembeni...ni rahisi sana kumlaumu adam
Ø Cha ajabu
ni kuwa iko wazi kabisa kwamba nyoka alimdanganya mwanamke lakini adam
hakudanganywa. Yeye alikula tunda kwa sababu ya ushawishi wa mpenzi wake.
Ø kuna namna adam alitakiwa asimame katika zamu
yake.
Ø ili kuthibitsha kuwa adam alitoka kwenye
nafasi yake...tuangalia haya....
mwanzo
3:7
“wakafumbuliwa
macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini,
wakajifanyia nguo.”
Ø Wakafumbuliwa
macho....kwani walikuwa vipofu? Hii inashitua sana. Kumbuka mwanzo 2:25.
mwanzo
2:25....mwanzo 3:7...linganisha
linganisha na efeso 1:18//
Ø Tuunganishe hiyo mistari mitatu sasa ili tujue hii
siri hapa....
1.kwanza kutoka mwanzo 2:25, walikuwa uchi na hawakuona aibu,
hii inamaanisha macho yao yalikuwa sio vipofu bali walikuwa wanaona na ndo
maana hawakuoneana aibu. So mpaka hapa sio issue ya macho tu ya kawaida.
2.mwanzo 3:7,lile tunda halikuwa la kawaida kwani baada ya
kula tu wakafunbuliwa macho,wakajiona wako uchi na aibu ikaja. Hapa utaona kuwa
tunda na macho ya kimwili yalibeba maarifa na taarifa ya rohoni ambayo hapo
kwanza mungu hakupanga adam ajue ila alipoijua ikamfumbua macho yake ya mwili
na kumpofusha macho yake ya rohoni.
3.efeso 1:18,kumbe ni
macho ya moyo ndio yalipata shida ya anguko. Maana yake ufahamu wa mwanadamu
uliharibika hapa na akawa kipofu, akawa hawezi tena kuelewa mambo ya mungu kwa
kutumia akili zake.
(mpaka hapo
tuko sawa?)
so baada ya anguko...ufahamu wa adam uliharibika
kabisa. Akawa hawezi tena kumwelewa Mungu. Alirugugwa...lakini kuna kitu pia
hiki hapa angalia.....
Mwanzo 3:8
“ kisha wakasikia sauti ya bwana mungu,
akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; adamu na mkewe wakajificha kati ya
miti ya bustani, bwana mungu asiwaone.”
Walijifichaje wakati
siku zote wamekuwa na mungu masaa yote?
Walidhanije kuwa wamejificha wakati mungu ndiye aliyetengeneza bustani
yenyewe? Kama walijificha ina maana kuna kitu kilitokea ndani ya ufahamu wako
kuhusu kosa walilofanya. Walipokea ufahamu wa uharibifu.
Jambo lingine hili hapa....
Mwanzo 3:9
“ Bwana Mungu akamwita adamu,
akamwambia, uko wapi?”
hili
ni swali la muhimu sana
Where
are you-uko wapi....hili swali aliulizwa nani?
Ø Adam wa
kiume aliulizwa....uko wapi.....adam wa kike aliulizwa...umefanya nini?
Linganisha
mwanzo 3:9....na mwanzo 3:13
“Bwana Mungu
akamwambia mwanamke, nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, nyoka
alinidanganya, nikala.”
Swali moja kaulizwa
kiongozi...swali lingine kaulizwa msaidizi...do you see that????????????????/
Ø Uko
wapi...maana yake hakuwepo mahali alipotakiwa kuwepo...alitoka nje ya nafasi
yake.
Ø Mpaka leo,
kila wakati mwanaume akitoka nje ya nafasi yake hakuna mahusiano yako salama,
hakuna ndoa iko salama na hakuna familia iko salama.
Ø ndo maana watu wengi hawajui kwanini familia
zinayumba
Ø Kwanini
famiia zimevurugwa
Ø Familia
ndio si unit of God's mission to the world.
Ø shetani nae aliliona hilo akaamua apige
panapouma.
Ø Akawavuruga
wote wawili kwa kuwapa tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya...yaani aliwapa
taarifa iliyoharibika ambayo alikuwa nayo yeye na mungu tu. Akaipenyeza kwenye
familia. Toka wakati huo,familia hazijabaki salama mpaka sasa.
Ø Wote wawili
waliulizwa swali moja na wote hawakupatia kujibu...
mwanzo
3:10-11
“akasema,
nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha
Akasema,
ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti
niliyokuagiza usiyale?”
aliulizwa uko wapi...huu ndo mwanzo wa makosa
na kujitetea na kusingiziana.
Quotes by raphael jl:
“kama hauko tayari
kupoteza kiwango fulani cha uhuru wako binafsi ujue hauko tarayi kuwa kwenye
mahusiano ya kukupeleka kufunga ndoa. Mnapokutana watu wawili mlio tofauti ni
lazima kukubali kuwa kuna mambo ya kuongeza na ya kupunguza, mchakato wake
unahitaji hekima ili usije ukajikuta unaishi peke yako kwa kuendekeza ubinafsi
wa kutaka tu mambo yako ndo yafanyike. Relationship is a function of sacrife.”
Ykm-satisfied
in jesus!
Tuendelee
mwanzo 3:10-11
“akasema,
nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
akasema, ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi?
Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?”
Ø Tunda la
ajbu sana hii. Ukila unajikuta uchi. Haha hahaha
Ø Tukisoma
kwa makini tutagundua kuwa kumbe mungu alikuwa anatafuta utii wa adam katika
agizo au neno la mungu. Kutokutii kunakufanya uwe uchi na adui anapata kila
sababu ya kukudhuru.
Ø Mti ambao
adam alikula tunda lake unaitwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kumbuka mungu
alitaka adam asiyajue mabaya. Hii inamaanisha kuwa nyoka alifanikiwa kupitisha
taarifa mbaya kwenda kwenye familia ya kwanza kabisa duniani na kuivunjavunja
vipande vipande.
Ø Fahamu
tatizo lililowakalia wanaume wengi. Na upange kuwasaidia.
Wanaume wengi wanasumbuliwa na tatizo la
kutojali, kwa kimombo tatizo hili huitwa passivity.
Ni ile hali ya kuwepo mahali lakini haupo.
Yaani present but not available.
Wanaume wengi hawana muunganiko wa kihisia na
watoto pamoja na wake zao kwa sababu ya huu ugonjwa wa kutojali. Wapo nyumbani,
lakini hawapo
Wapo nyumbani, mambo yanaharibika lakini
hawajali.
Wapo nyumbani, watoto wanaharibika lakini
hachukui hatua. He is passive.
Majority of men are present at home in
quantity but not in quality. They are physically present but emotionally
absent.
Men
have not emotional bonding with their children, especially boys. The boys are
more connected to their mothers who are always available for the children. If
you talk to any child or youth of school going age about their home affairs
she/he will repeatedly mention mom did this and that, mom taught me this and
that, mom told me not to do this and that.
This
tells us that, there is only mom in the mind of our children. And mom is in
their mind because she always connects with them even the teachings and
trainings are done by the mother. But where is the father?
Boys
are less trained, even the church has not done this because even the church is
kwa kiwango kikubwa linaongozwa na wanaume. Mara nyingi children are not in the
mind of many men.
But
if you read many of the Church strategic plans. You will find plans to train
women, to train girls and widows. But in essence men need a substantial
training about manhood for the good of the family and the church at large.
It
is our dear cry to our almighty God, that one day this truth will be seen and
given due attention by the church elders and leaders.
Please,
let us come together and pray for mindset transformation of the Church so that,
men may be considered for his glory.
Mwl
balele
#nothing
changes until your mind changes!
Haya ndio mapenzi ya mungu-kutakaswa na kuuweza mwili kwa
utakatifu na heshima
Ninasoma 1 wathesalonike 4:3-8, yapo mapenzi
ya Mungu na katika mengi ambayo ungetamani kuyajua basi haya hapa ni mojawapo
ya msingi sana. Hebu jaribu kuyatafakari na kuyaomba pamoja nami leo.
Ni mapenzi ya Mungu kwamba sisi tutakaswe, tuwe
wasafi, tusio na mawaa kwa ile imani yetu ndani ya damu ya Yesu. Tunatakaswa
kwa lile neno ambalo ndio kweli kila siku maana kila siku kuna uchafu mwingi
tunaona na kusikia kama Isaya 6:5. Tuombe Mungu atatukase na
kutusamehe. Kama tunatakaswa basi ni wazi kuna yanayotuchafua na neno limeweka
wazi kwamba tuepukane na hayo.
Tuepukane na uasherati na uzinzi maana haya ni
kama kiungo na katika kuenenda kwetu basi tujue namna ya kuuweza mwili katika
njia ya utakatifu na heshima. Lazima tuelewe hapa kuwa katika kuuweza mwili
yaani kuufanya mwili usitutumikishe katika yale yanayotuchafua yaani uasherati
na uzinzi tunatakiwa kufanya hivyo kwa utakatifu na heshima. Na ndio maana ni
muhimu kupata muda wa kufunga na kujizuia kufanya mambo yanayoweza kukusaidia
kuzidi kuwa mchafu. Kufunga sio kuacha kula maana kama ni kuacha kula basi
wengi sana wanafunga kila siku. Mwii huu ni kizuizi kikubwa sana cha kutimiza
kusudi la mungu kwani umejaa tamaa ambazo zote haziendani wala kukubaliana na Mungu.
Kumbe ni mapenzi ya Mungu tutakaswe na kuuweza
mwili kila mmoja wetu na hii inamaanisha kuwa hakuna atakaejitetea maana kila
mmoja anawajibika kwa mwili wake katika kuuweza kwa utakatifu na heshima badala ya kuweeza kwa tamaa mbaya kama
mataifa wanavyofanya.
Tususahau kuwa ule wito ambao Mungu ametuitia sio
wito wa uharibifu bali wito wa uzima katika yesu bwana. Hatujaitwa kuwa wachafu
wala hatujaitwa kuwa wachafu. Tumeitwa katika utakaso. Tumeitwa kutakaswa kila
siku. Na haya ndio mapenzi ya mungu kwetu.
Eeh Bwana Mungu, mwingi wa rehema na huruma
nakuomba ututakase leo tena kwa damu ya Yesu na utupe neema ya kuwa na kiu ya
kuzama katika kweli ya neno lako ii tuzidi kutakaswa kila iitwapo leo maana
tumejua kuwa haya ndio mapenzi yao kwetu. Naomba kwa ajili yangu na uzao wangu
pamoja wote watakaosoma na kuomba pamoja. Kwa Jina la Yesu.
Amani na salama kwako.
By raphael jl:
0767033300.
KOSA ALILOFANYA ADAM WA KIUME NDIO KOSA
LINALOTAFUNA WANAUME NA NDOA NYINGI LEO.
NI KOSA NI KOSA GUMU KUJIFUNZA BAADA YA KUOA.
NI KOSA JEPESI KULIFANYIA KAZI KABLA YA KUOA.
Ø Kumbuka
kwanza kuwa, Adam wa kiume alipewa agizo moja kwa moja na Mungu. Adam wa kike
alipewa agizo na Adam. Ndio maana Adam wa kiume ni kiongozi. Lakini alikosea.
Ø So utaona
hapo kuwa sio kwamba Adam hakujua ukweli maana yeye ndio alikuwa na huo ukweli
kuliko hata adam wa kike.
Ø kwahiyo kama Adam wa kike alikosea inamaanisha
kuna namna Adamu wa kiume alikosea.
Ø Umedaka.
Lakini nachotaka kuwaonyesha hapa ni namna Adam wa kiume alizingua na kama wewe
na mimi leo hatuzingui.
Ø Adam wa
kiume aliamua kukaa kimya. Alipuuzia. Hakuzingatia. He stayed passive.
Hakujali. Hakuipa uzito. Hili ndio kosa linalotutafuna wanaume mpaka leo.
Ø Ndo maana
mpaka leo, wanaume wengi ni wapuuziaji, ni watu wa kurahisha sana mambo. Wengi
hawajali wala hawajali kutokujali kwao.
Ø wadada wengi huumizwa na hilo kwa wao wadada
wanajali sana halafu unakuta mkaka anajiona kama mdogo wake shetani. Ndo maana mahusiano mengi sana huwa
yanashikiliwa na wadada. Wakaka ni wapuuziaji sana.
Ni kitu cha
ajabu sana.
Ø Hii ndio
sababu wadada huumia zaidi ikitokea mahusiano yanavunjika. Maana kule kujali na
kufuatilia kwao kunawaweka mahali pagumu jambo baya likitokea. Na wakaka kama
kawaida anaweza asijali lolote na baada ya wiki akadaka mdada mwingine.
Ø kama wewe humu unaweza kujipime kwenye
mahusiano yako kama uko kwenye mahusiano. Angalia kiwango chako cha kujali.
Angalia kama hujamuona babu adam ndani yako.
Ø kwa mdada msg moja ya kusema unampenda inaweza
ikawa kubwa kama mlima kilimanjaro lakini wewe usione kama ni kitu. Ni akili za
kupuuzia tu.
Ø Naomba
tujadili jambo hili kama sio kweli, njoo tusemezane hapa maana wengine mko
kwenye mahusiano na ahayaendi na mnamtafuta mchawi nje.
Ø Kama pia
ulishafundishwa kanisani kwenu au kwenye huduma sijui wewe leta hapa maarifa
haya tuyapime tuone.....
Maana wengine vibuti mnajitakiwa wenyewe...
