KULIISHI KUSUDI LA KUUBWA.
KULIISHI KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO
UTANGULIZI.
Shalom, Naitwa Shemeji Melayeki,Ninaishi Arusha Mjini. Nimeoa. Nina mke mmoja (mwanamke) aitwaye Neema na kubarikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye David. Ni mwandishi wa vitabu hadi Sasa ni sita kwa idadi
1.Principles of Growth,
2.Principles for Greatness,
3.The power of Vision,
4.The power of taking the first step
5.The power of Reading Books na
6.Nguzo za Siku Msingi wa Kwanza,
Pia nafanya makongamano mbali kwa kuandaa na kualikwa.
Ninafanya kazi huduma ya Global Family Gatherings Ministries kama Apostle kwa sasa nasimamia kanisa la Arena of Greatness Arusha.
Kuhusu kufundisha juu ya Kusudi nimeanza 2012 kwenye makongamano/semina mbalimbali na baadaye kuanzisha *Online Discovery Seminars* nikifundisha Somo hili kwa undani zaidi.
*Ikibidi nitawaomba Discovery Team wanisaidie baadhi ya vipengele*
Ninaona Somo hili ni Somo Muhimu hasa baada ya Mtu kumpokea Yesu ni vyema akafahamu kwa nini yuko duniani..
Uzoefu wangu unaonyesha kuwa Somo hili ni gumu na ni rahisi...
Ni rahisi kwa kufundisha lakini ni gumu kwa sababu huwezi kumwonyesha mtu kilichoko ndani yake ila tu utamweleza namna ya kutambua na kuvumbua vitu vilivyojificha ndani yake
Lengo la Somo hili ni kukufungua macho ili uone...
Pia, kukufanya upanuke uelewa juu ya Kusudi la Kuumbwa kwako kwa manufaa yako na watu wengi wanaokuzunguka!
Somo hili lina vipengele vya maswali utakayojiuliza na kuuuliza hata wengine
Somo hili halimfai kabisa mtu ambaye hayuko tayari *kutulia na kutafakari maisha yake kwa kina*
Somo hili pia halimfai mtu ambaye hayuko tayari kumwomba Mungu aliyemuumba kwa habari ya Kusudi la Kuumbwa kwake
Somo hili halimfai mtu asiyetaka kukubali ukweli kwamba inawezekana hapo alipo yupo nje ya Kusudi la Kuumbwa kwake kwa sababu moja au nyingine
Somo hili halimfanyi mtu akimbilie kuacha kufanya mambo anayoyafanya mfano kuacha kuajiriwa na kuanza biashara au kuacha biashara na kutafuta ajira bali linakupa mwanga wa kuona mbele yako na ikiwa itakubidi kubadilisha unachokifanya (kwamba ulikuwa nje ya mstari) utafanya kwa kufuata ushauri wa kitaalamu (NAVIGATION PROCESS) ili uweze kuvuka salama..
Hii ni kwa sababu nimeona watu wengi baada ya kufundishwa somo hukurupuka na kuteseka bila kujua.
Somo hili pia halitafundisha namna ya kuliishi Kusudi (specific purpose) ila namna ya kutambua ili uweze kuliishi kwani kila Kusudi la mtu lina Workshop yake, hivyo baada ya kutambua ni vyema kujifunza namna ya kuwa Bora katika eneo lako...
Somo hili lina lengo la kuwasaidia watu kupata majibu ambayo mara nyingi hujiuliza bila kupata majibu
Kati ya maswali hayo ni...
1. Kwa nini niko duniani?
2. Hivi, hiki ninachokifanya ni mpango wa Mungu kweli?
3. Kwani kipaji changu hasa ni kipi?
4. Ni jambo gani naweza kufanya vizuri sana?
5. Sina furaha na maisha. Ni jambo gani litanipa furaha?
6. Nawezaje kuishi kusudi la Mungu maishani mwangu?
Kwa sababu.....
“Kusudi la kuwepo duniani ni muhimu kuliko maisha yako. Ndiyo maana kulijua kusudi la Mungu ni ulinzi wa kwanza kabisa katika maisha”
*UTANGULIZI HUU NI MUHIMU KULIKO SOMO LENYEWE*
Baada ya kutuma mambo ya kuzingatia naomba mitume *UTANGULIZI juu ya Somo letu*
Pesa na Umaarufu huwa ni matokeo ni kama harufu ya pilau ukilifuata Kusudi la Kuumbwa kwako na kufanya kiukamilifu; vitu ambavyo wengine wanajiumiza kuzitafuta zinakufuata!:
Changamoto kubwa kwenye duniani ya Leo ni msisitizo mbovu kwenye matokeo badala ya process ya kuleta matokeo au chanzo cha matokeo hayo.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; *wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.*
Hii ni sawa na kusema-Na tutengeneze simu *itumike kutumia SMS, kupiga na kupokea calls, kumulikia na kuonyesha muda*
Hapo Mtengeza simu atakuwa alianza kuwaza nini?
Sababu, Nia ya kufanya jambo ina nguvu kuliko jambo LENYEWE
Intentions are powerful than actions!
Mungu aliumba Dunia iwe kama Perfect Ecosystem!..
Kila mtu akisimama kwa nafasi yake kusingekuwa na haja ya kusukumana, kushindana wala kunyang'anyana
Kila mtu angekaa kwa safu yake! *Tungekuwa kama hawa*
Yoeli 2:7-8. Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao.[8]Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao.
*Kama kutakuwa na maswali mpaka hapa nilipoishia *
Kwa hiyo uwe HURU kuuuliza!...
Swali la kwanza: Kwani ukishajitambua ndani ya Mungu ni lazima ufanye kazi ya madhabahuni tu?? Ni kitu ambacho huwa kinachanganya wengi sana, Mwl naomba utakielezea kwa ufasaha,, maana kuna watu hawezi kuingia kwenye siasa sababu ni mtu wa Mungu, mtu hawezi sijui fanya nini na nini nje ya madhabahu anaanza kuona hafanyi kusudi la Mungu,, na vingine vingi,, naamini darasa hili litatoa jibu nzuri
UKIJIBU HILI, KATIKA MAELEZO YAKO JIBU NA HILI
"Je ni dhambi mtu alieokoka kujiunga kwenye chama cha *upinzani* maana kuna mwanzo nilikua katika chama cha upinzani nikawa napata ugumu kuelezea mbele za watumishi wenzangu maana ilionekana kama nakosea sana!! Ikanibidi nihame ili kupata Amani ya kumtumikia Mungu,, ila ukweli hata huku niliko hakuna tofauti na nilikokua,,maana bado bado vikao vya mbinu za ushindi ni maudhi mbele ya mungu? Napenda sana siasa ili kwa mtindo wa siasa za kiafrika naona kwa muamini wa kweli inahitaji moyo, na ujasiri wa kumuweka kristu mbele,,, Bado napenda kusonga mbele katika siasa maana ukweli napenda kuwakilisha na kusimamia rasimali za watanzania je unanishauri vipi?
Shemeji Meleyeki-Atoa jibu: Biblia ina viongozi wa kisiasa wengi kuliko hata wahubiri!
Ninaposema viongozi wa kisiasa namaanisha watu kama akina Sauli, Daudi, Daniel, n.k ambao pia walikuwa wacha Mungu!
Swali ni KWA NINI UNAENDA KWENYE SIASA? (KUSUDI LAKO HUKO NI NINI?)
Kusema siasa ni dhambi na kila mwezi una maombi ya kuombea *Raisi Mungu amwongezee hekima atuongoze vizuri* ni ukosefu wa hekima ya Hali ya juu!
Kumwombea mkulima alime vizuri na huku unajua kulima ni dhambi ni ugonjwa...
*Huhitaji kuwa madhabahuni ili uliishi Kusudi la Mungu*Unaweza ukawa unashona kama Dorcas tu!.
Siyo kila mtu asiye na kitu cha kufanya hana cha kufanya ila *mwingi hajui cha kufanya* Mtu akijua Kusudi la Kuumbwa kwake atakuwa na njia nyingi za kulifanikisha
Leo sehemu nyingi sana kipaumbele cha Kusudi la Kuumbwa kwa mtu halipewi kipaumbele. Umewahi kusikia maneno haya?
