UAMINIFU

*HATUA NDOGO NDOGO KUELEKEA MAFANIKIO*

SOMO MUHIMU KWA WOTE WANAOTAKA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA

Habari rafiki yangu mpendwa katika safari ya Maisha ya mafanikio, matumaini unaendelea vizuri kuhakikisha unafikia mafanikio makubwa katika Maisha. Mafanikio ni hitaji la kila mmoja anayeishi Hilo halina ubishi. Tatizo lipo hapa watu wengi wanahitaji mafanikio lakini hawakubali kulipa gharama sahihi ili kuyapata haya mafanikio namimi Kwa kuliona Hilo nimeamua kujipa jukumu la kuhakikisha nakupa wewe rafiki maarifa sahihi Ambayo yatakusaidia wewe uweze kufanikiwa. Ninachokuomba nikitu kimoja endelea kufuatana namimi katika mfululizo wa masomo haya kila ninapokaachini na kukuandikia wewe masomo haya wewe chukua mda wako kuweza kujifunza ya niliyo kuandalia nimuhimi sana kufanya hivyo ili kuweza kujifunza mambo mbambali Ambayo yatakusaidia Sana katika safari yako ya Maisha ya mafanikio.

Baada ya utangulizi huu mfupi sasa twende moja Kwa moja katika somo la ambalo nimependa tujifinze pamoja na somo Hilo siyo lingine Bali *uaminifu* Hilo ni somo muhimu Sana Kwa kila msafari safari ya mafanikio *uaminifu* naweza nikasema ni tiketi ya mafanikio iwapo utakosa tiketi hii sahau kuwa Na mafanikio Maishani. Hebu chukulia unahitaji kusafiri kutoka mwanza hadi kigomo alafu mkononi hauna tiketi hautaweza kupanda Gari Au ndege kuwasababu hauna tiketi yakukufikisha kule unakohitaji kufika, sasa katika safari ya Maisha ya mafanikio ni muhimu Sana ukawa Na tiketi inayoitwa *uamimi* iwapo msafari wa safari ya mafanikio hatakosa tiketi hii basi ataishia kuhangaika tu stand akijaribu kuangali magari yanavyosafiri wewe rafiki ambaye ni msafari katika basi liitwalo mafanikio kubali kulipia tiketi yako ili uwe Na safari ya uhakiki usikubali hata siku moja kukosa tiketi hii muhimu katika safari ya mafanikio.

*TIKETI YA MAFANIKIO MWANADAMU NI UAMINIFU*

Ninapozungumza uaminifu siyo neno geni Kwa watu kwasasa ni neno ambalo linazungunzwa mala nyingi Zaidi. Lakini kuzungumzwa Sana Na watu siyo sababu ya Mimi kushindwa kukuambia maana ya uaminifu. Unaweza kuweka maana yeyote kuhusu uaminifu lakini Mimi ninapozungumza uaminifu ninakuwa Na Maana nyingi lakini chache kati ya hizo nyingi ni

Uaminifu ni tabia ya kubaki kuwa mkweli Kwa mtu Au kitu Na kusimamia Ukweli Bila kujari mazingira uliyonayo. Au unaweza kusema Uaminifu ni tabia ya kutimiza ahadi uliyoahidi. Au unaweza kusema uaminifu ni Kufanya kitu katika Hali ya Ukweli na uwazi. Au unaweza kusema Uaminifu ni kufanya kitu katika unyoofu wote. Kuna maana nyingi Sana za uaminifu lakini yote ya yote ni kubaki kuwa mkweli Na kuwa Na msimamo thabiti juu ya kile unachoahidi Kwa maneno mengine ni kuwa Na msimamo usiobadilika badilika, kujiungamanisha, kujitoa kuhakikisha unasimamia kile ulicho ahadi Bila kujari ni mazingira gani unapitia wewe baki katika Ukweli kuhakikisha unatimiza kile ulichoahidi/ kile ulichopewa kusimamia katika misingi ya haki.