Ndo maana kilio kikubwa duniani mpaka sasa ni ukosefu wa akina baba na
waume. Sio kwamba hawapo, wapo ila wanaishi ka kosa lile la kukaa kimya na
upuuzia na kutokujali na kutokuchukua hatua.
Pastor
hapo kwenye kujali huwa kuna kazi sana hasa kwa vijana wa kilokole. Naona kama
"tunaenenda kwa imani kuliko kuona"
Ø Ninaandika
kitabu kinaitwa the passivity of Adam in the garden of eden...maana hili kosa
limevunja mahusiano na ndo nyingi sana mpaka sasa.
Ø Wala
haihusiani na imani ni upumbavu na ujinga wa kosa lile lile. Mpaka mtu aamue
vinginevyo atarithi kosa la Adam.
Ø wewe unadhani ni wakiume wangapi waliomo humu
wanaojivunia baba zao kama mama zao? Wangapi wanataka wawe akina baba kwa
watoto wao kama baba zao walivyo au walivyokuwa?
( kwa kweli wakaka tumekuwa majipu sana kwenye eneo la
mahusiano. Imani yetu sijui ni ya rangi gani!!!)
Ø Unaweza
kuwa mhubiri na mtume na nabii na mchungaji na mfanyakazi na mfanyabiashara
mzuri lakini usiwe baba au mume mzuri
Ø Unaweza
ukawa baba mzuri kwa watoto lakini ukawa kitu ch ajabu sana kwa mkeo
sio kila mwanaume ni baba
Sio kila mwanaume ni mume
Unaweza ukawa unahudumia familia yako kwa chakula na mahitaji
yote lakini usiwe baba na mume
Unaweza ukawa unawahi kurudi nyumbani kabisa lakini usiwe
baba mzuri au mume
Kumbuka baba ni kwa watoto, na mume ni kwa mke. Unaweza
kuwapenda na kuwajali watoto lakini ukampuuzia mkeo na hasa baada ya yeye kuzaa
na mwili wake kubadilika.
Ukitaka kujua akina baba na maisha yao kama kweli ni waume
wazuri, usipime kwa ubaba wao kwako. Kaa na mama, muulize kwa utulivu kama
anajivunia baba ako kuwa mumewe. Anajivunia kuolewa na baba ako? Hapo ndo
utajua ukweli maana ni rahisi kwa mwanaume kuwa baba mzuri kwa watoto lakini
sio mume mzuri kwa mkewe. Kuna vitu ni vya kufanyia kazi hakika.
(haha hahahahah) he
can be a good father to you,eating all your needs but not a good husband to
your mother....nimesema hivo kwa ukweli unaouma sana personally. Baba kivuli
huonekana jua likiwepo.
( mama yangu hawez niambie kabisa hata kama kuna hiki kitu but
ninavyowafahamu wazazi wangu kweli sioni gap kati yao.. I mean kuwa baba not
mme)
(
usijali...lengo ni kujifunza jerry haha hahahaha)
Hili ni tatizo komavu sana
Tatizo lingine kwa wanaume ni tatizo la kuzoea. Mara
nyingi wengi huwa na moyo wa kujali sana mwanzoni lakini baada ya muda, lile
kosa linazaa mazoea, kuzoea mdada na kumchukulia wa kawaida. Na huku mdada
anataka kujaliwa na kupewa muda wake.
Ø Pima kwa
asilimia utaona.....fanya kautafiti kadogo utaona
Ø Mdada
akishazaa kwa mfano, wakiume wengi sana huingia majaribuni kuanzia kipindi cha
mimba mpaka kujifungua
Ø wanaume ni rahisi sana kuvutiwa mwanzoni
kwasababu ya macho na baada ya muda macho yakishazoea kuona inakuwa shida sana.
Ø siwezi kufanya assumption ya jibu...hapo
nimefundisha tu kitu,sijasema nenda kaulize...nimekuonyesha kanuni...sasa ni
wajibu wako kufanyia kazi.
Ø Mimi mwenye
najifunza huku nafundisha, kuna mengi nimekosea kwa upumbavu wa kosa lile
lile...kuna mambo yanatakiwa yafundishwe kabla mtu hajaoa makanisani lakini ni
vigumu sana....kuna mambo utajifunza ukilia kama hukuandaliwa....maisha ya
kwenye isidingo huwezi kuayleta nyumbani,
Ø kuna vitu nilitamani nifundishwe vizuri kabla
sijaoa lakini unafundishwa kupapasana tu na kupewa vya juujuu...inabidi ukubali
kujifunza sana kwenye ndoa. Sasa kama moyo wako hauna ufahamu unaweza ukamuona
mdada ana kimbelembele na kumbe yeye ni msaidizi wako na hawezi kukaa kimya
maana ameumbiwa ustadi.
Ø Kwenye
mahusiano, akina adamu wa kiume wengi ni wabinafsi sana na huwa hawapendi
kuambiwa ukweli maana wanajisikia vibaya kwani wao uanaume ni kujua yote na
kutoshaurika. Kuna vitu kama mwanaume usipokubali kuvielewa ni heri usiwe na
mahusiano na kaa mbali na kuoa. Kama hauko tayari kukosolewa na adam wa kike
kwakuwa wewe ni mwanaume ni hatari sana.
Ø Haitakiwi
kuwa hivo...ndo maana unakuta watu wanaoana ndani ya mwaka wameshaachana maana
kuna basics lazima uzijue. Na kuna mambo ya kujifunza mwenyewe mbele ya safari.
Ni lazima kuwa na thamani ya waliotangulia mbele kama yusufu kwa wana wa israel
vinginevyo hakuna haja ya mtu kusema nilitangulia.
Ø kuambiwa ukweli na mtu unaemuona ni dhaifu
inauma sana, unaweza kumpiga mtu makofi...haha hahahahaha
( kuna salamu ambazo mwanaume huona kama kero kabisa )
lazima kukaa na
kuzungumza... Relationship diagnosis lazima ifanyike...kujua kwanini mmefika
mlipofika na kuwa very honesty
NIMEONA KUNA MJADALA HAPA....
Mchango wangu ni huu hapa...
Swali la kwanza linatakiwa liwe
kuhusu wazo kuu....goti.
ni sawa
kupiga goti kwa kila mtu au mtu yoyote. Jibu ni ndio maana kila kupiga
goti kuna maana yake kwa anaepiga na anaepigiwa.
Swali la pili...je ni sawa adam wa kiume kumpigia
magoti adam wa kike pale anapomvisha pete ya uchumba? Au kinyume chake? Jibu ni
ndio pia kwa maana ya hilo nililosema hapo juu.
Kumbe swala sio goti, wala nani hasa
kapigiwa...context yetu inataka goti la mkaka kwenda kwa mdada na sio
vinginevyo.
Kwenye mantiki hiyo lazima tuanze kuchambua kama
ifuatavyo:
1. Tambua mamlaka yako
inayoruhusu au kukataza vitu-hapa tunakubali kuwa biblia au mungu ndiyo mamlaka
ya juu na ya mwisho kabisa. Je imesema kitu kuhusu hili? Hapana. Yenyewe
imesema kila goti litapigwa kwa yesu na sio kwa mwanadamu,sembuse mpenzi. Kama
biblia iko kimya kwenye jambo huwa tunategemea sana maongozi ya roho mtakatifu
na kama yeye hajasema basi tunaenda pointi number 2.
2. Mila, tamaduni na
desturi za wakati na jamii husika. Hizi ndio chimbuko la mambo mengi sana ya
ajabu ajabu na saha kwenye ulimwengu wa sasa ambao umejaa mitandao ya kijamii.
Mfano, kupiga goti kiulaya ni tofauti sana na kupiga goti kiafrika.
kwa afrika goti ni moja
ya ishara za heshima na utii wa juu. Yaani ukikuatana na mkubwa wako na ukawa
unamsalimia au anakupa kitu ni wazi kuwa jamii nyingi sana huku kwetu goti ni
moja ya ishara ya utii na heshima.
Kabila na kabila inaweza kuwa tofauti lakini wazo kuu
litabaki kuwa lile lile.
Kwa picha hii goti linauhusiano na heshima au utii kwa
maana ya ukubwa.
Kupiga goti imeenda hata makanisani ambako wapo
wanaowapigia magoti wachungaji , manabii wao au mitume wao na kwao hiyo ni
ishara ya kunyeyenyekea na kutii hiyo mamlaka anayoipigia goti.
Watu wanapiga magoti mbele ya misalaba, mbele ya
madhabahu, mbele ya chochote ambacho kwake kimepewa maana na tafsiri hiyo ya
ukuu unaostahili heshima ya mpaka kupiga goti.
lakini ukisoma
historia mbali mbali utaona ni ulaya ndio ilianza na mtindo huu wa mkaka
kumpigia goti binti akiwa anaomba uchumba. Ni kwenye karne ya 18-19 huko. Haijulikana sana nini kilikuwa ni sababu
nyuma yake lakini wengi walioandika wanaonyesha ni heshima na utii na kujikabidhi.
Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa jambo hili
liliingiaje makanisani?
hatuna
kumbukumbu ya kanisa gani lilianza rasmi kuwapigisha magoti wa hata
kuwafundisha wakaka kupiga magoti.
kwakuwa dunia
imekuwa inaonyesha mambo mengi inayofanya kupitia mitandao ya kijamii basi
makanisani walijikuta tayari wameshaanza kupiga magoti hata bila kujifunza
kujua kwanini.
Tanzania the same...na hapa niseme hivi...
(umaarufu
sio kipimo cha usahihi).
kuna watu maarufu au
mitume na manabii maarufu au wachungaji maarufu wamekuwa wakifanya kama hivyo na
hiyo haimaanishi kuwa jambo hilo ni sahihi.
(usahihi haupimwi na nani anafanya.)
Sasa twende kwenye biblia niwaonye vitu vya kustusha
sana....
(kupiga goti pia kumechochewa na
michezo ya "isidingo" na zile za 'la mujee de vida' za itv enzi hizo)
Waefeso
5:25-27
“ enyi waume, wapendeni wake
zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na
kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa Tukufu,
lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo
na mawaa
Waefeso 5:22-24
“enyi wake, watiini waume
zenu kama kumtii bwana wetu.
23 kwa maana mume ni kichwa
cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni Mwokozi wa mwili.
24 lakini kama vile kanisa limtiivyo
Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.”
Akina Adam wa kiume wote wamepewa agizo la kuwapenda
wake zao maana hii ndio shida yao kubwa. Kutoka kwenye kosa lileee ambalo
tumeliona.
Akina adam wa kike wameagizwa kuwatii waume zao. Pia
rudi kwenye lile kosa.
Ishara ya upendo ni kujitoa. Ishara ya utii ni
kunyenyekea.
( mimi wakati naoa sikupiga goti maana hata ajenda ya
goti haikuwepo. Pili hata kama ningekuwa nao leo nisingipega goti, sio
kwasababu simpendi mke wangu au siwezi kupiga goti bali sitaki kuingilia kazi
za watu.)
Wajibu wangu ni kumpenda mke wangu. Na wajibu wake ni
kuniheshimu.
Natakiwa nimpende kama kristo anavyolipenda kanisa. Na
mwanamke anatakiwa kumtii mumewe kama kumtii bwana.
Mume ni kichwa cha mkewe...kichwa kimechanganyikiwa
sasa.
Biblia inasema mume ni kichwa cha mkewe, yaani ndio
kiongozi na ndio foundation ya mke kwa mfano ule ule wa adam wa kike na wa
kiume. Adam alipokaa kimya, mwanamke alikosea na kumkosesha na mwanaume pia
Ila najua
makanisa na huduma za kisasa zinaruhusu hivo vitu kwani they have nothing to
loose..basi hata wangefundisha implication za kupiga goti ili watu wajue na
waamue....
Jambo hili la kupiga goti limeshavunja mahusiano mengi
sana maana wadada wanalipenda, wanalitaka, wanalitamani sana maana lina roho ya
haki sawa ndani yake....ila ukimkuta binti aliyefundishwa misingi
vizuri...hawezi kukubali apigiwe goti na mkaka
Kanisa la
leo linaenda na fashion, shows na mionekano kama dunia inavyofanya. Ndio maana
utaona watu wanapiga picha wanafungana viatu au anazuga anamvisha kiatu mdada
ili picha zipigwe na ili dunia ionyeshwe kuwa hawa wawili ni lovebirds....vitu
vingi vimejaa maonyesho sana leo....roho ya sabasaba na nanenane imelivaa
kanisa. Mitandao ya kijamii itatumaliza.
Imefika mahali
kanisa linatafsiri social media kuwa ndio standard na wewe kama humpost mkeo au
mpenzi wako na zile picha zenu za kukumbatiana basi inaonekana kama hujui
kupenda. Ndio maana kiwango cha uzinzi na uasherati kimeongezeka makanisani na
kwenye huduma kibao za kikristo mapaka ukristo unapoteza ladha yake.
Ishi maisha yako kama mtu aliyejitambua. Kubali
kuongozwa na mungu.
Ila niseme hivi
kama wewe una mdada na unatarajia kumvisha pete hivi
karibuni......................
Ili ujue kuwa swala hili la pete lina roho ya
haki sawa jaribu kuongoea nae uone mtazamo wake...jifanye kama wewe uko tayari
kupiga goti ili uuone moyo wake umejaa nini...kisha anza kuongea nae kwa
kumuonyesha implication ya goti kama tulivyosoma kwa waefeso.....