*Chagua kozi yenye mkopo*
*Chagua profession ya heshima*
*Somea kitu hiki kinalipa*
*Soma kozi hii ina ajira ya moja kwa moja*
*Omba kazi hii ina madili mengi*
HAPO MTU ANAAMUA KUFUATA MAMBO AMBAYO PENGINE HAKUUMBIWA KWA SABABU MBALIMBALI
Matokeo yake watu wanaanza kubanana sehemu fulani Fulani
Kuna sehemu zimeachwa na kuna sehemu watu wamebanana na wanazidi kubanana kwa sababu,Wamekuwa Mislead (wamepotezwa wasilione Kusudi) Au Confused wamechanganyikiwa hawajui kipi wafanya kipi waache Au wameacha Kusudi (avoid) na kukimbiza mambo mengine\
Au hawajatambua (undiscovered) Kusudi la Kuumbwa kwao. So, wengine wanakuwa UNEMPLOYED
MISPLACED
RIGHT PEOPLE WRONG PLACES
Kila mtu angefuata Kusudi la Kuumbwa kwake, kila mtu angekuwa na Cha kufanya
Wengine wanajua tuko duniani tunajiandaa kwenda mbinguni
Ingekuwa ni upotevu wa rasilimali Mungu kutuleta duniani ili atuandae Kwenda mbinguni.
Hatuko hapa kwa bahati mbaya
10500/70 actually maisha ya watu wengi ni trial and error.
Picha hii ina mambo mengi ya kujifunza kuanzia kwenye Kusudi vs Muonekano Vs Uwezo!
*Baada ya Kumaliza UTANGULIZI Kwa sasa naomba nimkaribishe Mentee Noel Pallangyo afundishe kidogo juu ya Maana ya Kusudi*
NAWASALIMU WOTE KWA JINA LA YESU.....
Ninaitwa Noel Pallangyo, niko Morogoro kwa sasa na niko na huduma yangu inayoitwa World Change Initiators. Ninamshukuru sana Kaka yangu na Mentor wangu Shemeji Melayeki kunipa hii nafasi.....
Karibuni tujifunze kwa habari ya kusudi japo kwa ufupi....
*KUSUDI LA MUNGU KWENYE MAISHA YA MWANADAMU.*
Nataka tuangalie kwa ufupi kwenye hili eneo la kusudi angalau tuweze kuongeza ufamu zaidi tena tukijua sehemu sahihi ya kupata taarifa ni kwa muumbaji wetu ambaye ni Mungu kwenye neno lake.
=KUSUDI ndilo maisha ya mtu na maisha ya mtu ndilo kusudi la yeye kuumbwa.
=Huwa nasema hivi “Mungu huwa anaumba kusudi, halafu kusudi linamuumba mtu” Kwa maneno mengine, kilichosababisha Mungu akuumbe ni baada ya kuona uhitaji wa kitu fulani kukamilika au kufanyika hapa duniani, ndipo akaitengeneza inaitwa kusudi; akaanza kuangalia mtu wa kulibeba hilo kusudi ndipo akakupata wewe.
=Kwa hiyo ukiweza kujijua kusudi la maisha yako, basi umeyapata maisha yako.
*KUSUDI NI NINI?*
Ni sababu ya wewe kuumbwa na kuzaliwa hapa duniani. Ni ile sababu ya wewe kuwepo kwenye kizazi hiki, kuzaliwa Tanzania au nchi uliyozaliwa, kuzaliwa kwenye hiyo familia, kuzaliwa na hiyo sura yako, kuzaliwa na hilo umbo lako….nk
KUSUDI linatengeneza wito….. Mungu alikuleta kutoka alikokuwa amekuweka ili uje kutimiza kazi fulani.
WITO - ni haja iliyopo inayomsukuma anayeitaka ifanikiwe akiite.
Kusudi ni sababu ya wewe kuumbwa lakini inaanza kuhesabiwa pale unapozaliwa hapa duniani.
Kuzaliwa ni wito kabisa, ile kwamba umezaliwa maana yake umeitwa tayari na Mungu kwa sababu ameona uhitaji wa kitu ambacho ameshakiweka ndani yako ili ukakifanye hapa duniani.
Hebu fikiri ni wangapi leo hii wanajua kwanini walizaliwa na wanafanya nini kulingana na vile walivyoitiwa kuvifanya?
KUSUDI linalenga wajibu wako ambao Mungu anataka aukamilishe hapa duniani, kwa hiyo anamtafuta mtu wa kulikamilisha ndiyo lazima aweke ndani yako wa kukamilisha kile alichokutuma kukifanya hapa duniani
Unapoishi kwa kufanya kile ulichojaliwa uwezo nacho kukifanya na kukifanya katika njia sahihi hapo ndo tunasema unaliishi kusudi. Watu wanaposhindwa kujua kusudi la maisha yao au vitu walivyonavyo na vilivyowazunguka, ndipo inatokea uharibifu kila siku.Kama hujui kwa nini uliumbwa mweusi utaanza kujichubua ili uwe mweupe, kama hujui kwa nini ulipewa ilo umbo nzuri utaanza kuwa malaya maana utasumbuliwa na wanaume sana. Kama hujui kwanini umepewa huo uwezo wa kuimba utautumia kuinua na kutangaza kazi za kidunia na uovu na hatimaye kusababisha maadili yaporomoke sana kwa jamii yako.
Fikiri ni watu wangapi leo hii Mungu aliwapa vipaji mbalimbali ikiwepo nguvu ya ushawishi ndani yao na wameitumia kuharibu jamii kubwa ya wanadamu, kwa kile kile Mungu alichowapa ili waijenge jamii badala yake imekuwa kinyume.
*KISUDI LINAKWENDA NA VITU VIFUATAVYO….*
##Mahali sahihi
##Kitu sahihi
##Muda sahihi
##Njia sahihi
Vinginevyo lile lile kusudi linaweza kugeuka likawa sumu kwenye maisha yako na ya wale waliyokuzunguka. Hiyo ni nguvu ya ajabu sana ya kiungu aliyoiweka kwa kila mwanadamu chini ya jua hata kama anajua au haujui, anamwamini Mungu au amwamini Mungu…….kanuni inafanya kazi kwa wote………..
*KAMA UNATAKA KUJUA KUSUDI LA KITU CHOCHOTE LAZIMA UMUULIZE ALIYEKITENGENEZA.*
Kwa mfano, huwezi kwenda kuulizia spea ya lap top yako ya dell wakati unatumiaToshiba…..kwa sababu ni kampuni mbili tofauti na zina miundo tofauti ya bidhaa zao.
Vivyo hivyo wewe unatoka kwa Mungu na chanzo chako ni Mungu, ukitaka kujua kwanini upo duniani muulize Mungu ndiye anayo majibu sahihi kwa ajili ya maisha yako
Hebu angalia hapa Mungu anavyosema,
“Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni. Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu
mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru”* ISAYA 45:11-12.
Yeye pekee ndiye aliyekuumba na yeye pekee ndiye mwenye taarifa sahihi zaidi kuhusu maisha yako, siyo wazazi wako wala mchungaji wako, wala mwalimu wako, au daktari au rafiki yako.
Hawa wanakusaidia tu kukupa taarifa sahihi kuhusu namna ya kumtafuta Mungu ili akupe majibu sahihi kuhusu maisha yako.
KUSUDI LINA UHUSIANO MKUBWA NA MUDA.
Kusudi limefungwa kwenye muda, ukicheza na muda wako unacheza na kusudi, na ukicheza na kusudi unacheza na maisha.
Kuna mambo mengine huwezi kuyafanya baada ya kuwa kijana, ulikuwa unayafanya utotoni tu. Pia ukisha kuwa mzee kuna mambo huwezi kuyafanya kama ulivyokuwa kijana.
Vivyo hivyo kusudi limefungwa kwenye muda, lazima ujue muda wako una thamani sana na mtu yeyote aliyekwisha kujua kusudi la maisha yake anautunza muda sana na anauheshimu kweli kweli.
Hebu angalia huu mstari;
MHUBIRI 3:1 *“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”* Kwa maneno mengine kila kusudi limefungwa ndani ya muda wake, huo muda ukiisha kusudi halifanyi tena kazi.
Yesu pia akasema; YOH 9:4 *“Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu”*
Mchana wako ni kipindi cha uhai wako, ukicheza na muda huu uliyonao kusudi lako linabaki vile vile sijui utaenda kumjibu nini Mungu.
Anaposema muda aishipo hapa ulimwenguni yeye ni nuru ya watu, maana yake na wewe kumbuka Yesu alituita nuru ya ulimwengu na namna pekee ya kuwa nuru ya ulimwengu ni kule kuliishi kusudi la maisha yetu.