Baada ya kupata maana hizo kuhusu uaminifu sasa twende katika Maisha yetu ya kawaida naomba ujiulize Mimi ni mwaminifu? Hili niswali la muhimu Sana katika Maisha ya mwadamu. Ukisoma katika biblia katika kitabu cha Luka 16:10-12 Neno la Mungu linasema "Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; Na Aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi kama ninyi hamkuwa waaminifu katika Mali ya udhalimu, ni Nani atakayewapa Amana Mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminimifu katika Mali ya mtu mwingine, ni Nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?" Hilo fungu linamaana kubwa Sana Kwa Habari ya uaminifu nikwamba Aliye mwaminifu katika lililo dogo huwa mwaminifu katika kubwa pia, sasa jiulize ninambo Mangapi unayaona madogo Na unashindwa kuwa mwaminifu katika mambo hayo, katika Maisha niheri ukachagua kuwa mwaminifu Kwa sababu ukiwa mwaminifu kila mmoja atahitaji afanye kazi nawewe. Mungu naye anafungua mibaraka Kwa watu wote walio waaminimifu Kwa watu wengi Na Kwa Mungu pia, ngoja nikwambie rafiki kipindi nafikiria Kuandika somo hili nilikutana Na changamoto nyingi katika biashara zangu mbalimbali Na changamoto hizo nilizipata Kwa watu ambao niliwapa kazi wafanye nakwakuwa sikupata kufanya nao kazi huko nyuma basi niliwapa kazi ndogo ili nione uaminifu wao Baada ya Kuona uaminifu wao umekuwa mdogo nikawafukuza kazi niliyowapa nakuajiri watu wengine Baada ya kulizika Na uaminifu wao nikawapa kazi kubwa Ambayo wale wa kwanza wanatamani ningewapa wao, shida ni nini hapa shida ni uaminifu basi ndio maana biblia inatuambia kuwa "kama hamkuwa waaminimifu katika Mali ya mtu mwingine, ni Nani atakayewapa Amana Mali ya kweli?". Rafiki uenda unahangaika kutafuta ajira lakini haupati shida siyo kwamba ajira hauna shida ni uaminifu wako, uenda unafanya biashara Na wateja mwanzo wakikuwa wanakuja Kwa wingi lakini sasa wamepotea unahisi Kuna watu wamekurogwa rafiki hakuna aliyekuroga Bali umejiroga wewe mwenyewe Kwa kukosa uaminifu, huenda wewe ni fundi mzuri Sana iwe fundi kushona/fundi selamala/fundi ujenzi/fundi Mashine yaani incubator licha ya ubora wako katika ufundi lakini unakosa wateja shida siyo nyingine Bali ni uaminifu.

Kuwa mwaminifu nimtaji mkubwa Sana Kwa katika safari ya mafanikio ndio maana nikaita tiketi ya mafanikio ni uaminifu Je wewe ni mwaminifu kwenye kazi yako? Ngoja nikwambie watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika Maisha yao Kwa Sababu ya kukosa uaminifu unamkuta mtu anashona nguo unampelekea nguo Na anakuahidi njoo siku fulani lakini ukienda siku Ambayo anakuahidi unakuta haja shona bado yaani unakela wewe fundi acha kabisa hata huokosi Sababu eti kilikwenda kimerudi huo niukosefu wa uaminifu Na ukikosa wateja unaanza kulalamika kwamba umerogwa kweli? Kwa staili hiyo unadhani kesho nikihitaji kushona nguo nitafikaje kwako? Uaminifu nikitu cha msingi Sana Kwa Maisha ya Kila mwanadamu chagua kuwa mwaminifu kuwasababu ukiwa mwaminifu utavutia watu wengi kuwa Kuja kwako unavuta fulsa nyingi Kuja kwako, unavuta Baraka za Mungu Kuja kwako yote hii inatokana Na uaminifu wako uliojijengea.