Kuna wadada wanasubiria kupigiwa magoti kuliko
wanavyomgonja yesu arudi.
akili za
kuegesha zio za kuziamini kabisa.
Jiulize umegipa magoti mbele za mungu mara ngapi? Hata
basi kwa kujionyesha. Unamuheshimu mungu kwa kiwango gni ndani yako?
kinachoendelea
sasahivi makanisani ni showoff za kijinga na kujionyesha kwa ajili ya picha.
kama kweli
unaelekea kuoa hivi karibuni, hilo la goti mlizungumze tu mapema ili menzio
asije akawa amesimama anasubiria uiname...usije ukaharibu sherehe za watu
Lakini
hakikisha vyote vimepiga goti...moyo na goti lenyewe....visipoendana step
itagoma.
kikubwa zaidi
ya yote: zungumza na mdada kwanza. Wadada wameshamezeshwa sumu za goti na
makungwi kwenye kiwango ambacho usipokuwa makini utajikuta kungwi na assistant
wife. Zipo sumu zinaua haraka na zingine zinaua polepoleeee kama kwinini
inavyoingia mwilini.
wajibu wetu
kama akina adamu wa kiume ni kuwapenda wake zetu...
.PIMA KWENYE HAYA MAMBO NANE (8)
1. Upende
moyo wake-yaani sehemu ya mihemko na hisia zake.
2. Mpende akili zake, yaani ufahamu wake
3. Mpende mwili wake,lazima akuvutie aiseeeee
4.Ipende
nafsi yake, yaani mambo ya roho yake
5. Yapende mahusiano yake, nae ana watu wa karibu
kama wewe ambao umemkuta nao,sio wote hawafai kama ilivyo kwako pia
6. Penda
uvumilivu wake, wanawake wamejaliwa kuvumilia sana.
7. Penda wito
wake, yeye ni msaidizi...mpe heshima ya nafasi yake.
8. Mpende
muumba wake.
Fanya hayo nane uone kama mdada anachomoka mikononi
mwako hata awe amekuzidi kila kitu.
Kusudi ni
usaidizi...hata awe mkurugenzi wa tiss bado kwa mume wake yeye ni msaidizi.
Every ability she has is to make her the best helper
to her husband.
“when god
says, “husbands, love your wives,” he speaks of the woman as a complex being.
He calls every man to love his whole wife just as every man loves his whole
self (eph. 5:29). This means that a husband must do all he can to understand
his wife’s world. What follows are eight admonitions to love our wives with
respect to their various facets.”
Lets dig deep....
1. Love her
heart—emotional love
The bible uses
the word “love” over 350 times. Almost 10% of these times are in the song of solomon (which comprises less than 0.5
percent of scripture). One thing we learn from this is that a husband should
use words to express his love for his wife. “rise up, my love, my fair one, and
come away! O my dove…let me see your face, let me hear your voice; for your
voice is sweet, and your face is lovely” (song 2:10). I know of no woman who
wouldn’t love to hear her husband speak to her like that. But this is not
easy,there is a price to pay too.
If you are ready to learn and make a change you must
experience the difference.
Imagine living with a woman you dont appreciate for
the rest of your life.
love her mind—intellectual love
A loving husband
graciously convinces his wife that, to him, she is the most important person in
the world. By this i don’t mean that he persuades her that he will never leave
her. That’s not good enough, of course. Does your wife know that you value her
above all else? Intellectual love also means engaging your wife’s mind. Many
men win the hand of their future wife by thoughtful, engaging, conversation.
Too many men fail to take this habit into marriage. I myself learnt this a hard
way.
This is the reason why most men will find it difficulty to go
with ladies who are educated than themselves.
Kuupenda ufahamu wake na huku unaogopa kuwa
challenged?? Unataka mdada wa kusukuma tu kila unachotaka.
hapo sio tena
uko kwenye mahusiano na mtu bali robot sophia.
Unauzima tu but yahitaji hekima sana maana sumu
ikishaingia mwilini ni kazi sana
maombi pamoja na
ufahamu.
Mwl wangu mchungaji wangu na mtumishi wa mungu raphael jl !!
Na vijana wenzangu humu ndani.
Jana nilileta mada ya ni nani anapaswa kupiga magoti
wakati wa kuvishana pete ya uchumba kanisani. Upishano huu ulitoka kwwnye group
la vijana wa kanisa ninalomuabudu Mungu la Calvary Assemblies of God (CAG)
morogoro. Ubishani ulikuwa mkubwa sana
nikaona niulete huku ili nipate pia mawazo.
Nashukuru wengi tulichangia lakini mwl wetu pastor
raphael akaja na kutufafanulia kuanzia mwanzo hadi mwisho vizuri.
Nikachukua fafanuzi za mwl zooote kuanzia ya kwanza
hadi ya mwisho nikaipost kwenye group lililoanzia ule ubishani.
Hakika wamebarikiwa sana na maneno ya mwl wetu na ufafanuzi
wake wa hekima na kiMungu.
Hizi hapa zifuatazo ni baadhi tuu ya shuhuda za haya
niliyosema.
Ubarikiwe mwl na mbarikiwe nyote kwa kushiriki.
Naomba radhi kama nitakuwa nimekosea katika hili.
( asante Yesu kwa ushuhuda huu)
Amebarikiwa utakaemuoa
na watoto utakaozaa
Umewasaidia wengi sana
kwa kuwashirikisha mambo haya
Asifiwe Bwana Yesu zaidi ya wote na yote
Mwanaume mmoja akikubali kujifunza na kubadilika ujue
umeokoa ukoo mzima
kuna wakaka ni
wagumu sana hata kumwambia mpenzi wake nakupenda
Mindset upgrade:
1 wathesalonike 4:7, maana Mungu
hakutuitia uchafu bali tuwe katika utakaso. Lolote lililo chafu sio sehemu
yetu, tuepuke na kukaa mbali na uchafu wote kuanzia kwenye fikra mpaka mwilini.
Mapenzi ya Mungu ni sisi kutakaswa. Kila unaposhuhudiwa uovu, kosa au dhambi
tubu hapo hapo. Don’t accumulate sin for repentance, ukisubiri jumapili ni
lazima ujue pia sio kila siku ni jumapili. Utusamehe makosa yetu
Nia ile ile, kama ya Kristo.
Ykm-satisfied in Jesus!
Basi kutoka
pale...utaona kuwa nafasi ya mwanaume ni muhimu sana
Mwanaume akikaa kimya anaharibu mfumo mzima
Ni tabia mbaya sana kupuuzia
kurahisisha
kuchukulia poa
ni vema
unapoanza mahusiano yako ukaelewa kuwa wewe n huyo mdada mko tofauti sana
mmezaliwa
tofauti
Mmekulia mazingira tofauti na hivyo hulka zenu ni
tofauti pia
Vipimo vya hisia zenu ni tofauti
Kuchukulia na kuyaelewa mambo ni tofauti pia sana
Wadada huguswa sana na hisia na mihemko ya kusikia na
kuambiwa
Ni lazima mkaka uwe tayari kujifunza, kufundisha na
kufundishwa
lazima ukubali
kuwa kuna vitu hujui, huwezi kujua kila kitu
Uko tayari kufundishwa?
Upo uzembe katikati ya vijana wa kiume ambao
unawaumiza sana wadada na hasa kama wewe mkaka uliyemo humu tayari una
mpenzi...
Angalia sana usiingie kwenye upuuziaji na kutokujali
ambako kutamuumiza mdada na mwisho kuyaumiza mahusiano yenu kwa ujumla
Moja kati ya maeneo ambayo kwa sasa yanasumbua vijana
wa kiume wakiwa kwenye mahusiano ni mawasiliano
Wakati wewe mdada akishakukubalia unaona umemaliza,
wadada huwa ndio mwanzo wa safari
Mdada angependa umwambie unavyojisikia kuhusu yeye hata
mara mia kwa siku
Umwambie unampenda kadri unavyoweza
Lakini sasa wewe unajifanya mgumu
Kama vile huna hisia kabisa
Kuna ugumu gani wa wewe kujiweka wazi hisia zako za
mapenzi kwa mdada uliamua kumuoa?????????
Wewe unaitazama kama kuwatetea, mimi naitazama kutoka
kwenye nafasi yako wewe kama mwanaume. Sasa mimi nitawatetea wanini wakati
nilishaoa? Wewe unaona ni kuwatetea ila mimi nakuonyesha common errors ambazo
wanaume wanafanya na kuwalazimisha wadada kukosea na kuharibu.
Hata hilo unalosema la wakiambiwa taarifa mbaya
inategemea wewe umemfundish nini na anaona nini toka kwako kila siku. Kama
unaishi nae katika namna ambayo hakuamini kwa maneno na matendo yako basi ujue
haki utavuna.
Badala ya kusubiria uone hicho unachokisema wewe kwa
maana ya hiyo hatari yao ni heri uamue kumfudisha. Ili ajue wewe ndio mwenye
taarifa sahihi na sio radio mbao za mtaani.
Naona Herman ameamua kuuona ubaya wao. Kila kitu
kinatengenezwa, uzuri au ubaya unatengenezwa pia. Wewe umeamua kutegeneza nini?
Wanawake wangekuwa wabaya hivo mungu asingewapa nafasi
ya usaidizi. Ila kila eneo ambapo mwanaume hatakaa kwenye nafasi yake ni lazima
mwanamke atakosea.
Everything is made my friends.
Mambo hayatokei tu wala hayaibuki tu.
Usipotengeneza wewe basi ujue kuna watu watatengeneza
huko nje na mwisho utalumu kuwa mwanamke ni shida.
Bila mungu ndani ya moyo wa bidamu yoyote, awe mkaka
au mdada sio mtu mzuri hata kidogo.
Ni lazima ukubali pia nafasi ambayo mungu amekupa.
Kumwelewa mwanamke nje ya mungu ni kujichosha sana
Unaona sasa hahaha hahah ili kumjua mwanamke ni lazima
ujue akili za mungu kumleta kama msaidizi na huko ndiko tumeanzia.
Juzi nilitaka kuwauliza wale walio na wapenzi wao...je
huwa unamwambia unavyompenda mara kwa mara au unauchuna tu maana wewe ni mbabe
huwezi kujishusha?
Sasa wewe endelea kujifanya husemi...ujue unampa fursa
mwingine akijitokeza akaanza kusema usije ukaanza kutia huruma mkuu.
Naomba mfahamu hili hapa......
Wanawake wanatafsiri upendo kwa kumjali, kumjali ni
pamoja na kumsikiliza, kumwambia maneno matamu matamu, kumpa muda na kuwa hapo
akikuhitaji. Yaani hata Kama uko busy ukimwambia tu uko busy kwake ni upendo
mkubwa sana.
Kwani nyie wenye wapenzi leo umemwambia unampenda? Au
wewe unaona kusema hivo ni kujishusha? Au ni kujidhalilisha? Au ni kujipunguzia
heshima?
Karibuni kwa maswali na mazungumzo sasa.
Niseme hivi, lolote jema unalopaswa kulifanya kwa
mpenzi wako, usipolifanya uwe na uhakika kuwa akitokea mwanaume mwingine
akalifanya kwa bidii utakuja kusema mwanamke ni msaliti na kumbe wewe ulisimama
kwenye nafasi ya adam pale bustanini... Hakika usikikose kitabu changu kipya
cha the passivity of Adam in the garden of eden.
Komaa my friend...lazima atakuwa anajivunia sana kuwa
na wewe. Yaani ukitaka kumuweza na kumtuliza mwanamke wewe mjali tu. Care for
her.
Kumbe kusema "nakupenda" inabidi liwe zoezi
endelevu kama la kupumua
Lazima uwe na
kazi ya kukuingizia kipato.
Wanawake wa
ukweli hawataki pesa nyingi wanataka pesa zilizo na moyo wa kujali.
Mtakuwa mnakutania kwa mzee wa kanisa?
Sio muda wote utapiga simu na sio muda wote utatuma
sms. Period.
Mwanake anahitaji mwanaume mwenye mungu, mwanaume
anaeijua nfasi yake na kuitendea haki.
ubaya wa
wanawake wengi huwa unatengenezwa na wanaume kutokujitambua.
Mwanaume ambaye hajajitambua ni hatari kuliko sumu.
Wekeza allan, wawekezaji wa nje wanabebaga na
kuhamisha migodi haha hahahah look you very very
Kwanza niwapongeze sana wale wenye wapenzi wao na
wanatarajia kuoa mwaka huu au mwakani, naamini hamchoki kuwa masaprize ya
upendo wenu wala msichoke...wapendeni...ni haki ya mwanamke kupendwa kibilia na
ni haki yako wewe mwanaume kuheshiimiwa. Hata sasa yaani unaweza ukamtumia msg
ya kumpenda tu maana sasa utamwambia nani mwingine?
hata kama wewe
ni mwanajeshi haha hahahah hahaha the easiest way to win a lady is to care for
her...na wala usisahau kuwa usipofanya wewe mwenye mpenzi ujue wawekezaji wa
nje watafanya na wao huwa wananunua mgodi kabisa, wanabeba na mchanga wanaenda
kuchambulia kwao, so be very careful. Naamini wewe adam wa kiume unanielewa sana.
Unachomfanyia mdada huwa kinatabia ya kuwa kama mbegu
ambayo itazaa mpaka utachukia au kupenda. Mfano ukimjali atakuheshimu mpaka
unaweza kuboreka.
Ogopa wawekezaji wa nje kwa mpenzi wako ndugu yangu
Pambana.