Sasa unaweza kuelewa ni wangapi wanaoishi wakiwa awaangazi kabisa na ndiyo maana dunia bado ipo gizani kwa sababu waliyoitwa kuwa nuru wameyakimbia majukumu yao ambayo ni kusudi la wao kuumbwa.
Shemeji Meleyeki: Baada ya kujifunza juu ya Kusudi kwa ufupi najua swali lililopo kwenye akili za wengi ni
*Nitatambuaje Kusudi?*
Ndiyo maana Yeremia aliambiwa ,Yeremia 1:5,Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Baadhi ya Maswali yaliyoulizwa....
1. Kusudi ni nini-Limeshajibiwa
2. Je kusudi la kuumbwa kwangu linafanana na mwingine? -Limeshajibiwa
3. ule mstari wa enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu ni Agizo au kusudi la kuumbwa kwetu?
Swali la pili: Nataka kujua wakati Yesu anawaita wanafunzi wake kwa ajili ya kuutangaza ufalme wa Mungu aliwakuta wakifanya kazi zao,wengine walikuwa wavuvi,watoza ushuru nk, katika maeneo mbalimbali,Je walikuwa nje ya kusudi au kule Yesu kuwaita inatufundisha nini ,ukihusianisha na darasa letu hili??
*Nitajibu na hili pia*Shemeji Meleyeki Said:
3. Ule mstari wa enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu ni Agizo au kusudi la kuumbwa kwetu?
*Jibu* Agizo Kuu (Great Commission)
Mambo haya ni Muhimu kuyajua
Maisha yalikuwepo kabla ya agizo Kuu hii ni sawa na Kusudi lilikuwepo na lingeendelea kuwepo hata kama agizo Kuu kusingekuwepo.. (Muhimu tu watu waendelee kuzaliwa)
Kila mtu kwenye nafasi yake anaweza kufanya agizo kuu
Wengi wanafikiri Agizo Kuu linahusika na kuhubiri watu waokoke *hiyo ni finyu* sana Agizo Kuu linahusisha kutengeneza wanafunzi (Disciples not Students)
MWANAFUNZI Aina ya Disciple hatengenezwi kwa kufundishwa bali kwa kufundishwa na kuonyeshwa namna ya kuishi maisha ya kila siku..
*NB* unavyoishi kila siku unatengeneza *Disciples*
Kumbuka mfano wa Chachu (hamira) au Nuru au Mbegu ya Haradali .Unaweza kuishi Great Commission ukiwa ofisini, shambani, shuleni, unavyoongea, unavyojichanganya na watu n.k.
NAMNA MUNGU ALIVYOPITISHA KUSUDI KWA BAADHI YA WATU
*Yesu- Mama yake* via malaika
Mathayo 1:20-21
[20]Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.[21]Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, *maana,* yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
*Samsoni- Mama yake* via malaika
Waamuzi 13:2-5. Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.[3]Malaika wa BWANA akamtokea yule
mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.[4]Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;[5]kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; *maana* mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; _naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
*Yeremia* Yeye Mwenyewe ...
Yeremia 1:5,10.Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; *nimekuweka kuwa* nabii wa mataifa.[10]angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
*Yohana -Baba yake* via Malaika
Luka 1:7-17.Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.[8]Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu,[9]kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.[10]Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba.[11]Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.[12]Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.[13]Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.[14]Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.[15]Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.[16]Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.[17]Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa._
*Sauli -Anania* via Maono
Matendo ya Mitume 9:10-12,15-16. Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.[11]Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;[12]naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.[15]Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.[16]Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu._
*Yusufu - Ndoto*
Mwanzo 37:5-10 [5]Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;[6]akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota.[7]Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.[8]Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.[9]Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.[10]Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?
Mwanzo 45:7-8. [7]Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.[8]Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
Katika kutambua kusudi la kuubwa kwako kuna mambo mengi lakini nimeyagawa katika sehemu tatu;
Kuangalia utofauti wako
Kumuuliza aliyekuumba(Inquiry prayer) Au
Kufanya vyote.
Shemeji Meleyeki: Leo tunarudi kwenye namba *1) Kuangalia utofauti wako* baada ya kumaliza ya Kumuuliza aliyekuumba.
*Utofauti wako umebeba angalau mambo matatu yanayohusiana na Kusudi*
1. Shauku (Passion)
2. Uwezo (ability)
3. Uhitaji (Demand)
*Shauku (Passion)*
Ni kama mchanganyiko wa kupenda/kuchukia hali Fulani ambayo mara nyingi husababisha msukumo wa ndani wa kutaka kuona kitu Fulani kinatokea au kinabadilika. Kama vile Habakuki alivyokuwa anaumia na hali ya nchi kisiasa na kiuchumia au Musa na mateso ya ndugu zake au Nehemia na hali ya ukuta wa Yerusalemu..
Hawa walikuwa na mwitikio wa TOFAUTI na watu wengine wakati huo!
*Walikuwa na Shauku*
Aina ya shauku huelezea Aina ya Kusudi
Mfano: niliposema *Nina Project ya kuhakikisha Wamasai 200 wanaokoka mwaka huu*
Walijitokeza watu wa Aina tofauti... Hali moja miitikio TOFAUTI.
1. Wengine walianza kunitia moyo kwa nguvu sana
2. Wengine wakaamua kufika eneo la tuki
3. Wengine walianza kuongoza maombi
4. Wengi walianza kukusanya fedha za kusapoti
5. Wengine walinionea huruma pia
*Jambo moja bila kujua watu wameona TOFAUTI*
Shauku pia yaweza kuwa hamu au ni hisia za ndani ambazo mtu anakuwa nazo juu ya jambo fulani.
*Ukijiuliza maswali yafuatayo kuna mambo utayagundua*
Kitu gani kinacho kufurahisha ama kukuvutia sana kukiona watu wakiwa nacho
Kuna nini unapenda kuona watu wakikipata. Lakini pia inaweza kuwa kinyume chake, jiulize kitu gani kinakukera kwenye jamii au watu wanaokuzunguka na ungependa kuto endelea kuwepo.
Kunaweza kuwa na hali ambayo ipo mahali ulipo lakini hakuna nayeona kuwa ni tatizo isipo kuwa wewe. Au inawezekana kuna hali ambayo haipo na kila mtu anaona ni kawaida isipo kuwa wewe. Ukiona hivyo, basi upo uwezekano kuwa wewe upo hapo kwa sababu ya hiyo hali. Inaweza kuwa kwenye jamii, Taifa au hata Dunia kwa ujumla.
Wakati mwingine unaweza ukajiona kama hilo ni jambo kubwa kukuzidi na kwamba hutaweza kubadilisha lolote. Huo siyo ukweli. Maadamu umeweza kuwaza, unaweza kufanya. Mtu mmoja aliwahi kusema ..’Kama unajiona wewe ni mdogo sana kuweza kufanya mabadiliko, jaribu kulala na mbu chumbani’
Usikubali kujiona mdogo kuliko tatizo lako. Kile unacho kifikiria na kukiamini una uwezo wa kukifanya kabisa.
Unapenda kufanya nini?
Jiulize ni jambo gani ambalo unapenda kulifanya, hata kama linaonekana halina faida inayo onekana kwako, lakini unahisi kuridhika nafsini unapo lifanya. Wakati mwingine linaweza hata kukugharimu muda, nguvu na hata fedha lakini unapenda kulifanya. Unalifanya siyo kwa kutaka umaarufu au fedha, bali unalifanya kwa kujiridhisha nafsi yako.
Inaweza pia kuwa ni jambo ambalo hujalifanya, lakini unatamani kweli kulifanya kwa gharama yoyote, basi tu hujaweza kupata nafasi ya kulifanya.
Unavutiwa na nani?
Pia shauku yako inaweza kuwa kutaka kufanya kama anavyofanya mtu fulani. Hapa sina maana ya kutaka kuiga bali namaanisha kupata hamasa kutoka kwa mtu fulani na kuyapenda mafanikio yake kwenye eneo fulani. *Shauku inaweza Ku dictate angalau sehemu hizo 3*
Baada ya kufundisha sehemu ya Shauku naomba nimkaribishe Mwalimu Mwingine *Severina Gabriel Kalukule*
Karibu sana Severina!
Severina: Leo tutakuwa pamoja kwenye somo la *KIPAJI*
💥Mimi ni *Severina Gabriel Kalukule* ni *mwandishi* wa vitabu, nimefanikiwa kuzindua kitabu changu cha kwanza kinaitwa *"Ishi Maisha ya Thamani "*, *mnenaji*, pia ni *mwalimu* by professional currently nafundisha Star High School Arusha, ni *mwanajamii/ mwanamabadiliko* (napenda kuona mabadiliko kwenye jamii inayonizunguka).