Nimekuwa nikifanya biashara Kwa mda mrefu sasa nimekutana Na watu wengi Sana katika ulimwengu wa biashara nimejua tabia za watu wengi Sana kuwa siyo waaminifu ndio maana hawafanikiwi hata siku moja, Kuna mzee mmoja yeye ni fundi mzuri Sana lakini amekuwa Na changamoto kubwa ya kupata kazi licha ya ufundi wako kuwa mzuri shida kubwa inayomsumbua nikushindwa kuwa mwaminifu Kwa wateja Na hii imempelekea kushona kufanikiwa nakuishia kuishi Maisha yakuunga Unga tu basi.

Rafiki iwapo utashindwa kuwa mwaminifu sahau kuhusu mafanikio katika Maisha yako. Utaishia kubaki unahangaika tu Maisha Bila kufanya kitu cha maana. Sasa kwanini uhangaike namna hiyo wakati unayonafasi kubwa ya kufanikiwa katika Maisha yako iwapo tu utakuwa mwaminifu katika jamii.

Uaminifu unalipa Sana Kuna kipindi nilienda maeneo fulani kufanya biashara kiukweli nilifanikiwa Sana Kwa katika biashara zangu Kwa maeneo hayo sasa Baada ya kufanya biashara Kwa kipindi fulani nilitakiwa kuondoka sasa Kuna watu waliona jinsi nilivyokuwa Na fanya vizuri katika biashara yangu katika maeneo hayo Baada ya Mimi kuondoka nayeye akanza kufanya biashara hiyo nikwambie nini kilimkuta haikumchukua mda aliacha kufanya biashara katika maeneo hayo kitu kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri kwenye biashara Ambayo Mimi nilikuwa nafanya vizuri ni uaminifu pekee, alishindwa kuwa mwaminifu Kwa vitu vichache matokeo yake akafunga biashara yake.

Naiona fulsa kubwa ya kazi katika taifa letu Naiona fulsa kubwa ya biashara katika taifa letu nayaona mafanikio ya watu wengi katika taifa letu kikubwa ni kuandalia tabia zako Je wewe ni mwaminifu kweli kama Kuna mahali umajiona siyo mwaminifu basi badilika rafiki kuwasababu ukiwa mwaminifu utavuta fulsa kubwa ya mafanikio Maisha mwako.

Ngoja nikuulize rafiki umewai kuona mtaani kwako Kuna mafundi wengi wakujenga lakini fundi mmoja yeye hakosi kazi kila ilitokea lazima afanye yeye Tena Kuna wakati unafikia mtu anahitaji kujenga nyumba lakini fundi huyo yupo bise nakazi anakubali amsubili yeye akimaliza ndipo amjengee licha yakuwepo Kwa mafundi wengine ambao hawana kazi, ukichunguza Kwa undani utakuja kugundua fundi huyo ni mwaminifu Sana tofauti Na mafundi wengine. Sasa kwanini wewe usiwe mwaminifu katika kazi yako? Hivi hujawahi kuona mpo watu wengi kazini ambao mlianza kazi pamoja likini mmoja wenu kila ilitokea Nafasi yakupandishwa cheo anapandishwa yeye unajiuliza kwani sisi basi hatuoni? Siyo Kwamba hawaoni shida ni kwamba amewaona siyo waaminifu hivyo anaogopa akiwapa Nafasi kubwa katika kazi mtamwibia Zaidi. Sasa Kwa nini upoteze kupandishwa cheo kwasasa ya jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako, Aaaaaah! Rafiki usiniangushe Bana hebu onesha uaminifu wako Na watu wakupe fulsa za Kukuwezesha wewe Ufanikiwe Zaidi.