Kumbuka: no
sex before marriage ndo msingi wa mahusiano matakatifu...nitaliongelea hili
vizuri huko mbele. Ila kwa sasa mtunze na mjitunze. Utakaa nae mpaka kufa huyo
so usione haraka kuanza mambo ya chumbani na mko sebuleni bado. Jizuie.
Nakazia sana hii pointi...ninaamini kuna mtu anavuka
pakubwa sana....wekeza kwa mpenzi wako....usione haya umwambia unampenda na
unayomuwazia yanayomtukuza mungu...ajue unamuombea na unajali maisha yake...ni
gharama kiasi gani kumwambia mdada unaetaka kuishi nae vile unajisikia juu
yake?
Naomba niweke angalizo hapa.....
Ni muhimu sana kuweka mipaka ii usijikute umekosea
katika caring yako. Mipaka ni kwa faida ya wote wawili. Ndo maana lazima
msaidiane, tutajifunza namna ya kufanya hili hapo mbele.
kama nilivosema huko
nyuma,wanaume wengi wanakutwa na changamoto ya kutokujali,kupuuzia,kutokuzingiatia,kurahishisha
mambo na kuyachukulia poa...hili ndio kosa alilofanya adam wa kiume pale
bustanini lakini matokeo yake hayakumuacha salama yeye wala mkewe.
Lakini pia nimeonyesha wazawazi kuwa kukosea kwingi kwa mwanamke kunatengenezwa
na wanaume,laiti kama wanaume wangekuwa wanasimama katika zamu zao kwa kujua
nafasi yao na kuisimamia basi ni wazi
wangeokoa familia nyingi sana.
Pia nimeonyesha kuwa kama wewe mwanaume hutafanya unayopaswa kufanya
kwa adam wa kike unaetaka kumuoa uwe na uhakika kuwa wapo wawekezaji wa nje
ambao watawekeza kwake na wewe utaanza kuona kidogokidogo moyo wake unaanza
kutoka kwako na kuhamia kwa mwekezaji. Usisahau kuwa wawekezaji wa nje huwa
wana tabia ya kubeba hata mchanga na kukuachia wewe mashimo ambayo yatatunza
maji wakati wa mvua.
Nilikuonyesha pia umuhimu wa mawasiliano kwamba kutoa taarifa ya jambo
unalofanya ni muhimu sana. Mdada anakuwa anasubiria kusikia kutoka kwako,
akikupigia na usipopokea basi tuma hata msg. Kama unajua hutapatikana basi toa
taarifa mapema ama sivyo utalaumiwa sana baadae na kwake yeye ataona na
kutafsiri kuwa wewe hujali.
Nilionyesha pia kwa mdada upendo ni kujali. Usipojali wewe,utasaidiwa
na usilalamike wala usiseme hujaambiwa.
HAPA
HATULAZI KIPORO...TUNAJIFUNZA ILI TUONE MABADILIKO NA NDIO MAANA NAWASIHI SANA
KUFANYA KWA VITENDO..WENYE BIDII WATAFURAHIA SANA
Ukipanda mawasiliano kwa mdada hakika hutajuta maana
atakurudishia mara dufu.
mfano...hujazoea kuwasiliana mara baada ya
kuamka...anza leo
Hujazoa kusema unaondoka kwenda kazini....anza leo
Hujazoea kusema unaenda kula mchana ...anza leo
Mfanyie suprize hata ya kumnunulia vocha ya buku au
mtokee uso kwa uso kama uko kwenye mazingira ya kuonana....
Be
unpredictable
Unataka kufurahia maisha ya ndoa? Jenga urafikia wa
kiwango cha kipumbavu haha hahahahahaa
kumbuka ile
point.....everything is made...kila kitu kinatengenezwa...kiwe kibaya au
kizuri.
Naomba nilete audio ya pili ambayo pia muitime kwa
wale wenye mahusiano...ni nzuri sana...very powerful
Mengi ninayowafundisha mimi nimejifunza kwa machozi
lakini ukivuka unajicheka kabisaaaa hha haha hahaha haha
RECKLESS LOVE OF GOD
Kujilipua pwaaaaa haha hahahaha a leader has no
private or public life, a leader lives both life all the time.
kweli inatuweka
huru.
wewe unataka
kukutana na Adam wa kike iwe hotelini khaaaaaaaaaaaaaa unatafuta nini wewe adam
wa kiume? Unataka aje mpaka room...mnataka kuombamaombi ya vita? Uhuru bila
mipaka ni uharibifu.
Hapa ulishavuka tayari sasa. Celebrate your victory
with the one you have now. Lipiza kisasi, kwenye eneo kama hili kisasi sio cha
bwana hahahahaha maana bwana haoi ujue.
Ukiviona vya kawaida unampa shavu muwekezaji wa nje
hhaahaha hahahahaha
Jifunze kufanya jambo la kawaida kwa namna isiyo ya
kawaida uone kama adam wa kike atafurukuta.
Yote yanawezekana maana hiyo sio tabia ya mdada wa
ukweli.
A good communicator
ULISHAWAHI KUWAZA KUOA MTU ASIEAMINI UNACHOAMINI AU USIEAMINI ANACHOAMINI?
ikawaje?
Eti wewe jumapili unaenda kusali kwa budha halafu yeye
na watoto wanaenda kusali kwa wahindu....
kuna kitu
natamani mkifhamu leo na kwa umuhiu wake naleta hapa audio
Yaani hakuna taasisi ya maana na yenye nguvu duniani
kama familia.
Familia ikipigwa hakuna kanisa linabaki salama.
Familia ikipigwa hakuna taifa linabaki salama.
Familia ikipigwa hakuna taasisi inabaki salama
Familia ikivurugwa hakuna jambo la kimaendeleo
litakaloonekana kufaa kitu.
Familia ikipigwa ni moyo wa mungu umepigwa
Family is the si unit of everything. Yaani ukichezea
familia ndugu daaaaaaaah
Sasa unakumbuka tulikotoka pale edeni? Familia
ilipigwa.
Adam wote wawili walivurugwa. Wakajivuruga.
Wakavurugika. Familia ikapigwa.
Nini kiliivuruga familia ya kwanza duniani? Taarifa na
kutokusimama kwenye nafasi. Nani hakusimama kwenye nafasi? Adamu wa kiume. Nani
alivurugwa na taarifa,adamu wa kike. Hapa kuna siri nzito sanaa katika kujenga
au kubomoa familia.
Hii inamaanisha kuwa katika familia, mwanamke ni
rahisi sana kuharibiwa na kuiharibu familia yake kwa taarifa anazosikia au
anazoona. Na mwanaume kwa kutokukaa kwenye nafasi yake.
Mwanaume
akikaa kwenye nafasi yake,anaweza kumsaidia adam wa kike hata kama ana taarifa
za uongo. Lakini kama adam wa kiume hayuko kwenye nafasi inahiaji neema sana
ili adam wa kike hata kama ana taarifa sahihi kuweza kuifanya familia ikae sawa.
Ndo maana ukiwa na adam wa kike ambaye hajui namna ya
kutawala maneno ya watu (taarifa) halafu na wewe ukawa hujajitambua kama adam
wa kiume, hapo ni uharibifu tu.
Ukiwa na adam wa kike ambaye anasikiliza maneno ya
watu kuliko anavyokuamini wewe ujue utapata tabu ya kukutosha.
ADAM WA KIUME NA CHANGAMOTO YA
MAWASILIANO.
1. Mawasiliano yenyewe kwa ujumla
2. Namna ya
kuwasiliana
3. Vya kuwasiiana
4. Mtazamo wa kimawasiliano kwa adam wote wawili
Jiwe:Ni aibu kuachwa au kumuacha Adam wa kike
au kuvunjwa au kuvunja mahusiano kwasababu hujui namna ya kuwasiliana nae.
Unaendekeza ubabe na sijui wewe kabila letu mnaongeaga kama mko vitani. Fahamu
kwamba Adam wa kike wa leo hawajui hayo mavita. Mtu akikusikia unaongea na Adam
wako wa kike akishindwa kutofautisha na kama unaongea na mlinzi basi ujue wewe
umevaa koti la upupu. Nitarudi nasema.
Familia isiyo na mawasiliano ni familia iliyokufa.
familia isiyo
na mawasiliano mazuri ni familia ambayo vita na malumbano havitaisha kamwe na
mwisho ni kuachana.
Mawasiliano ni kiini cha uhai wa familia lakini issue
sio tu kuwasiliana ila unawasilianaje na unawasiliana nini na unawasiliana na
nani na unawasiliana muda gani na kwa kiwango gani.
Naomba nisisitize jamani-Adam wa kike wanapenda
kudekezwa.
Adam wa kike wanapenda kudekezwa. Namna
unavyowasiliana nae inatafsiri mambo mengi sana zaidi ya kile unachokiona wewe.
No woman is powerful in front of a caring
man.
Every woman
is powerless before a caring man.
Hauna mwanamke mwenye nguvu mbele ya mwanaume
anaejali.
Kila mwanamke ni dhaifu mbele ya mwanaume anaejali.
Kama unabisha,jaribu kujali kwa wiki moja halafu
jaribu kutokujali kwa wiki moja.
Niliwaambia juzi kuwa adam wa kike wanapenda kusikia
sana, anataka asikie anavyopendwa, hata kama sio kila mara lakini awe ana
uhakika kuwa anapendwa. Kusema tu siku umemtongoza kuwa unampenda kwake ndo
mchakato unaanza wa kusikia anapendwa kila siku. Asiposikia wewe unasema mambo
mawili yatatokea....
Moja atajua una mtu mwingine anaeambiwa kupendwa zaidi
yake kwani kila mwanamke anataka kusikia hilo neno na kudekezwa. Na pili
atatafuta mtu mwingine wa kumdekeza kitu ambacho hutakifurahia.
Ndo ujifunze sasa humu humu...mimi mwenyewe nimekuzwa
na baba ambae sijawahi kusikia hata neno moja la kunipenda toka kwake. Lakini
inabidi nijifunze ili mke wangu asijute kuwa na mimi na watoto wangu wamtukuze
mungu mimi kuwa baba yao.
Wakaka wengi hujilaumu wakati wameshachelewa, sasahivi
unaweza ukajifanya uko busy na ndo maana huna muda wa kumwambia mdada vile
unampenda lakini nikwambie moyo wa mwanamke ukichoka na kuchoshwa utaumia sana
wewe.
Nawashauri wakaka mliomo humu, msiwachukulie poa
wadada mlio nao. Usione ataenda wapi sasa na anakupenda wewe,kumbuka kupenda ni
kuchagua yupi wa kumpenda. Akiondoka utaumia sana ukijua kuwa ulichezea dhahabu
mkononi mwako.
mawasiliano....je leo umewasiliana nae?
Umewasiliana nae kwa namna ya kumfanya ajione
anapendwa au anachukiwa au ajione yuko kambi ya jeshi ya makutupola?
Umewasiiana nae nini?
Mimi huu ni mwaka wa 10 toka nifunge ndoa lakini kila siku
ni kama mwanafunzi kwa huyu mdada niliyenae...na hata leo nimemwambia
ninavyompenda....sasa wewe mkaka hata mwezi hujamaliza hata mwaka hujamaliza na
hata kama ungekuwa umemaliza miaka lakini ina kugharimu nni kuwasiliana nae kwa
upole kama mpenzi wako?
Tatizo la Adam wa kiume ni
lilelile...umwamba...kutokujali...kurahisisha...kuchukulia poa...kuona mdada
ataenda wapi...kiburi cha uzima kinawamaliza akina adam wa kiume wengi
sana na mahusiano mengi yako
kisungusungu badala ya upendo wa dhati.
Mtu unaempenda kweli utataka uwasiliane nae mara kwa
mara...hebu angalia namna unavyowasiliana nae huyo mpenzi wako kama unae uone
kama kwa staili hiyo utadumu nae na kile kiapo cha mpaka kifo kiwatenge au
mmeshatengwa na ubabe na kutokujali?
mimi ntawaambia
ukweli tu ambao unaweza ukawa unauma lakini unaponya ukiamua kupona.
pastor kasema 10yrs bado anaelezea namna anampenda.
So sahau kuhusu kukata
tamaa hadi kieleweke mzee
Imagine bishop ryoba still anambembeleza mama hadi leo.
Sie ndo kwanza panakucha mzee
Kila mtu na mtu wake na mazingira yao.
Kama hajali ujue huyo sio adam wa kike maana maadamu
wa kike wote wanapenda na kutaka kujaliwa sana. Hapo ni pa kuchunguza sana. Si
kawaida hiyo.
Bonge la mzee....namkubali moja kwa moja na
ninamfahamu sana
Sasa nyinyi
mliochini ya huyu mzee nitawashangaa sana kama hamuwadekezi wapenzi wenu kama
mnao lakini. Nitawashangaaaaa sana maana yule mzee yuko wazi sana upendo wake
kwa mkewe na wote ni wazee jamani. Tujifunze.
Ugumu wa kuwasiliana unatoka wapi? Mbona wadada wengine
unachat nao yaani isipokuwa yule unaetaka kuishi nae mpaka kifo kiwatenge ndo
hutaki uwasiliana nae?
mdada
anakuuliza...mpenzi unanijali?....wewe unakuja na jibu lako la
kimgambo....kwani nani kakwambia sikujali....haha hahah hahaha nakukemea kwa
jina la yesu
Mahusiano mengi yanavunjika sio kwasababu waliopendana
sio watu sahihi, bali wengi wamekosa maarifa ya kuishi ndani ya mahusiano na
hawako tayari kujifunza.