Severina: Hongereni sana kwa kuwa na zawadi.
Maana kipaji ni zawadi kutoka kwa Mungu.Ni zawadi ambayo kila mtu anazaliwa nayo.
*KIPAJI* *Maana ya Kipaji*
💥Kipaji ni kufanya kwa urahisi kitu kuliko watu wengine. Au
💥Kipaji ni uwezo wa asili ndani ya mtu kufanya jambo fulani kwa namna nyepesi kabisa tofauti na wengine. Mfano kuongoza, kuimba, kuigiza, kushawishi, kuchekesha, kuandika na mengineyo mengi.
💥Muasisi na mfalme wa ucheshi Tanzania Fredy Chavala aliwahi kusema, "Furaha ya kweli maishani inapatikana pale mtu anapoamua kufanya jambo lile analolipenda zaidi, na upendo huo ndio husukuma kujua na kuweza zaidi".
💥Kila mtu ana kipaji na inawezekana mtu akawa na vipaji zaidi ya kimoja, lakini kuna kipaji kimoja kikuu ambacho ni msingi wa vipaji vingine vyote.
💥 Mfano, mwalimu na mwandishi Emmanuel G. Makwaya aliwahi kufundisha juu ya mcheza sinema Jack Chan. Jack Chan ana vipaji vingi sana kama uimbaji 🎼,uchekeshaji 🤣, ujasiriamali 👜💼 na vingine vingi lakini dunia inamtambua kama mcheza sinema🖥📹 au muigizaji.
💥Sasa kuna neno lingine linaloendana na kipaji linaitwa kipawa au karama. Ukiangalia kwenye kamusi ya kiswahili TUKI toleo la pili mwaka 2000 vyote vimeelezewa kuwa ni *zawadi*. Lakini kuliweka sawa hili karama au kipawa ni mafuta juu ya mtu yanayomtofautisha na mwingine katika kipaji.
💥 *Mithali 17 :8*Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.Ni ngumu sana kufanikiwa kama hujaweza kugundua zawadi iliyo ndani yako na kuanza kuifanyia kazi. Maana kugundua pekee haitoshi.
Haijalishi watu wanachukulia poa vipi kipaji chako, kama wewe unakithamini, unakifanyia kazi KUFANIKIWA ni lazima tu. 🔨
Leo tunaendelea na somo letu la *Kipaji*, tutaangalia *aina za vipaji* pamoja na *namna ya kugundua vipaji*.
Vipaji vimegawanyika katika makundi makuu matatu (3)
💥 Vipaji vinavyohusisha kichwa, mfano vipaji vya ugunduzi wa kisayansi, hesabu, kuongea, kuimba na vinginevyo.
💥Vipaji vinavyohusisha mikono, mfano vipaji vya michezo, kuchora, kupika, kuchonga, kuandika, kupamba na vinginevyo
💥Vipaji vinavyohusisha miguu, mfano kucheza mpira miguu, kucheza ngoma au nyimbo, nakadhalika.
➡Kumbuka vipaji vyote hivi kiini chake ni *akili au nia*. Huwezi kucheza mpira wa miguu au kuimba au kupika bila kutumia akili na vingine kadhalika.
NAMNA YA KUGUNDUA KIPAJI
Kuna namna mbalimbali za kugundua kipaji zikiwemo :-
(i) Kuangalia kitu ambacho ulikuwa unapenda sana kufanya zamani au ukiwa mtoto. Hii ni njia mojawapo ya kugundua kipaji chako na binafsi imenisaidia sana. Mtoto huwa anafanya vitu kutoka moyoni na anakuwa amevutiwa navyo kweli tofauti na mtu mzima ambaye anaweza fanya jambo sababu mwingine kafanya. Hivyo ukifanikiwa kugundua kitu au vitu ulikuwa unapenda sana kufanya ukiwa mtoto ni rahisi kujua kipaji chako.
(ii) Kuangalia kitu ambacho kwasasa unapenda sana kukifanya kwa muda mrefu bila kuchoka. Hii ni njia nyingine ya kugundua kipaji chako, kila mtu hapa duniani ana jambo ambalo anapenda kulifanya sana. Mtu anaweza kuwa tayari kutumia gharama yeyote ile na muda wake mwingi kulitimiza jambo hilo. Ukifanikiwa kulijua jambo hilo basi hapo ndipo kipaji chako kipo.
(iii) Kuangalia aina ya watu wanaokuvutia sana katika mambo mbalimbali wanayo fanya. Mfano ukiwa unavutiwa sana na viongozi na unapenda kufuatilia kazi zao, maandishi yao, na maisha yao kiujumla basi utakuwa na kipaji cha uongozi. Watu wanaokupa hamasa na motisha katika jamii wana nafasi kubwa ya kukufanya ujue kipaji chako pia.
(iv) Kuwa na bidii na shauku ya kusoma au kujifunza juu ya jambo fulani. Mfano, binafsi nilikuwa napenda sana kusoma juu ya ujasiriamali na hadithi za watu mbalimbali walio acha historia katika dunia kama Martin Luther King Jr, Mama Theresa na wengine wengi. Hapo ndipo nilianza kugundua kuwa nina kitu pia cha kipekee cha kuibadilisha dunia.
(v) Kujihusisha na mambo mbalimbali. Hii inasaidia kuweza kugundua ni mambo gani unayafurahia sana na yapi huyafurahii. Hivyo basi katika mambo unayafurahia sana ndipo huko kipaji chako kipo.
Pia leo tunaenda kumalizia somo letu kwa kuangalia namna ya kukiishi kipaji /vipaji vyako.
JINSI YA KUKIISHI KIPAJI CHAKO
(i) Kufanya mazoezi mara kwa mara. Hii ni njia moja wapo ya kukiishi kipaji chako. Kipaji cha aina yeyote ile kinahitaji mazoezi ya hali ya juu ili kuweza kuwa bora zaidi kila kukicha. Tunaona waimbaji wakifanya mazoezi ya sauti, wakipanga aina za vyakula vya kula na mengineyo. Hivyo hata waandishi, viongozi, wanenaji, wachezaji, walimu na wengine wanapaswa kufanya jambo fulani kila siku ili kuongeza thamani katika vipaji vyao.
(ii) Kuwa karibu na watu waliofanikiwa katika kipaji hicho na kukubali kufundishika. Katika kila fani kuna watu wanafanya vizuri sana, ni vema kujitahidi kuwa nao karibu na kufuata mafundisho yao. Hii itakupa nguvu zaidi ya kupambana na kufika mbali zaidi.
(iii) Kujitofautisha na kuwa mbunifu. Ili kipaji chako kiweze kuongezeka ladha ni lazima uweze Kujitofautisha na watu wengine wenye kipaji kama chako. Unapaswa kuwa mbunifu kila siku kwani kila mtu ana kitu cha pekee ambacho hakuna mwingine yeyote mwenye nacho duniani.
(iv) Kusoma vitabu mbalimbali vinavyogusa eneo la kipaji chako. Unapaswa kuwa na vitabu maalum kwajili ya kukuza kipaji chako. Hivi vinasaidia sana katika kugundua mbinu mpya na mambo mengine mengi katika kipaji chako.
(v) Kujitambua thamani yako na kutunza tabia njema, utu na heshima. Hiki ni kitu kingine muhimu cha kuzingatia katika kukiishi kipaji chako. Kuna watu pengine wangekuwa mbali sana katika muziki, uandishi, uigizaji nakadhalika lakini tabia zao za mbaya na kutojitambua kumewarudisha chini.
Severina: 💥 Niwaache na mistari hiyo mkitafakari. Pia nakaribisha maswali sasa.
*Mithali 22:29 Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.*
*1 Petro 4 :10 Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.*
Shemeji Meleyeki:
Katika kuliishi Kusudi la Kuumbwa kwako
Tumeona yafuatayo,
1. Umuhimu wa kulifahamu Kusudi la Kuumbwa kwako,
2. Namna ya kufahamu
Hapa tulijifunza umehimu wa Kumuuliza aliyekuumba na pia kutazama utofauti wako. (Uniqueness)
Katika eneo hili tuliangalia kuwa

2. Uwezo (ability)✅✅
Hapa ndipo Somo la kipaji lilipotokea.