Hivi umeshawahi kujiuliza Kwanini ndoa nyingi hazifanikiwi ila chache tu ndizo zinazofanikiwa shida ipo hawa wanandoa wengi siyo waaminifu hata kidogo hii inampelekea Mungu ashindwe kuwabariki, hebu fikiria kwenye ndoa baba mwizi anaiba Mali za ndani nakwenda kuuza ili akafanyie umalaya wewe unadhani Mungu anapendezwa Na tabia hizo? Hapana hata hapendezwi Hata kidogo, sasa unaweza kujiuliza ni Kwanini Mungu anashindwa kuwabariki jibu ni kuwa anafanya hivyo Kusudi uache makosa yako, uaeche tabia yako yakutawanya Mali uachane Na michepuko. Hivi unadhani kwanini kwenye biblia imeandikwa aliyemwaminifu katika vidogo pia atakua mwaminifu katika vikubwa pia Na aliye dhalimu Kwa vidogo atakua dhalimu Kwa vikubwa pia alichokuwa anamaanisha uaminifu unapimwa kwanza Kwa vitu vidogo kwahiyo Mungu anapopima ndao yako nakuona Kuna udhalimu katika vidogo alivyokupa hawezi kukuongezea kuwasababu vile vidogo alivyokupa umevitumia vibaya anakupaje vilivyo vingi? Hebu badilika rafiki Anza upwa mwenendo wa ndoa yako Na Mungu atawabariki Sana.


Naomba nimalize Kwa kusema kuwa Leo hii nenda Kubadili njia zako iwapo kama umeamua kufanikisha kweli katika Maisha yako, nenda kawe mwaminifu la katika maeneo makubwa Sita alafu njoo Na unipe ushuhuda jinsi Maisha yako yatakavyoenda Kubadilika.

*MAENEO SITA MUHIMU YA KUJENGA UAMINIFU KATIKA MAISHA*

1) ENEO LA KAZI/BIASHARA
hili nieneo muhimu Sana Kwa manufaa ya biashara yako. Katika eneo hili hakikisha unaendesha biashara zako katika msingi wa uaminifu Kwa wateja wako. Jinsi unavyoendesha biashara kila mmoja ajue kuwa hakuna chochote anachoibiwa kwao. Fanyia kazi eneo hili alafu njoo nipe ushuhuda.

2)VITU/PESA

Kumtolea Mungu juu ya vile alivyokujalia ni jambo la muhimu Sana katika kutengeneza msingi wa mafanikio yako, kuwa mwaminifu Kwa vile vichache ambavyo Mungu amekujalia Na yeye atakubariki Sana Katika Maisha yako. Hebu twende tukasome pamoja katika bibilia katika kile kitabu cha malaki 3:10 inasema "leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu Kwa njia hiyo, asema BWANA the wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni Baraka, hata pasiwepo Nafasi yakutosha Au la". Nini unajifunza hapa nikwamba utoaji ni jambo la uaminifu Kwa Mungu naye Mungu ni mwaminifu Na chochote anachoahidi kwetu huwa anakiteleza Bila ya shida yeyote. Nenda kaonyeshe uaminifu Kwa Mungu kupitia Mali alizokubaliki Na yeye ameahidi akukufanikisha hebu chukua hatua sasa.

3)ELIMU/UJUZI

Je unatumiaje elimu/ujuzi wako? Je unatumia Kwa uaminifu katika kutatua matatizo ya jamii husika Kwa uaminifu Au unatumia hovyo kuwasababu unao ujuzi? Je jamii yako Inanufaika nawewe kuwa Na ujuzi ulionao Au haifaidiki Na chochote? Rafiki jinsi unavyotumia ujuzu/elimu yako itaamua mafanikio yako yatakuwaje, Na siyo kutumia Kwa mazoea hapana tumia ujuzi wako wote kuhakikisha jamii Inanufaika Na ujuzi wako, fanya yote Kwa uaminifu Baada ya mda njoo Na ushuhuda wako naamini kabisa Maisha yako yatabadilika Sana.