Ndo maana huwa hata ni vigumu kujua kama ni mapenzi ya
mungu au hila za shetani watu wameachana kwani kuna mambo ya kijinga na kizembe
sana ambayo hufanywa kwenye mahusiano likiwemola adam wa kiume kupuuzia wajibu
wake.
mimi nawaambia
ukweli ambao baada ya kutoka humu aidha utafurahia sana au utabaki kijilaumu
sana.
hayo ndioo
maisha ya mapenzi. Ni full kupendana. Full kuambiana unavyompenda maana ni huyo
tu mmoja utakeishi nae. Huna mwingine wa kumwambia maneno hayo. Wekeza mwaya.
Hebu chunguza mawasiliano yako maana unaweza ukawa una
jambo zuri kabisa unataka kuwasilisha lakini ukakosea kwenye namna...namna ya
kuongea...ukakosea kwenye kuchagua maneno haha hahahah utachukiwa sana
nakwambia.
Badilisha mtazamo wako mpendwa.
Maisha ya ndoa ni maisha ya kirafiki,sio maisha ya
kambini.
Hebu usiku huu fanya kwa tofauti basi...
Kujiweka wazi kwa mtu unaeenda kumuoa haimaanishi kuwa
wewe ni dhaifu
Hebu soma hapa uone.....mwanzo 2:23...angalia hayo
maneno yanamtoka adamu wa kiume baada ya kumuona adamu wa kike....sembuse wewe
mkuu? Au ni cheo kinasumbua? Au ni kabila? Au ni ukoo? Au ni elimu? Au ni pesa?
Au ni ujinga? Au ni ulimbukeni? Funguka kwa jina la yesu.
Sasa wewe leo unashindwa kujilipua tu kwa kuwasiliana
na mtu wako na kumpa maneno ya upendo gb500...unaishia kumjibu vibaya...kisa
hutaki tu kusema unavyompenda...sasa ulienda kumtongoza ili iweje? Ili umuumize
au ili aendelee kusikia kupendwa akiangalia tamthilia?
Ndo maana watu huchelewa kuoa hivo hivo.
Kama nimekukwaza, natubu. Ila sifuti nilichoandika.
Naamini kuna kusaidika.
Halafu mpaka leo kuna wakaka wanalalamika kuwa wadada
wanafundishwa sana kuliko wao, semina nyingi ni za wadada....basi tujifunze tu
wakuu.
Hii ni kwa faida ya mke wako ajae na watoto wako.
Familia yaani.
SABABU ZA MSINGI ZINAZOPELEKEA MAHUSIANO MENGI YALIYOSAHIHI KUVUNJIKA
§
Kama Wewe Adam Wa Kiume Uko Kwenye Mahusaino Leo
Hebu Jaribu Kuangalia Uhalisia Wa Jambo Hili Kama Litakuwa Mbali Na Ukweli Hata
Kwako Pia. Kuna Namna Wewe Kama Mwanaume Usiposimama Kwenye Nafasi Yako Ni
Vigumu Sana Kuyasimamisha Mahusiano Mpaka Mwisho.
§
Ukweli Huu Ni Unpingikable Ingawa Mkaka Anaweza
Kupinga Kwa Haraka Lakini Ukitoa Fursa Ya Kujifunza Utagundua Kuwa Adam Wa
Kiume Wana Nafasi Kubwa Sana Ya Kuyafanya Mahusiano Yasimame Imara Au
Yasambaratike. Hii, Kwa Sehemu Inasababishwa Pia Na Kosa Lile Lile La Mwanzo 3:1-13 Ambalo Tumeshalizungumza
Sana Lakini Kwa Ufupi Ni Lile Kosa La Adam Kutokupatikana Kwenye Nafasi Yake,
Kosa La Kupuuzia, Kosa La Kupotezea, Kosa La Kurahisisha Mambo, Kosa La
Kutokujali.
§
Kwanza Niseme, Wakaka Wamekuwa Sababu Kubwa Sana
Ya Mahusiano Mengi Kuvunjika. Yaani Hapo Wakaka Kama Taasisi Ukilinganisha Na
Wadada. Mahusiano Mengi Yaliyovunjika
Utakuta Adam Wa Kiume Kuna Namna Alizingua.
§
Jambo La
Pili, Kumbuka Hapa Naongelea Kuvunjika Kwa Mahusiano Sahihi, Siongelei
Mahusiano Yasiyo Sahihi Ambayo Sina Hata Haja Ya Kuyazungumzia Kwani Hayana
Mahali Yanaenda. Kwahiyo Nataka Tukae Hapo Kwenye Mahusiano Sahihi Tukijua Kuwa
Katika Mauhusiano Yanayovnjika Kila Siku Yapo Mengi Ambayo Ni Sahihi Kuliko
Yasiyosahihi.
§
Uchunguzi
Wangu Usio Rasmi Unaonyesha Kuwa Wakaka Wanachangia Mpaka Asilimia 80 Ya
Mahusiano Kuwa Imara Au Kuliwa Na Madumadu. Na Pia Uchunguzi Wangu Usio Rasmi
Umenipa Kujua Sababu Ambazo Zinapelekea Mahusiano Mengi Yaliyo Sahihi
Kuvunjika.
§
Jambo La
Tatu, Ni Vema Kufahamu Kuwa Kuvunjika Kwa Mahusiano Haimaanishi Kuwa Mahusiano
Hayo Hayakuwa Sahihi, You Can’t Conclude That Way, Yote Mawili Yanawezekana.
Yaani Katika Mahusiano Yanayovunjika Yapo Ysiyosahihi Na Yapo Yaliyosahihi.
Kwamba Mahusiano Ni Sahihi Haimaanishi Hayawezi Kuvunjika Au Hayawezi Kupitia
Changamoto Ngumu Za Kuyavunja.
§
Kuna Siku Niliwaambia Hapa Kuwa Wapo Wakaka
Wanaogopa Kuwa Kwenye Mahusiano Na Wadada Wasomi Au Wenye Uwezo Kuliko Wao Au
Wanaoonekana Ni Warembo Sana. Hizi Zote Ni Ishara Za Mkaka Ambaye Hajajitambua
Wala Hajikubali Wala Hajui Anachotaka. Kujitambua Ni Jambo La Msingi Sana Kwa
Adam Wa Kiume Kwenye Mahusiano.
§
Kimsingi,
Zinaweza Kuwepo Sababu Kadhaa Zinazoweza Kufanya Mahusiano Sahihi Yavunjike Na
Kila Upande Ukabaki Kumlaumu Mwingine Au Kumsingizia Mwingine. Nikukumbushe
Kuwa Kosa La Edeni Kimsingi Lilikuwa La Adam Wa Kiume. Na Mpaka Leo, Mwanaume
Asipokaa Kwenye Nafasi Yake Mwanamke Atasimama Kwenye Hiyo Nafasi Bila Hata
Kuuliza. Wewe Angalia Tu Famiia Yenu Uone, Kama Baba Alizingua Mama Ako
Alifanya Nini.
§
Kutokujitambua Ni Zaidi Ya Kusema Mtu
Hajaokoka Maana Wale Wanosema Wameokoka Ndio Wanaongoza Kwa Kuwa Na Mahusiano
Yanayoliwa Na Madumadu Kila Siku,Hakuna Mwelekeo. Mkaka Kutokujitambua Ni Janga
La Kiroho Na Kiufahamu.
§
Kutokujitambua Kwa Adam Wa Kiume. Ni Heri Mdada
Akae Single Kuliko Kuwa Kwenye Mahusiano Na Mkaka Ambaye Hajajitambua. Mkaka
Asiyejitambua Ni Hatari Kuliko Bomu La Nyuklia Maana Yeye Anakuvuruga
Kidogokidogo Kuanzia Ndani Kuja Nje. Kutokujitambua Kumewafanya Wakaka Wengi
Wawe Kama Maroboti Kwenye Mahusiano. Kutokujitambua Kumewafanya Wakaka Wengi
Wawe Kama Mashabiki Na Wasindikizaji. Kutokujitambua Maana Yake Hawajui Wao Ni
Akina Nani Na Nafasi Yao Ni Ipi. Kwamba Hajui Nafasi Yake Inatosha Kumfanya
Kuwa Kitu Cha Ahajbu Sana
§
Mahusiano Sahihi Yakikutana Na Mkaka Ambaye Hajajitambua
Ni Wazi Kuwa Haya Muda Mrefu Yatavunjika Na Hasa Kama Mdada Akiwa Na Akili Zake
Timamu.
§
Sasa
Twende Tukaangalie Sababu Zinazosababisha Mahusiano Sahihi Yavunjika Kabla Ya
Safari Yenyewe Kufika Mwisho:
§
Adam Wa Kiume Aliyejitambua Hashindani Na Adam
Wa Kike Kwa Lolote Kamwe Kwani Anajua Kuwa Ushindani Ni Kwa Ajili Ya Watu Ambao
Wako Nje Ya Nafasi Zao. Ukiwa Kwenye Nafasi Yako Huna Muda Wa Kushindana Bali
Unakuwa Busy Kuwajibika Kwenye Eneo Lako.
§
Kujua Tu
Jinsi Yako Kama Mwanaume Sio Mwisho Wa Kujitambua, Ni Sehemu Ya Kujitambua.
Kuna Kujitambua Kunakoakisi Kama Umetambua Wajibu Wako Na Kuutekeleza Vile
Inavyopaswa. Kutokuwajibika Kwenye Nafasi Yako Wewe Kama Kiongozi Kunaharibu
Kabisa Ladha Ya Mahusiano Kwa Ujumla. Wadada Hufurahia Sana Wakiwa Na Mkaka
Aliyejitambua Na Anaejikubali Bila Kujali Uwezo Wala Elimu Yake.
§
Mkaka Aliyejitambua Anajua Kuwa Adam Wa Kike
Anahitaji Kujaliwa, Na Kwahiyo Anatumia Mbinu Zake Zote Alizonazo Kuhakikisha
Kuwa Hakuna Mwanaume Mwingine Anaeonyesha Kumjali Kama Yeye. Adam Wa Kiume
Anahakikisha Kuwa Mdada Anatambua Nafasi Yake Kwa Kila Jambo Afanyalo Kwake.
§
Adam Wa
Kiume Aliyejitambua Hawezi Kumziria Mdada, Hawezi Kumpiga Wala Kumfanyia Jambo
La Hiana Maana Anajua Nafasi Yake Ni Kukaa Kama Kiongozi Na Kuwajibika
Sawasawa.
§
Twende Sababu Ya Pili...
§
Ujinga Au Kutokujua Au Uhaba Wa Ufahamu Sahihi
Kuhusu Mahusiano Kwa Ujumla. Kama Sababu Ya Kwanza Ni Changamoto Basi Ya Pili
Ni Shida Kubwa. Wakaka Wengi Kwanza Hawapendi Kujifunza Au Kufundishwa Kwani
Kwa Wengine Hiyo Ni Ishara Ya Kuonekana Dhaifu Na Kwahiyo Wakaka Wengi
Wamejifunza Kupambana Na Hali Ya Upungufu Wa Ufaham Sahihi Ulio Ndani Yao.
§
Huo Atakuwa Mwanamke Wa Ajabu Ambaye Tabia Yake
Halisi Wala Sio Hiyo Ya Usaliti. Wengine Ni Mapepo Tu Mzee Yaani Nguvu Za Giza.
Ila Mwanamke Wa Kawaida Hawezi Kuwa Namna Hiyo.
§
Asante Sante
Kwa Ushauri Wako But Nadhani Kuna Mambo Mengi Hutokea Kwenye Mahusiano
Mengi Nilikuwa Napenda Kufaham Pamoja Na Mada Tajwa Hapo Juu Zilivo Jiekeza Ni
Kwann Muda Mwengine Mwanamke Unaweza Kumpa Kila Kitu Na Bado Akakusaliti? Maana
Hapa Neno Usaliti Lina Maana Nyingi But Nazungumzia Usaliti Wa Mdomoni Kwa Watu
Hadi Wa Ndani Kutoka Na Wanaume Wengine Nni Solution Yake Ya Hilo Jambo?
§
Wakaka Wengi Kuna Vitu Vingi Wanavifahamu Ila
Sio Sahihi. Mwisho Wa Siku Wanaishi Katika Kiwango Kile Kile Cha Ufahamu Wao Wa
Mambo Mengi Yasiyosahihi. Sasa Wewe Mkaka Utakuwa Na Bahati Mbaya Sana Wewe
Ukiwa Una Madudu Kichwani Halafu Unakutana Na Mdada Aliyepikwa Akaiva. Atakuwa
Anakufundisha Na Utamuona Much Know Na Kumbe Ni Kwasababu Ya Kiwango Cha
Ufahamu Wako Mwenyewe. Fundishika Tu Rafiki Yangu.
§
Kuhusu
Ufahamu Yaani Mambo Unayoyajua Zingatia Kwamba Kila Mtu Kuna Vitu Anajua, Kuna
Vitu Hajui. Pili Ubora Wa Unayoyajua Na Usiyoyajua. Halafu Weka Akilini
Kwamba...Ni Heri Mtu Akunyime Taarifa Kuliko Akupe Taarifa Zilizopotoshwa Au Za
Uongo.