3. Uhitaji (Demand)
Sasa kwenye Demand
UHITAJI. (DEMAND )
Uhitaji ulipo mahali wewe ulipo unaweza kuwa sababu ya kuwepo kwako hapo. Hapa ni kuanzia kwenye familia, mtaa, kijiji, nchi na hata dunia. Yale mapungufu yaliyopo yanahitaji mtu wa kuyatatua. Jiulize maswali haya yafuatayo:
Unapenda jamii inayo kuzunguka iweje?
Inawezekana kuna aina fulani ya maisha, ama aina fulani ya huduma au mfumo fulani wa maisha au aina fulani ya tabia unapenda jamii au mahali ulipo iwe nayo. Na unaona kabisa huu ni uhitaji na upo ndani ya uwezo wako. Wengine wanabaki kulalamika au kuvumilia tu. Usisite kufanya hivyo maana inawezekana kabisa hakuna mwingine atakayefanya isipo kuwa wewe.
Nini ambacho hakipo ila ungependa kiwepo au kifanyike
Inawezekana unaona kuna jambo linahitajika kufanyika mahali ulipo na hakuna anayelifanya. Inawezekana hakuna nayeona huo uhitaji, au hata kama wapo hakuna mwenye utayari ama uwezo ama shauku ya kulifanya. Ukiona unao utayari na uwezo basi ujue wewe ndiye mtu wa kulifanya na ndilo kusudi ya kuwepo kwako hapo.
*Nabii Habakuki aliona tatizo na akawa analalamika*
Habakuki 1:2-5. Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.[3]Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.[4]Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.[5]Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.
*Hata hivi Hii ni sehemu Ndogo ya malalamiko yake*
Angalia Alichoambiwa na Bwana
Habakuki 2:1-3. Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.[2]BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao,ili aisomaye apate kuisoma kama maji.[3]Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
*Habakuki aliyekuwa analalamika juu ya waovu na uovu* Akaona *Hali ikiwa imebadilika*
Baada ya Mungu kubadilisha mtazamo wake
Habakuki 3 yote, Kwenye kutaka maisha ya watu yawe ya Aina fulani au mabadaliko ya Aina fulani una develop kitu kinachoitwa *Maono/Vision/Njozi*
Leo Mwalimu *Gladpeace Bakary ataendelea na kipengele cha maono na uhusiano wake na Kusudi*
📓Sasa wanafunzi wangu wazuri, Usiku wa leo nitaanza kwa kuwaachia kazi ya kufanya
Naomba kila mmoja afanye maswali yafuatayo /ayajibu na kisha anitumie majibu inbox kwangu au unaweza kunitumia majibu kwenye email yangua ambayo ni
*gladpeace1@gmail.com*
*MASWALI KUHUSU MAONO*
Maono ni nini?
Faida za maono ni zipi?.
Namna gani unaweza kuyaandika maono yako.?
Namna gani unaweza kuyatimiza maono yako????
*NAWATAKIA UTEKELEZAJI MWEMA*🎁Wa kwanza kutuma majibu atapata zawadi
Kumbuka tunajifunza juu ya *Kulitambua na kuliishi Kusudi la Kuumbwa kwako*
Leo tutajifunza:-
📌Maono ni nini?
📌Kwa nini niwe na maono?
📌Na faida za maono
*🔜MAONO*
*MAONO NI NINI?*
👉Udhihirisho au kufunuliwa kwa kusudi la mtu ndani ya moyo wake kwa mfumo wa picha ambayo inaonyesha maisha yake ya baadae.
👉Ni Picha aliyonayo mtu kuhusiana na maisha yake ya baadae.
👉Ni ile picha ambayo unaiona kwenye akili yako na kuanza kuifikiria na kuitendea kazi.
📝Maono ni kwa ajili ya watu wengi na si mtu mmoja.
Maono hubeba majibu na utatuzi wa matatizo ya watu wengi.
📖Pale penye maono watu hujizuia, huwa na nidhamu, huwa na mwongozo katika maisha.
*“Pasipo maono watu huacha kujizuiza….” Mithali 29:18*
👌Maono ni kitu cha muhimu sana.
👌Maono hulinda watu. Maono huongoza watu.
💓Kama unajipenda, hakikisha unakuwa na maono, utaishi kwa mpangilio na utatimiza kusudi lako hapa duniani.
❌Usidharau maono yako, yafanyie kazi.
✅ Upatapo picha halisi ya kusudi la maisha yako ifanyie kazi
*✈“ANZA SAFARI, IFATE NDOTO, PIGA MBIO 🏃♂TIMIZA NDOTO YAKO”.*
❌Hatuko hapa duniani milele na muda ⏰tulio nao ni mchache lakini inawezekana kutimiza maono yetu kama tu tupo tayari kulipa gharama zake.
👉 Mara nyingi maono hututoa katika sehemu au mahala tulipo pazoea na pengine kupapenda na kutupeleka mahala ambapo hatujapenda😪, hatupajui na hatujapazoea.
👌Ni watu wachache wanaokuwa tayari kuondoka 🚶♂🚶♀na kulipa gharama.
🔎Maono huona mwisho kabla ya mwanzo.
*Maono huwa makubwa :*
Ni picha ambayo hukuchangamotisha na kukufanya ufikirie na kutafakari kwa makini namna ya kuitimiza.
Maono haya hukuhitaji kuwekeza sala na jitihada zako kwa Mungu🔥 apate kukusaidia na kukuwezesha kuyatimiza.
*MAONO NA NDOTO:*
Vyote humaanisha kitu kimoja.
MAONO SIYO SAWA NA CHEO AU WADHIFA ALIO NAO MTU.
Cheo chako au elimu yako au nafasi yako mahali fulani ni njia inayokuwezesha wewe uweze kutimiza maono yako.
Mfano kuwa Daktari siyo maono lakini ni nini ambacho utafanya kupitia udaktari wako. Maono ndiyo yanayokupa cheo au nafasi.
*⁉⁉KWA NINI NIWE NA MAONO*
Kwa sababu, kila mtu hapa duniani ana *KUSUDI* na kazi ya kutimiza kabla hajaondoka hapa duniani. Ili kusudi hilo liweze kutimia unahitaji *maono.*
*FAIDA ZA MAONO*
Maono:-Yanakupa nidhamu ya matumizi ya muda.
Watu wengi wanapoteza muda kwa sababu hawajui cha kufanya, hawajui wanataka waweje, hawajui wanapotaka kwenda wala hawana maono ya wanapotaka kwenda.
🖊Yanakuwezesha kutengeneza muda wa kufanya mambo ya msingi kwa ajili ya maisha yako ya baadae.
🙌Yanabadilisha namna unavyosali na kuomba pale usalipo.
💪Maono hukupa nguvu ya imani yako.
⏭Yanakupa mwongozo wa maisha yako.
🤔Yanabadilisha mfumo wako wa kufikiri na kutenda.
👦Hukuchagulia marafiki na watu wa kukaa nao.
📖Hukuchagulia vitu vya kusoma na kusikiliza. (vitabu, majarida, magazeti, habari, video, miziki n.k)
👌Hukufanya ufikiri na kutafakari kwa kina kabla ya kuongea, kunena na kutenda.
❌Hukufanya uache mambo mengi yasiyo ya msingi na kuchagua na kufuata machache ambayo ni yenye manufaa kwako.
💯Hukuwezesha kutimiza kusudi lako hapa duniani.
😊Hukupa furaha na amani kila iitwayo leo.
🔰Hukufanya ugundue talanta na uwezo ulionao ndani yako wa kufanya mambo makuu na makubwa.
🙅♀🙅♂Hukufanya uwe msaada kwa watu wenye shida mbalimbali.
😘Maono si kwa ajili yako mwenyewe ni kwa ajili ya watu wote.
Natumai pia umeandaa mpango kazi wako wa mwezi na to do lists zako (ambazo wakati mwingine ndo huwa prayer points zako😊),
Yote hayo yakiwa na lengo la kukupeleka na kukufikisha kwenye *maono* *yako*😊
Nakuombea ufanikiwe katika yale yote ambayo umeyapanga kuyafanya mwezi huu
Ili ifikapo mwezi mwingine, uwe na kitu cha kujifanyia tathmini kwa kipindi cha mwezi kilichopita.Yawezekana pia huwa huna utaratibu wa kuandika mambo ya kufanya, na huwa unafanya tu pale inapotokea,
Embu leo amua kufanya tofauti, chukua kalamu na daftari kisha andika mambo ya kufanya May, na uyafatilie na kufanya kila siku na hatimaye utajikuta umeweza...