4)MANENO YAKO.

Je unatumiaje maneno yako katika jamii yako? Je meneno yako Kwa jamii yako ni yakujenga Na kuinua jamii Au maneno yako yakuifarakanisha jamii? Je ahadi zako unazoahidi ni za kweli Au umekuwa Na ahadi zauongo zisizo Na utekelezaji? Rafiki ikiwa unataka kupanda basi hili la kuelekea mafanikio ya kweli hakikisha unakuwa mwaminifu katika kunena kwako, unakuwa mwaminifu katika ahadi zako, jamii inufaike Na maneno yako. Kunena kwako Mbele ya jamii kunaamua Mafanikio yako yatakuwaje.

Ngoja nikazie kidogo hapa hivi itokee Kuna vijana wawili mtaani mmoja maneno yake kila siku ni yakujenga, anamaneno yakutia moyo Sana, anajua kutengeneza mahusiano bora Na watu ni mtu ambaye kweli yake huwa ni kweli haswa ni mwaminifu Kwa kila kitu Na mwingine maneno yake kila siku ni yakukatisha tamaa, maneno chonganishi, kweli yake siyo kweli. Sasa swali ni ilitokea unanafasi moja ya kazi Ambayo unatakiwa kumpa mtu mmoja wa hapo mtaani kwako utampa Nani? Najua kila mmoja angependa kufanya biashara Na kijana wa kwanza kuwasababu ya maneno yake Na tabia yake, inavutia wengi kumpa kazi.

Sasa mfano huo huo ulete kazini wewe ni bossi Na changamoto unao wafanyakazi wengi likini unahitaji mmoja umpandishe cheo kati ya Hao wawili utamchagua Nani? Najua jibu unalowewe mwenyewe basi Maisha yako yote kama umechagua kupanda Gari la safari ya mafanikio Katika Maisha yako.

5)MUDA

Hili ni eneo lingine muhimu Sana katika kujenga uaminifu katika Maisha yetu, unautumiaje mda wako je unautumia Kwa manufaa ya biashara yako/mafanikio yako. Jinsi unavyotumia mda wako Kwa uaminifu ndivyo unavyojenga msingi imara wa mafanikio yako.

Hivi biashara zako unafungua saa ngapi? Je unao mda sahihi wakufungua bias zako, je kila siku unafungua biashara yako Kwa mda huo huo Au hauna mda kamili? Biashara nyingi hazina za wa Afrika hazina Muda sahihi wakufungua biashara zao, Leo utakuta wamefungua biashara saa mbili Na saa saba wamefunga, sasa tisa wanafungua Tena ikifika saa moja tu wamefunga Tena hadi kesho ambaye atafungua saa nne Asubuhi. Najua wewe nishahidi huu ni kukosa uaminifu katika mda uliopewa na Mungu. Rafiki watu wote unaowaona wamefanikiwa katika Maisha yao walikuwa waaminifu Kwa Habari ya mda, hawakukubali kupoteza mda ovyo.

6)NDOA
Hili Ni eneo Muhimu kwa habari ya mafanikio ya mwanadamu iwapo utakosa uaminifu katika ndoa nindra sana kufanikiwa kama wewe ni mwanandoa ishi katika ndoa yako kwa uaminifu pangeni mambo pamoja kila kitu mnachokifanya katika maisha yenu fanyeni katika msingi wa uaminifu. Mungu atabariki ndoa yako  iwapo mtakuwa waaminifu katika ndoa yako.


Kwa leo tuishie hapa tukutane wakati mwingine kwa masomo mengine.


Ni Mimi Rafiki yako
FRANK MAPUNDA
0758918243/0656918243
Nimeandika kitabu cha UFUGAJI WA KUKU KIITWACHO *TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*
Karibu upate nakala yako

Softcopy 7000/=
Harcopy 12000/=

Comments

Popular posts from this blog

KULIISHI KUSUDI LA KUUBWA.