§
Wewe Fikiria Mambo Uliyojifunza Toka Umeingia
Boyzmen Talk Mpaka Leo, Ungejifunza Wapi? Ila Pamoja Na Hayo Uliamini Kuwa
Mauhusiano Yako Yangekuwa Mazuri. Ungeishi Kwenye Mahusiano Yako Kwa Kiwango
Cha Ufahamu Wako. Na Ndio Maana Hata Kuna Wengine Humu Wamejitambulisha Kuwa
Wako Single Ingawa Wana Wadada Ila Ni Vile Hana Uhakika Haha Haha Hahah
Hahahaha
§
Kuwa Na Washauri Wabaya Au Kutokuwa Kabisa Na
Washauri. Hivi Ni Nani Hapa Duniani Anaweza Kufanikiwa Pasipo Ushauri Wa Watu
Wengine? Kumbe Swala Sio Ushauri Bali Ubora Wa Ushauri. Nani Ni Mshauri Wako
Ukiwa Na Maswali Magumu Ya Mahusiano? Nani Anaweza Kukukalisha Chini Na Kukupa
Ukweli Wako Bila Kupepesa Macho? Nani Unajua Kabisa Anaweza Kukutoa Tongotongo
Na Ukawa Na Amani Kabisa Kuwa Ni Mtu Sahihi? Ukikutana Na Changamoto Kwenye
Mahusiano Unaweza Kumfuata Huyo Mtu Hata Kama Yuko Mbali Na Wewe Akakusaidia?
Wakaka Wengi Hupambana Wenyewe Maana Hutafsiri Kusaidiwa Kama Unyonge Lakini
Pia Ile Hali Ya Kiburi Ya Kujionyesha Kuwa Hata Wewe Unaweza. Ni Kweli Unaweza
Lakini Ipo Thamani Ya Yusufu Kutangulizwa Misri. Inawezekana Kabisa Mahusiano
Yako Yasingevunjika Kama Ungeshauriwa Vyema.
§
Kutokuwa
Halisi. Dishonesty. Kutokuwa Mkweli. Kuficha Ficha Mambo. Kutokuweka Wazi Mambo
Ya Msingi. Kuishi Maisha Ya Rangi Saba Au Nne. Kuwa Mchanganyiko Wa Mtu Ambaye
Haeleweki. Yaani Mdada Anashindwa Kujua Kama Unampenda Au Unamtamani Au Ni
Nini. Mdada Anashindwa Kukuelewa Maana Ikifika Kwenye Maswali Fulani Hivi
Unakuwa Kama Mbogo...Sasa Ukiwa Mbogo Na Hujamuoa Je Ukimuoa Si Ndo Utahamia
Porini? Ni Vema Sana Kuwa Mkweli Na Muwazi. Kumbuka Ukweli Na Uwazi Sio Issue
Ya Kutokuweka Password Kwenye Simu, Ni Issue Ya Moyo.
§
Ulimbukeni. Ulimbukeni Ni Ile Hali Ya Ushamba
Iliyochanganyikana Na Ujuaji Wa Mambo Usiyoyajua. Kuna Namna Ya Kupapatikia
Mambo Ambayo Adam Wa Kiume Anayo.Upande Huu Wa Ulimbukeni Ninaousemea Unahusu
Hasa Ushamba Wa Vijana Wengi Wa Kujifanya Wajuaji Halafu Wanashindwa Kutoa
Fursa Ya Kujifunza Pindi Wanapokutana Na Mdada Mwenye Ufahamu Mkubwa Kuliko
Wao. Mathalani Wale Ambao Wameokoka, Kuokoka Hakumfanyi Mtu Ajue Kila Kitu.
§
Akili Za
Kuegesha Za Mfumo Dume. Mahusiano Mengine Yamevunjika Kwa Sababu Ya Ubabe Na
Undava Wa Makabila Au Ukiroho Usio Wa Roho Wa Mungu. Wakaka Wengi Hutaka
Asemalo Yeye Liwe Alfa Na Omega. Maamuzi Yake Yasipingwe Wala Kuhojiwa. Awe
Anamburuza Tu Mdada Anavyojisikia. Ni Kweli Unaweza Ukafanya Hivo Lakini Sio
Kwa Wadada Wa Kizazi Cha Leo, Wenye Ufahamu Na Ambao Wenginwe Wamedungwa
Sindano Za Uharibifu Na Makungwi Wao.
§
Kutokuwa Tayari Kulipa Gharama Ya Uwekezaji Wa
Ndani. Kwakuwa Utajikuta Kwenye Mahusiano Na Mtu Ambaye Hajakamilika
Inamaanisha Kuwa Ipo Fursa Ya Kukamilishana Kwa Pamoja Kadri Mnavyoendelea
Mbele. Hii Ni Kinyume Kabisa Na Ready Made Approach Ambayo Unataka Ukutane Na
Mtu Amekamilika Kabisa. Wakaka Wengi Hukimbia Kulipa Gharama Ya Kuwekeza Kwa
Wapenzi Wao Ila Huwa Kipaumbele Kuwapost Mashemeji Zao Wakidhani Wale Wengine
Wametokea Mwezini Na Kumbe Mambo Ya Uwekezaji Ni Gharama. Usichokilipia Gharama
Hutakiheshimu Kihivyo.
§
Kutokuwa
Tayari Kukubali Kukosea Na Kuomba Msamaha Kwa Wakati Husika. Hapa Ni Muhimu
Kufahamu Kuwa Hisia Za Mwanamke Yoyote Wa Kawaida Mwenye Akili Timumu Ziko
Karibu Sana. Unapokosea Na Ukajua Au Ukaambiwa Umekosea Wewe Kama Adam Wa Kiume
Ni Vema, Hata Kwa Kujilazimisha Uombe Msamaha Na Kukubali Kosa...Hii Inaleta
Uponyaji Wa Wakati Husika. Mambo Ya Kujifanya Wewe Ni Mgumu, Sijui Diminder
Yatakufanya Uishie Kutamani Kuwa Na Mahusiano Ya Kwenye Vitabu Au Movie Tu.
Fahamu Pia Kuwa Kumuomba Msamaha Mtu Aliye Chini Yako Kimamlaka Inakupa Wewe
Nguvu Kubwa Zaidi Kwake Na Heshima Ya Kutosha.
§
Kutokuelewa Maana Ya Udhaifu Wa Mdada. Ni Vema
Wewe Kama Mkaka Ukajua Kuwa Mungu Anasema Mwanamke Ni Kiumbe Dhaifu Sio Ili
Ukionee Bali Uwe Na Akili Za Kujua Namna Ya Kuishi Nae. Ni Lazima Ujue Kuwa
Lazima Kuna Maarifa Unahitaji Kuwa Nayo Ya Kukusaidia Kuweza Kuishi Nae Na
Kumwelewa. Mojawapo Kubwa Ni Kumsikiliza. Hata Kama Anaongea Kuliko Wewe, Ni
Vema Ukajifunza Kusikiliza. Usisahau Kuwa Kusikiliza Ni Moja Sifa Nzuri Za
Kiongozi Mzuri.
§
Mabadiliko Mengi Ya Wakaka Huwa Yanachukua
Muda Mrefu Sana Na Hasa Linapokuwa Ni Jambo La Tabia Fulani Hivi Ambayo Mdada
Anakwambia Lakini Wewe Unachukulia Poa Na Kuona Utabadilika Tu Mungu Akipenda.
Hii Kwanza Huwa Inatengeneza Maumivu Na Makovu Ya Kutosha Kwa Mdada Na
Akishakomaa Huzaa Kitu Kigumu Sana Ndani Yake. Changamoto Huwa Ni Katika
Kujiuliza Huwa Ni Kwanini Hutaki Kubadilika Kwenye Jambo Ambalo Litawasaidia
Wote Wawili? Kadri Unavyokaa Kwenye Hali Ya Kutokubadilika Unaongeza Walakini
Kwa Mdada Mpaka Anaweza Kufika Mahali Akakuona Kuwa Wewe Sio Mtu Sahihi Na
Kumbe Inakuwa Si Swala La Usahihi Bali Uwezo Wako Wewe Wa Kufanya Maamuzi Ya
Mabadiliko.
§ Kuwa Na Akili Za Mpito Uliokosea Njia. Ni
Kweli Kuwa Wadada Wazuri Wako Wengi. Ni Kweli Kuwa Wadada Wazuri Kuliko Huyo
Ulonae Wako Wengi Sanaaaaa Ila Sahihi Ni Mmoja Mtu Na Kama Ni Huyo Uliye Nae
Ndo Sahihi Basi Akili Zile Za Kusema....Wadada Wako Wengi Ni Akili Za Mpito
Zilizokosea Njia. Wazuri Wako Wengi Ila Sahihi Ni Mmoja Tu Kwenye Majira Hayo.
Hiyo Kauli Pia Huwa Ni Kauli Inayoonyesha Kiburi Cha Uzima. Kama Unabisha Wewe
Muache Huyo Ambaye Ndo Sahihi Uone Kama Utafika Mbali. Ni Kweli Unaweza Ukaona
Mambo Yanaenda Mwanzoni Lakini Ndani Ya Moyo Wako Hutakuja Kujisamehe Kwa Kosa
Hilo. Dont Leave What Is Right For Only What Is Good For Not Every Good Thing
Is Right All The Time.
§
Nina Hakika Kuwa Wale Waliokuwa Wanakaribia
Kuvunja Mahusiano Yao Watawaza Mara Mbili Baada Ya Kusoma Hizi Nondo Na Wengine
Watajilaumu Sana Mioyoni Mwao Kwanini Walivunja.
·
Kuwasikiliza Watu Wanyonge Na Dhaifu Kifikra.
Hawa Wako Kwenye Makundi Kadhaa Ila Maneno Yao Yanadhihirisha Kuwa Wao Ni
Dhaifu Na Wanyonge Kifikra. Wapo Wanoitwa Washauri Wa Kiroho Sijui Dady Sijui
Papaa Sijui Nani Bin Apostolic Prophet. Hawa Unahitaji Mungu Kuwaelewa Na Kujua
Matakwa Na Nia Zao. Sio Wote Ni Wazushi Ila Wapo Wazushi Wengi Ambao Anaweza
Kukupangia Hata Mtu Wa Kuoa. Anaweza Kukuwekea Mazingira Ya Kiroho Ambayo
Yatakusaidia Wewe Kukosea Na Kumucha Mtu Sahihi Na Kujikuta Mikononi Mwa
Nyangumi Ambye Kwa Muda Huo Anaonekana Kama Sato Mtamu Tokea Ziwa Victoria.
Yapo Pia Mapepo Ambayo Hufanya Kazi Za Kuvuruga Mipango Ya Wana Wa Mungu Kwa
Njia Mbali Mbali Ikiwemo Marafiki Na Mitandao Ya Kijamii Mpaka Unafika Mahali
Unaanz Akumuona Ulienae Anachuja. Wengi Hutawaliwa Na Ubinafsi Wa Nia Zao Ili
Waendelee Kushika Usukani Wa Akili Zako Maana Sasa Wewe Uko Kama Mwanasesere.
Unapomuacha Mdada Sahihi Kwakuwa Tu Nani Wako Wa Kiroho Sijui Amekwambia
Amemuota Kwenye Ndoto Unakuwa Umekubali Ushauri Dhaifu Sana Na Ujue Maisha Ya
Ndoa Utaishi Wewe Na Nyangumi Na Huyo Nani Wako Wa Kiroho Sijui Atakuwa Anakula
Tu Bata Kwa Jina La Sadaka Zako Ikibidi. Nalisema Hili Kwa Umakini Mkubwa.
Nasema Uwe Makini Sana Kwenye Makundi Ya Watu Wenye Nguvu Ya Ushawishi Maishani
Mwako.
Nadhani Haya Mambo Yatakuwa Yamejibu Maswali Yenu Mengi Kwenye Hili
Eneo
UMUHIMU WA ADAM WA
KIUME KUWA NA CHANZO CHA KIPATO KATIKA KUIPA NGUVU NAFASI YAKE KWENYE MAHUSIANO....
Mwanzo 2:15
“Bwana Mungu Akamtwaa
Huyo Mtu, Akamweka Katika Bustani Ya Edeni, Ailime Na Kuitunza.”
Waefeso 5:28
“Maana Hakuna Mtu
Anayeuchukia Mwili Wake Po Pote; Bali Huulisha Na Kuutunza, Kama Kristo Naye
Anavyolitendea Kanisa.”
Mwanzo 2:15.. ”Ailime
Na Kuitunza.”
Waefeso 5:29: “Huulisha Na Kuutunza.”
Tuanze Na Mwanzo....
·
Ni Muhimu Sana Kwako Wewe Kaka Unaetaka Kuoa Au
Unajipanga Kuoa Kuwa Na Chanzo Cha Kukuingizia Kipato. Hata Kama Unafanya
Huduma,Kumbuka Huduma Ya Kuomba Omba Ili Kuishi Ni Mateso Sana Na Wala Sio
Sahihi.
·
Mungu
Alipomuumba Adam Wa Kiume Jukumu La Kwanza Alilompa Ni Kazi Ya Kutunza Na
Kuilima Bustani.
·
Tafsiri Ya Kingereza Ina Mamneo Kadhaa Ya Mwanzo
2:15.....Hebu Leteni Version Za Kingereza Hapa
Genesis:2:15 Kjv
“And The Lord God Took
The Man, And Put Him Into The Garden Of Eden To Dress It And To Keep It.”
Amplified Bible Genesis 2:15
“So The Lord God Took
The Man [He Had Made] And Settled Him In The Garden Of Eden To Cultivate And
Keep It.”
Genesis 2:15 Nkjv
“ Then The Lord
God Took The Man And Put Him In The Garden Of Eden To Tend And Keep It.”