Hujachelewa, anzia hapo hapo ulipo,Baada ya salam za utangulizi,Sasa karibu darasani tuendeleze somo letu
Leo tutajifunza kipengele cha kuandika maono
*NAMNA YA KUANDIKA MAONO YAKO*
Kabla hatujaandika maono yetu hebu tujifunze kitu kutoka kwa Habakuki.
*“……..Bwana akanijibu, akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.* *Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuifikilia mwisho wake, wala haitasema uongo ijapokawia;**ingojee kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia”*
*Habakuki 2: 2-3*Kutoka kwenye huo mstari tunajifunza mambo *sita* yafuatayo:-
Ndoto au maono ni lazima yaandikwe. (….iandike njozi hii…)
-Usikariri❌!
-Andika chini kwenye karatasi.
Ukishaiandika uielezee (……iwe wazi sana katika vibao…..)
Maono hukufanya uyafanyie kazi.
📌Yanatakiwa yakuhamasishe, yakutie moyo na kukuchangamotisha wewe na wengine pia.
Maono yana kikomo.
📌Hautaishi milele, hivyo basi ni vizuri maono yako yakawa na kikomo.
Maono lazima yawe na uhalisia.
📌Usiwe na maono ya kujifurahisha tu ambayo hayana hata uhalisia, maono ya kujenga ghorofa angani🤔🙆♂.
Maono yanahitaji uvumilivu.
📌Usikate tamaa mambo yanapokuwa ndivyo sivyo, ugumu wa jambo haujakuja kukaa, umekuja kupita, ni hali ngumu ya muda tu, lakini maamuzi ufanyayo ndiyo ambayo hayabadiliki milele.
*🖊📖KUANDIKA MAONO📝*
*(Ni vizuri zaidi kama ukiwa na kalamu🖊 na karatasi📖 kwa ajili ya hili zoezi)*
🦋Chagua kipaji (vipaji) kati ya ulivyonavyo ambacho utakitumia kwa makini na kukipa muda mwingi kukikuza na bila kusahau ni kipaji ambacho unakipenda💓.
Kwa kutumia kipaji ulichonacho utapata kusudi nalo kusudi litazaa ndoto au maono.
*Yaani*
*KIPAJI➡KUSUDI➡ MAONO*
🦋Tambua ni nini haswa unataka kufanya na maisha yako na uandike
⁉Ni kitu gani ambacho kama leo hii ungekuwa na siku saba za kuishi ungekifanya kwa juhudi zako zote.
⁉Ni kitu gani unataka dunia ikukumbuke nacho?
Jaribu kufunga 🙈macho👀 kwa dakika kumi⏰ na kujiona ukitimiza ndoto au maono yako.
✔Jaribu kuona mwisho wa kile ambacho kweli roho yako inataka ukamilishe hata ukiwa leo unakata roho utakuwa tayari kufumba macho kwa furaha na tabasamu.
🦋Tambua pia ni jinsi gani unaweza kuishi maisha ambayo yatakusaidia uweze kutimiza maono yako.
📌Ili maono yako yatimie huna budi kuishi maisha ambayo yataipalilia ndoto au maono yako ili ipate kukua.
Ndoto au maono ni kama mbegu, inahitaji mbolea, maji, hewa na mwanga wa jua ili ikue.
Pale inapokosa vitu hivi muhimu haina budi kufa.Kwenye maisha yetu tuna tabia ambazo ni za kuacha😬, kuna marafiki wa kuwaacha🙅♀🙅♂, kuna mahali itabidi tuondoke🏃♀🏃♂ ili tuweze kutimiza ndoto zetu.
Orodhesha mambo ya kuacha ❌naya kuambatana nayo✅.
*Anza kuyafanyia kazi yale ya kuambatana nayo huku ukiikimbiza 🏃♂🏃♀ndoto yako.*
*🗣 Bwana akamwambia Abraham,*
“Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayo kuonyesha; nawe nitakufanya wewe kuwa Taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaanie nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”*Kut 12:1-3*
Na sasa karibu darasani tuendelee na somo letu la *maono*
Siku ya leo tutajifunza juu ya
🖊Namna ya kuyatimiza Maono
🖊Mambo muhimu kuyafahamu na kuyafanya kuhusiana na maono
🖊Hitimisho
MAONO yako unaya weka katika mtindo uitwao Malengo
Kisha Malengo hayo unayavunja katika vipande vidogo vidogo (Mwaka, miezi, wiki, siku, masaa)
Halafu unaweka bidii na jitihada ili kukamilisha na kufanikisha malengo yako.
*Mfano mrahisi*
Mtu x ana *maono* ya kuja kuwa mchambuzi wa Biblia,kuifundisha na kuielezea kila kitu kilichoandikwa humo.
*LENGO / MALENGO*
- Kuisoma na kujifunza Biblia yote katika lugha zaidi ya moja,
Mfano Kiingereza na Kiswahili.
*MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO / MALENGO*
- Kila mwezi kuhakikisha amesoma vitabu "x" kwa kila Bibllia
- Kila wiki kuhakikisha ametafsiri sura "x" kwa kila Biblia
- Kila siku kuhakikisha amesoma sura "x" kwa kila Biblia na kuandika alichojifunza
(Kwa kila siku ametenga masaa "x" ya kusoma sura za Biblia)
*JITIHADA*
- Kuhakikisha hakuna kulala hata iweje mpaka awe amesoma na kupitia sura kadhaa za kila Biblia
*📌Mambo muhimu ya kuwa nayo ili uweze kutimiza maono yako.📌*
1. Jambo la kwanza kabisa la kufanya ili kutimiza maono ni kuwa na *MAONO*.
2. Maono hayo unayavunjavunja katika visehemu vidogo vidogo viitwavyo *(MALENGO)* katika mwaka, miezi, wiki na siku.
🤔Yaani kila siku unafanya angalau jambo moja ambalo litakusaidia kufikia *lengo kuu.*
Kuna usemi unasema,
*“Ukitaka kummaliza tembo 🐘mzima, mle kidogo kidogo”*
🙃Hivi vinakuwa kama vituo ambavyo hukupatia muda na wakati wa kujitathmini.
✍Malengo yanaweza yakawa ya muda mfupi au mrefu.
3.Andaa mikakati na mipango ambayo itakusaidia kufikia maono yako.
🖊Ni vitu gani ambavyo ukivifanya hakika utafikia lengo kuu.
4.Fanyia kazi mikakati na mipango yako.
Kuwa mwaminifu, timiza mipango yako na malengo yako.
*‼MAMBO YA KUFANYA;‼*
🔰Mkabidhi *Mungu* maono yako na uyaombee.
*“Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri Yeye, naye atanyoosha mapito yako.”*
*Mith 3:5-6*
🔰Uwe na *Imani* kwamba unaweza kutimiza maono yako hata kama ni makubwa kiasi gani.
🤷♂Jinsi ulivyo ni *matokeo* ya vile unavyofikiri na jinsi unavofikiri ndivyo ulivyo.
🖊Mawazo yetu yana nguvu sana.
Kama unafikiri unaweza✅ utaweza kweli na kama unafikiria kushindwa❌ utashindwa kweli.
*“FIKIRIA KUSHINDA ILI UWE MSHINDI”*
🔰Fanya jambo la kwanza la kwanza.
🔰Jitie moyo mwenyewe.
✍Jifunze kuwa na tabia ya kujitia moyo mwenyewe.
Hii ni ishara ya kujipenda😘.
🔰Jitie moyo mwenyewe usisubiri mtu, mama au rafiki wa kuja kukufariji.
✍Wewe ndo faraja yako mwenyewe, jifariji, jitie nguvu, simama, endelea na safari.
🔰Jinenee🗣 maneno mazuri.
Kila ukiamka asubuhi, jiangalie kwenye kioo na ujiambie na kujinenea maneno ya ushindi.
*Jiambie,*
👌Mimi ni mzuri.
👌Mimi ninaweza kuyatimiza maono haya.
👌Nina akili na busara.
👌💪Mimi ni mshindi…..n.k.
🔰Usikate tamaa.
Katika safari yako ya kutimiza ndoto yako, utakutana na majaribu mengi tena ya kukatisha tamaa na wakati mwingine hata utataka kuishia njiani.
*❌HAPANA, USIISHIE NJIANI, JIPE MOYO❤.*
🔰Fanya jambo moja kila siku ambalo litakusaidia kulifikia lengo lako kidogo kidogo.