Ephesians
5:29 New International Version
“ After All, No
One Ever Hated Their Own Body, But They Feed And Care For Their Body, Just As
Christ Does The Church”
Genesis 2:15 Nlt
“The Lord God Placed The Man
In The Garden Of Eden To Tend And Watch Over It.”
- Cultivate And Keep
- Tend And Keep
- So You Can See These Words All Together...To Dress, To Cultivate, To Tender And Keep
I Want To Expound This As
Follows:
·
Put Him Into The Garden - To Dress It, And To
Keep It - Horticulture, Or Gardening, Is The First Kind Of Employment On
Record, And That In Which Man Was Engaged While In A State Of Perfection And
Innocence. Though The Garden May Be Supposed To Produce All Things
Spontaneously, As The Whole Vegetable Surface Of The Earth Certainly Did At The
Creation, Yet Dressing And Tilling Were Afterwards Necessary To Maintain The
Different Kinds Of Plants And Vegetables In Their Perfection, And To Repress
Luxuriance. Even In A State Of Innocence We Cannot Conceive It Possible That
Man Could Have Been Happy If Inactive. God Gave Him Work To Do, And His
Employment Contributed To His Happiness; For The Structure Of His Body, As Well
As Of His Mind, Plainly Proves That He Was Never Intended For A Merely
Contemplative Life.
·
Kumbe Mungu
Hakumuacha Adam Wa Kiume Akae Bila Kazi. Alimpa Kazi Ya Kufanya. Ailime Bustani
Na Kuitunza.
·
Kumbuka Hapa Ni Kabla Hata Adam Wa Kike Hajaja.
·
Ni Vema Kupata Shughuli Ya Kufanya Hata Kabla Ya
Kuingia Kwenye Mahusiano Ya Kuelekea Ndoa. Huu Ndio Mfumo Wa Kibiblia.
·
Work
Should Precedes Her.
·
Mtazamo Wa Mwanzo
2:15 Unasisitiza Sana Mwanaume Kufanya Mambo Ya Msingi Kwanza. Shughulika
Na Vipaumbele Vya Msingi Kwanza. Kipaumbele Cha Kwanza Ni Kufanya Kazi, Yaani
Kuwa Na Eneo Ambalo Unalima Na Kulitunza. Ukisoma Hii Vizuri Utaelewa Kuwa
Mungu Aliweka Mazingira Ya Kilimo Kuwa Kazi Ya Kwanza Ya Mwanaume.
·
Hata
Baada Ya Anguko Tunaona Wazo La Kazi Lipo Pale Pale Ila Sasa Limeboreshwa
Zaidi...Adam Ni Kula Kwa Jasho Toka Ardhini.
·
Hivo Ni Muhimu Sana Kuwa Na Kazi Inayokuingizia
Kipato. Huu Ni Mtazamo Wa Jumla Wa Kazi
Twende Upande Wa
Pili...
- Ni Wajibu Wa Mwanaume Kumlisha Na Kumtunza Mwanamke. Usikwepe Hili Jukumu. Ni Hatari Sana Kwa Mkaka Kulelewa Na Mdada.
- Wazo La Mwanaume Kumlisha Na Kumtunza Mwanamke Ni La Mungu Na Sio Mwanadamu. Na Hapo Imetolewa Kwenye Kiwango Cha Maisha Ya Ndoa Kabisa Kwani Wanakuwa Mwili Mmoja.
- Sasa Unadhani Utamlisha Na Kumtunza Kwa Maneno Tu Ya Kinabii?
- Kumtunza Sio Jambo Jepesi Maana Lina Gharama Zake. Kumtunza Ni Zaidi Ya Kumvalisha Nguo, Ina Maana Pia Ya Kumkalisha Na Kumuweka Awe Kwenye Kiwango Chake. Itunze Rangi Yake. Tunza Ngozi Yake. Utunze Mwili Wake.
- Sasa Kama Huna Kazi Ya Kukuingizia Kipato Utamlisha Na Kumtunza Kwa Kutumia Ukarimu Wa Marafiki Au Sadaka Za Huduma Kama Ni Huduma Lakini?
- Usije Ukaingia Kwenye Mkumbo Wa Vijana Wa Kileo Ambao Wanaamini Kuwa Unaweza Kuoa Hata Kama Huna Kazi Maana Hata Mahari Yenyewe Unachangiwa. Huu Ni Upuuzi.
Halafu Ngoja
Niwaambie Kitu....
·
Sio Kwamba Wadada Wanataka Wakaka Wenye Hela.
Wala Usije Ukaitumia Hii Kama Pointi Ya Kukudhoofisha. Ukweli Ni Huu
Hapa....Wadada Wanataka Mkaka Mwenye Akili Za Kuweza Kuleta Maboga Mezani Au
Makande...Unaweza Ukawa Huna Kazi Moja Kwa Moja Lakini Akili Zako Zinamshawishi
Mdada Kuwa Wewe Ni Mpambanaji Na Sio Mkaka Golikipa.
·
Mdada Mwenye Akili Timamu Anataka Mkaka Mwenye
Akili Na Anaejua Kuzitumia Akili Zake Kuleta Matumaini Ya Tumbo Nyumbani. Sasa
Kama Wewe Tu Sasahivi Kwenye Mahusiano Huna Mwelekeo Wowote Wa Kuonyesha Kuwa
Una Mpango Wa Kuzitumia Akili Zako Ili Kuonyesha Kuwa Unajiandaa Kumlisha Na
Kumtunza,Utamlaumu Akikupa Kibuti Cha Shahada Mbili?
·
Ni Aibu Na Ajabu Sana Leo Kwamba, Wakaka
Waliokaa Kihuduma Huduma Ukiwaambia Wafanye Kazi Anaweza Kusema Huduma Ndio
Kazi Yake Haha Hahaha Hahaha Sasa Ukiangalia Kiuhalisia Huduma Ni Kutoa Na Sio
Kupokea...How Can Ministry Be Work My
Friends? Hebu Fanya Kazi,Acha Ujinga Wako. Fanya Kazi. Kumbuka Kazi Ni Akili Na
Kila Mtu Ana Akili. Funguka.
·
Narudia Tena...Wadada Wenye Hofu Ya Mungu Sio
Kwamba Wanapenda Pesa Kihivyo Kama Wakaka Wengi Wanavyolalamika. Wadada Wa
Mungu Wanajua Nafasi Ya Mwanaume Ni Kiongozi Na Kiongozi Lazima Awe Mzalishaji.
Lazima Aonyeshe Kuchakarika Na Kupambana Ili Alete Zawadi Ya Kanga. Ukiona
Mdada Anakuhamasisha Kuhusu Kuzalisha Au Kupata Kazi Ujue Umepata Mtu Sahihi
Sana Ila Akili Zako Zikikwambia Kuwa Lengo Lake Ni Kukuchuna Ujue Unajichuna
Mwenyewe.
·
Sasahivi Kwenye Utalii Kuna Aina Ingine Ya
Utalii Inaendelea Kushika Kasi Inaitwa Sexual Tour...Wazungu Wamama Wazee Wenye
Hela Zao Wanakuja Tanzania Na Kutafuta Vijana Magolikipa Na Kuwanunua Ili
Wawahudumie. Akili Za Kuegesha Wewe Kaka Unataka Mdada Ndo Akulishe? Akuvishe?
Usije Ukajikuta Unavishwa Na Kulishwa Na Mwanaume Wa Huyo Mpenzi Wako Huku Wewe
Unamshukuru Mungu Kwa Muujiza. Acha Ujinga Nakwambia. Amka.
·
Mdada Wa Mungu Ni Mvumilivu Sana. Ili Mradi Wewe
Ni Mpambanaji Anaweza Kuvumilia Hali Zote. Wadada Wavumilivu Bado Wapo Na Hasa
Kama Amekupenda. Anaweza Akawa Tayari Kula Ugali Na Chumvi Akiona Bidii Yako
Wewe Mkaka Ya Kutafuta. Anakuona Unatoka Home Na Unarudi Jioni,Yaani Hata Kama
Umerudi Na Vumbi Tu Kwakwe Ina Maana Kubwa Sana Kuliko Unakaa Tu Au Unakuwa
Mbishi Tu Wa Kutafuta Kazi Wakati Una Akili. Tumia Akili Zako. Wala Usiue Wala
Kula Rushwa Wala Usitende Dhambi Ili Useme Ni Kazi. Kazi Lazima Imtukuze Mungu
Hata Kama Ni Kushona Viatu.
·
Unasubiri Na Wewe Mdada Akushonee Shati La
Kitenge? Ameshakushonea Kama Saba Hivi, Wewe Ndugu Yangu Hapa Hujatoa Hata
Mia...Hujisikii Kuwa Una Roho Ya Kigaidi? Upendo Ni Kutoa. Anaekupenda Anatoa
Na Wewe Toa. Lakini Utatoaje Na Huna Cha Kutoa? Kama Huna Cha Kutoa Basi
Kakitafute. Go To Work. Find Something. Use Your Mind. Connect Yourself.
Kumbuka Kuwa Kazi Ni Zaidi Ya Kuajiriwa. Open Your Mind Wewe Mkaka.
Utasema Hukuambiwa? Hukushauriwa? Hukuhimizwa?
·
Basi Mungu Akubarikie Sana
·
Nakuombea
Neema Ya Kukaa Vizuri Na Akili Yako Kutulia.
·
Mungu Akufungue Macho Ya Moyo Wako.
·
Kama Huwezi Kupata Kazi Kwa Ulichosomea Basi
Tafuta Au Tengeneza Kazi Kwa Unachoweza Kufanya. Usilazimishe Kupata Kazi Ya
Ualimu Wakati Uliamua Kusoma Ualimu Ili Upate Mkopo Full. Kuna Akili Unahitaji
Kuzitumia Kupambana Na Hali Halisi Kuliko Kulalamika Kuwa Kazi Hakuna.
Inawezekana Kazi Ambazo Hazipo Ni Zile Za Mambo Uliyosomea Ambayo Ni Ya
Uongo,Sasa Wewe Fanya Kazi Unazoweza Maana Ziko Ndani Yako.
·
Angalia Watu Wenye Huduma Kubwa Kuliko Wewe, Na
Wakongwe Kuiko Wewe Na Ujifunze Kwo. Angalia Kama Wanaishi Kwa Kuangalia Huduma
Na Bahasha Zake. Uwe Makini Sana Kijana Wangu Usije Ukajikuta Unaanza Biashara
Ya Mawe Kwa Kuyaita Anointeda Stones Au Mawe Ya Upako. Mungu Ni Shahidi Juu Ya
Jambo Hili
·
Employment Is
Work But Work Is Not Employment All The Time.
·
Ajira Ni Kazi Lakini Kazi Sio Ajira Wakati Wote.
Quotes By Raphael Jl:
Mtu Akikupa Fursa Ya Kumwambia Ukweli Wa Mwenendo Wake, Au Hata Mungu
Akikuonyesha Udhaifu Wake; Wewe Usinyanyue Pembe Na Mabega Na Kujisifu Kuwa
Unamfahamu Huyo Mtu. Kwanza Fahamu Umepata Neema Ambayo Usiku Wa Leo Inaweza
Kuondoka Ukabaki Na Maumivu Ya Kiburi Cha Uzima. Ni Kweli Umeota Katika Ndoto
Na Kuona Shida Yake Lakini Haikufanyi Wewe Kuwa Kipeo Na Kipimo Cha Maisha Ya
Huyo Mtu. Unyenyekevu Sio Upole Au Ukimya. Hatuwaheshimu Watu Kwa Kuwa
Tumewazidi Ukiroho Wa Rohoni Au Kwa Kuwa Mtu Anaona Mambo Ya Rohoni Kuliko
Mwingine; Maana Hata Shetani Yuko Huko Huko Rohoni. Usijihesabie Haki Kwa Anayestahili
Heshima.
By Raphael: Joachim Lyela
Classified Mindset
·
Pata Muda Wa Kuombea Mahusiano Yako.
·
Kama Huna Basi Muombe Mungu Akuandae Pia
Boyzmen Talk Kesho: Makuzi
Yanaathiri Mahusiano Yako Mpaka Ndoa Kwa Kiwango Cha Makuzi; The Impact Of
Upbringing On Your Relationships To Marriage.
Boyzmen Talk Leo: Makuzi Yanaathiri Mahusiano Yako Mpaka Ndoa Kwa
Kiwango Cha Makuzi; The Impact Of Upbringing On Your Relationships To Marriage.
LEO TUNAONGELEA
NAFASI YA MAKUZI NA NAMNA MAKUZI YANAATHIRI MAHUSIANO KWA UJUMLA.
·
Makuzi Ni Mazingira Ya Jumla Ambayo Kila Mmoja
Wetu Amekulia
·
Makuzi Ni Pamoja Na Wazazi Waliokuzaa Na Kukulea
Au Hata Kama Ulilelewa Na Watu Baki.
·
Makuzi Ni Pamoja Na Mkoa Uliozaliwa Au Kukulia
Na Jamii Yake Kwa Ujumla
·
Makuzi Ni
Pamoja Ufahamu Uliokua Nao Au Ufahamu Uliokukuza
·
Kuhusu Makuzi Huwa Napend Kutumia Neno Wiring..
·
We Are Wired Differently
·
Wewe Mkaka Lazima Ujue Kuwa Wewe Sio Na Huwezi
Kuwa Kama Mdada
·
Mitazamo
Yenu Ni Tofauti Sana
·
Hisia
Zenu Ni Tofauti Sana
·
Namna
Mnavyoangalia Maisha Ni Tofuati Sana
·
Sasa Unaponzisha Mahusiano Ni Lazima Ujue Kuwa
Nyie Ni Watu Wawili Tofauti Sana
·
Lakini Kila Mmoja Ameathiriwa Sana Na Makuzi
·
Eneo La
Kwanza Ambalo Limeathiri Tabia Na Mwenendo Ni Wazazi
·
Wengi Wetu Tumeathiriwa Sana Na Ubora Na Kiwango
Cha Mahusiano Ya Wazazi Wetu.
·
Kama Wewe Umekulia Kwenye Familia Yenye Upendo
Wa Kweli Na Inayojali Mawasiliano Basi Utatamani Upate Mtu Wa Namna Hiyo
·
Na Kama Ukipata Mtu Wa Tofauti Basi Kuna Namna
Utaona Ugumu Sana Wa Kutengeneza Mahusiano Yenye Ufanisi
·
Kama Umekulia Uswahilini, Utahitaji Msaada Sana
Kuishi Na Mdada Aliyezoea Maisha Ya Kizungu
·
Kama Umezoea Unalala Halafu Unaamka Kwa Yesu
Amefufuka Staili Hakika Utaona Mzingo Sana Ukiambiwa Utandike Kitanda.
·
Makosa Mengi Kwenye Mahusiano Pia Hutokea Eneo
Hili La Makuzi
·
Kabila Lako Linaweza Kuwa Kizuizi Kikubwa Sana
Kwenye Mahusiano Yako Maana Watu Wameshakubali Kuwa Kuna Makabila Ambayo Hayako
Friendly Kwa Kuoa Ingawa Sio Kweli Kimsingi.
·
Unatoka
Na Mpenzi Wako Unaenda Kumtambulisha...Unaulizwa Kabila...Unasema Ni
Mfipa...Utaambiwa Huko Hapana Kwani Ni Wachawi...Weka Kabila Lako Utaona Kuna
Tabia Gani Ambayo Imefungwa Na Desturi.
·
Unaweza Ukawa Una Kosana Na Mpenzi Wako Kila
Siku Na Kumbe Sababu Ni Kutokujua Kuwa Makuzi Yenu Hayafanani
·
Kama Umekua Ukiona Wazazi Wako Ni Kupigana Au
Kutukanana Kila Siku Au Mara Nyingi Basi Ni Lazima Utakua Na Athari Ya Jambo
Hilo Hata Wewe Mpaka Uamue Kujifunza Na Kufanya Kwa Tofauti
·
Kama
Umekua Na Hujapata Mapenzi Ya Wazazi Inawezekana Kabisa Ukawanyima Watu Wako Wa
Karibu Huo Upendo Maana Hauna..Ni Mpaka Ujifunze.
·
Makuzi Na Malezi Yana Mchango Mkubwa Sana Katika
Mahusiano Ya Kila Siku
Quotes By Raphael Jl:
Kuisahau Thamani Yako Haimaanishi Haipo. Kutokujua Thamani Yako
Haimaanishi Huna Thamani. Mtu Akisema Wewe Huna Thamani Bado Haiondoi Thamani
Yako. Thamani Yako Haitokani Na Mawazo Yako Au Mawazo Ya Watu Bali Inatokana Na
Asili Yako. Siku Nyingine Mtu Akikwambia Huna Thamani, Wewe Mwambia Hayo Ni
Mawazo Yako. Haiwezekani Uumbe Na Mungu Halafu Usiwe Na Thamani Labda Kama Bado
Unaamini Wewe Ulikuwa Sokwe, Hata Sokwe Wana Thamani Pia. Value Is A Function
Of Source.
Ykm-Satisfied In Jesus!
·
Naomba Nimalizie Jambo La Mwisho Ambalo Nataka
Tu Niliseme Kwa Jinsi Ingine....
Quotes By Raphael Jl:
Wewe Sio Wa Kwanza Na Wala Hutakuwa Wa Mwisho. Yanayokutokea Wewe Leo
Yalishawatokea Wengine Hata Kabla Hujazaliwa. Wewe Sio Wa Kwanza. Usikubali
Hali Ya Sasa Ikufanye Upoteze Tumaini La Kesho Wakati Bado Uko Hai. Ili Mradi
Kinachoutokea Leo Hakijakuua Basi Unayo Nafasi Ya Kusimama Tena. Even This Shall
Pass Too, Hata Hili Litapita Pia.
Ykm-Satisfied In Jesus!
·
Usioe Kama Bado Wewe Ni Mvulana Na Sio Mwanaume
·
Hapo Ni Usioe Wala Usiingie Kwenye Mahusiano
Kama Wewe Bado Ni Mvulana
·
Wavulana
Wengi Waliooa Na Kuingia Kwenye Mahusiano Wameleta Shida Sana Hayo Maeneo
·
Mvulana Ni Adam Wa Kiume Ambaye Bado Hajakomaa
Kubeba Majukumu Ya Familia Na Wengi Huwa Wanadeka Sana
·
Wavulana
Wengi Wakiwa Kwenye Mahusiano Hutaka Sana Kulelewa Na Kufanyiwa Vitu Na Wadada
Kwa Kisingizio Kuwa Ni Wapenzi
·
Wavulana
Wengi Hukaa Kwenye Mahusiano Wakiwa Tegemezi Sana Kwa Wapenzi Wao
·
Wavulana
Wao Huingia Kwenye Mahusiano Kwa Ajili Ya Tamaa Za Ngono Na Sio Wajibu Wa
Kusudi La Mahusiano Yenyewe
·
Wavulana
Wakiambiwa Wamekosea Mahali Huwa Wanachukia Na Kuona Kama Wananyanyaswa Na
Wengi Huishia Kuzira
·
Wavulana Wakiambiwa Na Adam Wa Kike Au Akaulizwa
Swali Kuhusu Maisha Yake Ya Baadae Na Mipango Yake Kama Mume Mtarajiwa Hujibu
Kiroho Sana Kwamba Bwana Atafanya...
·
Wavulana Huwa Hawako Tayari Kuzungumza Hard
Talks Ambazo Zinaonyesha Wajibu Wao Na Hutaka Kuzungumzia Vitu Vyepesi Tu
Kwenye Maisha
·
When A Boy Marries, Divorce Is Predictable.
·
Sio Kila Mwanaume Ni Mume Au Anafaa Kuwa Mume.
·
Sio Kila Mvulana Ni Mwanaume.
·
Ni Lazima
Ukubali Kutengenezwa
·
Ni Lazima Ukubali Kulipa Gharama Ya Kuwa
Mwanaume Ili Isikusumbue Sana Kuwa Mume.
Kwani Mwanzo 2:24 Inasmeaje Lakini
“Kwa Hiyo Mwanamume
Atamwacha Baba Yake Na Mama Yake Naye Ataambatana Na Mkewe, Nao Watakuwa Mwili
Mmoja.”
·
Usikubali Kulazimisha Kuoa Na Huku Una Kila
Dalili Ya Uvulana,Utoto Na Kudekadeka Tu
Kwahiyo, Maana Yake Kwa Kudusi Hilo Au Kwa Sababu Hiyo...Ni
Lazima Mwanaume Ajue Na Awe Na Kusudi...Tena Inasema Mwanaume, Haisemi
Mvulana...Lazima Uwe Mwanaume Ili Uoe.
·
Ujue Maisha Ya Mahusiano Ni Maisha Ya Kuwajibika
Kama Mwanaume
·
You Have To Be Independent From Your
Parents...Sio Unaoa Lakini Kutwa Kucha Unapiga Tu Mizinga Wazazi Wako Au
Unamuhamishia Mke Kwa Wakwe Ili Kupunguza Makali Ya Maisha. Huu Ni Ujinga.
·
Mvulana Akikosana Na Mkewe Anakimbilia Kusema
Kwa Wazazi Wake, Huu Ni Upuuzi.
·
Ni Lazima Ukubali Kuwa Mwanaume...Wewe
Umehsmuacha Baba Na Mama Yako Umeambatana Na Mkeo Sasa Lazima Ujue Kuyabeba
Mambo Na Kuyapa Ufumbuzi Wa Pamoja Na Sio Kukimbilia Kwa Watu Nje.
·
Wavulana Wengi Ni Wabishi Sana Kwani Huwa
Wanakuwa Bado Na Mambo Mengi Sana Ndani Yao Na Bado Wanakuwa Hawajaweka
Viapumbele Vizuri
·
Wavulana Wengi Wanapenda Kulelewa Jamani
Khaaaaaaaaaa
·
Wavulana Wengi Wanapenda Kupetiwapetiwa Mpaka
Wanaboa
·
Wavulana Wengi Huwaacha Tu Baba Zao Halafu
Huenda Na Mama Zao Kwenye Makao Mapya Na Akina Adam Wa Kike Akikutana Na
Mvulana Kama Huyu Atakuwa Na Kazi Sana Maana Kila Wanachofanya Lazima Kwanza
Mama Akijue Na Kukikubali. Huu Ni Ujinga Mkubwa Sana. Kama Hauko Tayari
Kumuacha Baba Na Mama Basi Endelea Kuishi Kivulana Nyumbani Kwenu.
·
Ukiona Kila Unachofanya Au Kukubaliana Na Mpenzi
Wako Ni Lazima Umuulize Mama Yako Ujue Hakika Wewe Ni Mvulana Bado Na Hutakiwi
Kuoa Maana Utakwa Mwiba Kwa Adam Wa Kike.
·
Kukubai
Kuambiwa Ukweli Ni Moja Ya Maeneo Ya Kuonyesha Kuwa Wewe Unakua...Yaani Unapiga
Hatua Maana Wavulana Wengi Huamini Wanchojua Wao Ndio Pekee Cha Kweli.
·
Makosa Ya Uvulanani Yanakera Sana
·
Utakuwa Tayari Kukosolewa Na Adam Wa Kike?
·
Utakuwa Tayari Kuambiwa Madhaifu Yako Usoni?
·
Utakuwa Tayari Kusema Nisamehe?
·
Utakuwa Tayari Kukubali Kwamba Umekosea Hata
Kama Umeokoka Mpaka Umefika Kitabu Cha Warumi?
·
Hakuna Adam Wa Kike Aliye Tayari Kuolewa Na
Mvulana. Never Ever. Wavulana Wana Stress Kuliko Siafu.
USHAURI WA MWISHO
MWISHO......
- Mahusiano Yaliwekwa Na Mungu Ili Tuyafurahie, Kama Huyafurahii Rudi Nyuma Hatua Tatu Na Ujiulize Sana. Hapo Sijasema Ujilzamisihe Kuyafurahia, Tunatakiwa Kuyafurahia Automatically Ingawa Ipo Gharama Ya Kulipa Katika Kujifunza.
- Weka Nia Ya Kuyafurahia Mahusiano Yako Na Mungu Akusaidie Ufike Mpaka Ndoa Na Uifurahie Ndoa Yako.
- Kuifurahia Ndoa Yako Hakutokeo Tu Kama Popcorn Bali Lazima Ujifunze...Kwa Mwezi Mzima Tumekuwa Humu Kwenye Boyzmen Talk Kujifunza Unadhani Usingejifunza Haya Hali Yako Ingekuwaje?
- Najua Wengine Kwakuwa Mliamua Kujifunza Basi Mwakani Lazima Kuoa, Wengine Mnaoa Mwaka Huu Ni Lazima Haha Hahaha Haha Maana Mmekuwa Wanaume Sasa
- Kubali Kujifunza Kwa Faida Yako Na Ya Mkeo Mtarajiwa Hata Kama Unaoa Mwaka Ambao Yesu Anarudi
Usiache Kujifunza
·
Ila Bado Nawaangalia Nyie Ambao Mpaka Sasa Bado
Mnaendeleza Mahusiano Ya Kibabe Kwa Adam Wa Kike...Hamtaki Kuwasiliana
Nao...Mnajitambulisha Kama Single Na Huku Una Mdada Kabisa
Yaani....Nawakemea...Kama Huwezi Kujivunia Akiwa Hayupo Basi Akiwepo Atakunywa
Chai Ya Pilipili.....Ila Kama Kweli Huna Basi Na Uwe Huna Mpaka Uwe Nae
·
Kumbuka Hili:Adam Wa Kiume Ana Tatizo La
Kupenda. Adam Wa Kike Ana Tatizo La Utii. Yaweke Moyoni Mambo Haya Yatakusaidia
Kila Unapojikuta Umekosana Na Adam Wakike.
·
Pia
Kumbuka: Adam Wa Kike Anasumbuliwa Na Taarifa-Information. Adam Wa Kiume
Anasumbuliwa Na Nafasi Yake-Position. Wakati Wowote Ukiona Mambo Hayaendi Basi
Angalia Kama Uko Kwenye Nafasi Yako Au La...Na Swali Kwako Ni....Adam Wa Kiume
Uko Wapi?
·
Kaa Mbali Na Uasherati. No Sex Before Marriage
Ndio Kanuni Ya Kimungu Ya Mahusiano Salama Na Safi. No Romance Wala Kushikanashikana.
Hata Hivyo Ukimuoa Utamshika Mpaka Ujiulize Hivi Ile Haraka Ya Uvulanani
Ilitoka Wapi Kimsingi. Vumilia Na Jitunze.
·
Mungu Awashindie Na Kuwavusha Wote
GO AND PRACTICE UNTIL THEN
Comments
Post a Comment