🔰Kabla ya kulala 🛏fanya tathmini ya mambo uliyofanya kwa siku hiyo.
⌛Hii itakusaidia kufahamu ni wapi panahitajika kuongeza juhudi ili kuifikia ndoto.
🔰Andika ratiba ya siku inayofuata kabla hujalala.
🔰Kuwa mwaminifu, timiza wajibu wako.
🗝Kuwa mchapakazi. Mafanikio hayatokani na kusali na kukaa tu. *HAPANA!* Ni lazima ufanye kazi ili ufanikiwe.
😉Kuna wakati utakuwa hujisikii kabisa kufanya chochote, usiache kufanya kazi, jiitie moyo fanya kazi hata kama ni polepole.
*“Huwezi kupanda mlima* *na mikono mfukoni*,*na ukitaka juisi kutoka kwenye chungwa sharti ulikamue 👌.”*
🔰Fanya tafakari ya mwezi.
😷Tafuta mahali tulivu palipo tulia na ufanye tathmini na tafakari ya mwezi mzima.
✍Fanya marejeo ujue kama umeyafikia malengo yako ya mwezi.
🖊Angalia mapungufu na namna ya kuyatatua.
✍Angalia makosa na namna ya kuyarekebisha.
*📌HITIMISHO📌*
*Maono:*
Picha aliyonayo mtu moyoni mwake kuhusiana na maisha yake ya baadae.
MAONO ni kama kuwa na picha akilini mwako, KUYAISHI MAONO ni kama kuichora hiyo picha.Maono ni kama kujenga jengo akilini mwako (Maisha yako ya mbeleni).Wewe ndiyo fundi mwashi.
*Mfano waFundi ujenzi (Mwashi)*
▶Kusudi la jengo:
Tambua kusudi la jengo.
▶Unaona nini : Ni picha gani unayo akilini mwako.Iweka katika mchoro wa kwanza.
▶Mchoro wa mwisho.
*JENGO LINAKAMILIKA KABLA HALIJAANZWA!*
*“ It’s your mental picture that determine your actual future”**Bishop David O. Oyedepo*
▶Maono huamuru:
Uchaguzi wa watu wa kukaa na kuambatana nao.
Uchaguzi wa taarifa, vitabu, habari, shule, magazeti, majarida, vipindi na televisheni ya kuangalia.
Uchaguzi wa watu watakao kuelekeza na kukuvutia.
▶Maono huongoza:
👌Tabia zako.
👌Imani yako.
👌Nidhamu yako.
👌Matumizi ya muda wako.
👌Mawasiliano au lugha yako.
✍Watu wengi huwa hawaandiki maono yao.
*“Siri kubwa ya mafanikio ni hii: Fikiria kwenye karatasi”*(🗂THINK ON PAPER🤔)*Brian Tracy*
▶Maono hukupa upekee na kukutofautisha popote uendapo.
▶Wabeba maono ni watu ambao hufikiria kwa kina na kutafakari juu maisha yao kila siku.
🤔Hufikiri namna ya kuyaboresha na kuifanya leo kuwa njema na nzuri zaidi ya jana.
Kama unataka kuacha alama nzuri ya kukumbukwa hapa duniani lazima ujifunze kufikiria.
*“JIFUNZE KUFIKIRIA KWA MAKINI”*
▶Watu wengi huwa hawapendi kuchukua muda kufikiri tena hasa pale inapokuwa kufikiri kuhusu maisha yao ya baadae.
HEBU ONA HII
*“Asilimia tano ya watu hufikiria,* *asilimia 10% hufikiri* *wanafikiria;**asilimia 85% ya waliobaki ni bora wafe kuliko wafikirie”*Thomas Edison
*‼‼(jiulize uko wapi?‼‼)*
▶Huwezi kuwa na maono kama haufikirii kuhusu maisha yako ya baadaye.
▶Kama unataka kuacha alama hapa duniani, amua leo kubeba na kutembea katika *maono* makubwa yatakayo kuchangamotisha na kukufanya uyafanyie kazi kwa bidii ili uyatimize.
▶Kama hauna maono hutafanikisha chochote.
▶Usipokuwa na maono utakuwa mvivu tu.
▶Maono huongoza hatua zako.
Hukufanya uache kufanya kila kitu na kuiweka akili yako katika jambo moja ambalo uko vizuri sana.
❌Bila maono watu wanapotea kwa kufanya kile ambacho hakikukusudiwa wao kufanya.
*▶MWISHO🔚*
*😊Somo langu nimehitimishia hapo😊*
⏰🙏Asante sana kwa muda wako na kufuatilia somo tangu mwanzo, asante pia kwa ushirikiano wako
Naamini *HAUJABAKI KAMAULIVYOKUWA*
Nakuombea Bwaana akuwezeshe kuishi *maono* yako, Amen
*Shukrani kwa**🙏Shemeji Melayeki*,*🙏Uongozi mzima wa RYM*Na*🙏Wote ambao mpo mahali hapa*,*💓Love you all, always💓*
*MWISHO*
*➕NYONGEZA😊*
Kuna *vitabu* vingi waweza soma ....Ila kama hujapata vitabu hivi, tafadhali vitafute, naamini utapata vitu humo vya kukusaidia juu ya mafundisho haya. Yawezekana pia unavyo na ulishawahi kuvisoma lakini ulivisoma tu *ilimradi*, sasa embu *rudia* tena kuvisoma
*Vitabu hivyo ni*
1⃣ Nguzo za sikuAmeandika *Shemeji Melayeki*
2⃣Principles of growth "Everybody wants to be:no body wants to grow"🖊Ameandika *Shemeji Melayeki*
3⃣The power of Vision (Nguvu ya *maono* ambalo lilikuwa somo letu)Ameandika *Shemeji Melayeki*
4⃣ To Be Is To Do (Kuwa ni Kufanya)Ameandika Mwalimu*Emmanuel Makwaya*Wapo waandishi wengine pia,
Tafadhali watafute na usome vitabu vyao (Vile ambavyo vita add value kwenye maono na malengo yako)*Kama*
📌Robin Sharma
📌Brian Tracy
📌Dr. Myles Munroe
📌Rick Warren
📌Todd Henry.....Na wengine*Ingia kwenye website hii*,*Na huko utapata kila aina ya kitabu utakachokihitaji for free*,(Kama *maono* yako ni kuwa ,Mwandishi, Muhubiri,Mjasiriamali,Mwalimu…,Muimbaji,Mchoraji,Mzungumzaji / au wale wa Public Speaking,Muhamasishaji,Mwanasayansi,Daktari.. Na mengineyo vipo vitabu humo kwa kila kipengele).Website hiyo ni www.pdfdrive.com
*❤LOVE YOU ALL, ALWAYS, MFANIKIWE❤*
Shalom FAMILY.... Habari za wakati huu
Naamini uko vizuri na unapambana kuyafikia *maono* yako kupitia *malengo* uliyojiwekea
Kama ambavyo tulijifunza kwenye somo lililopita. Karibu darasani tumalizie somo letuLeo tutajifunza somo la *mwisho,* linalohusu.
*ORODHA YA MAMBO YA KUFANYA*AU KWA KIZUNGU*TO DO LIST*
*ORODHA YA MAMBO YA KUFANYA*
*(TO DO LIST)*
▶Mafanikio ni fungu alilowekewa kila mtu ila wengine wanasinzia na wengine wamelala kabisa ,hawajachukua mafungu yao kwa kuwa hawajitambui ,hawajui watokako,walipo wala waendako badala yake mafungu yao yamechukuliwa na watu wengine wasiosinzia wala kulala na ndiyo maana tuna idadi kubwa ya watu tegemezi hususani barani Afrika.
▶Mafanikio hutokeza penye maono thabiti na malengo binafsi yanayoeleweka na kutekelezeka.Lakini ni lazima mtu ajitambue kwanza ili aweze kupanga maono na malengo sahihi.Ni hatari kubwa kuweka jambo katika orodha ya mambo ya kufanya na ukalifanya kwa bidii ukidhani umepatia kumbe umepatia kukosea.
Maono na malengo ni dira kuelekea kilele cha mafanikio.Mkufunzi, mzungumzaji na mwandishi chipukizi wa vitabu nchini Tanzania *Shemeji Melayeki* katika moja ya vitabu vyake alisema …
*“ni bora kuwa chini ya ngazi inayoelekea kileleni , kuliko kuwa juu ya ngazi isiyo kupeleka kokote”.*Hivyo ili kufanikiwa katika malengo uliyojiwekea lazima uwe na *orodha ya mambo sahihi ya kufanya* yatakayo kuongoza kufikia kilele cha mafanikio.
📝Orodha ya mambo ya kufanya ni mpangilio na mchanganuo wa majukumu sahihi ya kufanya kulingana ulazima na umuhimu wake .Mpangilio huu wa majukumu lazima uandikwe kwenye *karatasi* ili kurahisisha kumbukumbuku katika utekelezaji wake.
Orodha hii inaweza kuwa kwaajili ya mtu binafsi, kikundi cha watu, taasisi au shirika.
Orodha ya mambo ya kufanya inaweza kuandaliwa katika mfumo wa kawaida (yaani kuandika katika kikaratasi ), kalenda au excel. Orodha ya mambo ya kufanya ni lazima isadifu kusudi, maono, malengo na ndoto ya mtu husika.
Huwezi kuiga au kuitendea kazi orodha ya mambo ya kufanya ya mtu mwingine ukitegemea kufanikiwa kwa kuwa haitaendana na shughuli zako halisi unazopaswa kufanya na hivyo katu huwezi kufikia malengo na ndoto yako.
Utashia tu kuona wengine wakifanikiwa na huku wewe ukibaki umetoa macho kama *fundi saa anayetafuta nati za saa gizani.*
*🖊NAMNA YA KUANDAA ORODHA YA MAMBO YA KUFANYA*✍
*Unapoandaa orodha ya mambo ya kufanya hakikisha unafuata hatua zifuatazo;*
📍Lazima uwe na lengo/malengo makuu ya maisha uliyopanga kuyafikia yanayolenga ndoto yako.Kama hauna malengo, maono wala ndoto chukua hatua uandae haraka tena kwa kuyaandika vizuri kwa kuwa tayari umekosa sifa na vigezo vya kuendelea na zoezi hili tangu ukiwa katika hatua ya kwanza.
📍Yavunje vunje malengo yako makuu ya maisha katika vipindi vifupi, inaweza kuwa miaka 10, 5, 2, 1, miezi, wiki hatimaye siku.Hii itarahisisha utekelezaji wake na katika kufanya tathimini.
📍Baada ya kuvunja vunja malengo yako katika sehemu ndogondogo ni vema ukaandaa orodha ya mambo ya kufanya kwa wiki ili ikuongoze kuandaa mambo ya kufanya katika siku.
📍Yapange mambo yako ya kufanya katika orodha kwa kuzingatia umuhimu na ulazima wake.Anza na lile jambo la muhimu na la lazima kuliko yote, kisha linalofuata kwa umuhimu na ulazima, fanya hivyo mpaka lile jambo la mwisho kulingana na idadi ya mambo katika orodha unayoiandaa.
📍Kila jambo katika orodha ya mambo ya kufanya liwekee ukomo wa muda katika utekelezaji wake.Hii itakuongezea hamasa na kuongeza kasi ya kuwajibika pale unapoona unalega lega.
📍Hakikisha kila ulichoandika katika orodha ya mambo ya kufanya kinatekelezeka.
Usiandike tu ili uonekane upo miongoni mwa walioandika hali huwezi kutekeleza hata jambo moja kati ya yale uliyoandika.
📍Jipe muda wa kufanya tathimini kila baada ya kumaliza hatua moja katika kufanya zoezi hili.Hii itaongeza ubora na ufanisi kuelekea utekelezaji wa orodha ya mambo yako ya kufanya uliyojipangia.
*Nidhamu ya kufuata ratiba yako uliyojiwekea kulingana na orodha ya mambo ya kufanya *
✔Ni lazima uwe na nidhamu ya kufuata ratiba ya orodha ya mambo ya kufanya uliyojiwekea kwa kufanya yafuatayo;
❌Jikane kufanya mambo yasiyokuhusu, fanya yale yaliyo katika ratiba yako tu hata kama umeona yanavutia kiasi gani
✅Anza na jambo linalopaswa kuanza katika utekelezaji, fuata mpangilio wako kwa jinsi ulivyoyapanga hata kama unahisi jambo hilo ni gumu.
Hii itakuepusha na hali ya kuahirisha mambo kwa kukwepa ugumu na kusema utafanya baadaye au kesho kisha unasahau kufanya na pia itasaidia kupunguza mlundikano wa majukumu.
🙉Jifunze kusema hapana kwa vishawishi vinavyojitokeza na kupelekea kuvuruga ratiba yako.✍Uwe mtendaji zaidi kuliko kuongea sana kwa kuwa maneno matupu hayatakusaidia kufikia malengo yako kama wahenga wasemavyo, maneno matupu hayavunji mfupa.”
❌Usijihurumie, wajibika, jitume ili kufikia lengo la siku hata kama unajiskia kuchoka.
🙈Ona aibu kulala kabla hujamaliza kutimiza majukumu yako ya leo, kwani kesho yako inatokana na nini umefanya leo.
❌Usibweteke pale unapogundua kuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hata kuvuka lengo ulilojikea katika orodha ya mambo ya kufanya. Tazama mbele, usilegee, ongeza kasi ya utendaji.
Ikiwezekana ongeza idadi ya majukumu ya kufanya katika orodha yako ya mambo ya kufanya pale unapoona unafanikiwa sana na siyo kupunguza majukumu, ratiba ya leo iwe na mambo makubwa zaidi ya yale ya jana
❌Usikate tamaa na kuamua kuacha pale unapokutana na changamoto na kuhisi kama hautafanikiwa kutekeleza majukumu yaliyopo katika orodha ya mambo ya kufanya na kufikia malengo yako.
💪Thubutu, Jitie nguvu, jiambie ninaweza, upige moyo konde.
Usiogope kuchekwa kwasababu hao wanaokucheka mambo yao yamewashinda.
Amua na fanya unachopaswa kufanya kwani hakuna mteremko katika safari ya mafanikio.
🤔Jifanyie tathimini ya utekelezaji wa majukumu uliojiwekea katika orodha ya mambo ya kufanya.
Inashauriwa zoezi hili lifanyike kila siku baada ya kumaliza majukumu yako ya siku yaani kabla ya kulala, kila mwisho wa wiki, kila mwisho wa mwaka na zaidi ya hapo kwa wale wenye malengo ya muda mrefu.
✍Boresha orodha yako ya mambo ya kufanya kwa kadri na kila inapohitajika kufanya hivyo, angalau mara moja kila mwezi.
Hapo mwisho nitakutumia mfano wa plain template ya kuandalia orodha yako ya mambo ya kufanya ingawa *sio lazima ifanane hivyo, waweza design ya kwako*
🙏🙏Asanteni kwa muda wenu, usikivu wenu na ufuatiliaji wenu mzuri wa masomo tuliyotoa
🤷♂Kwa yeyote mwenye kuhitaji msaada zaidi au ufafanuzi zaidi kwa somo hili au somo lilopita, karibu, nitakusaidia
*Mbarikiwe, nawapenda😘**👉Gladpeace Bakari👈*
*MWISHO*
Shemeji Meleyeki: Shalom Rafiki wa Yesu Ministries,
Ahsanteni kwa nafasi mliotupa kuwasilisha somo la *Kulitambua Kusudi la Kuumbwa kwako*
Ahsante kwa uongozi, ahsanteni kwa wote mliokuwa mnafuatilia pamoja na walimu wote nilioambatana nao
Noel Pallangyo,
Severina Gabriel,
Gladpeace Bakary,
Na Destea Kagine.
Ahsanteni sana!
Kama kutakuwa na Maswali Mengineyo,Karibuni!
Mama Fortune: Shalom Apostle!
Napenda kuchukua nafasi hii kwa namna ya kipekee kumshukuru Mungu kwa ajili ya kibali.
Hakika tunamtukuza Mungu kwa ajili yako pamoja na team nzima ya *Global Family Gathering*.
Kwa namna ya kipekee tunapenda ufikishe salamu zetu kwa Mama Apostle(Neema Shemeji) pamoja na King David kwa kukubali utumike madhabahu hii.
Walimu wetu tunasema Asante sana kwa muda,chakula na zaidi upendo mlioonyesha kwetu.Hakika tulitamani tuendelee kujifunza tena na tena.Lakini hatuna budi kuanza kuyatendea kazi yale yote mliyotufundisha.
Mungu aendelee kuwatumia kwa utukufu wake,toka Utukufu hadi Utukufu.Mbarikiwe mno mno.

Comments
Post a Comment