NGUVU YA UDHAIFU
Huduma hii inaitwa Time Investing Program ambayo kifupi
chake ni T. I. P, na hili ni darasa la pili kwa njia ya whatsapp kufanyika.
Asili ya hii huduma.
Kwasababu Mwenendo wa dunia unaratibiwa kimuda, hivyo
basi uwepo wa hii huduma ni kusaidiana
kuweza kujua na kuwekeza kwenye muda wetu wa kila siku.
Sasa basi kwasababu pia mtu anayewekeza kwenye huu muda
ameumbwa na Mungu na tunaona mambo mbalimbali yamekuwa hayafanyiki kwa
kisingizio cha uwepo wa Udhaifu fulani, Neema ya Mungu ikatujia kwa ajili ya
somo hili. Na hakika utajifunza vitu vingi sana kutoka kwa walimu
walioandaliwa.
Napenda kukukaribisha sana.
By Mwl. Hadson Ngata
Walimu wa darasa hili ni
Mwl. Hadson Ngata na Bro. Jr. Dugilo.
NGUVU YA UDHAIFU.
Ndo somo kuu katika Darasa letu hili
Sasa tuanze hivi
Hivi umewai kufikiria kwa
habari ya vita kati ya Daudi na Goliathi, ngoja nikutazamishe hivi kwanini
Daudi alimlenga Goliathi kwenye paji la uso? Je unadhani ndipo mahali penye
udhaifu wa Goliathi? Mana si jambo rahisi eti shujaa kupigwa jiwe moja tu
kwenye paji la uso na kufa hapo hapo? Lakini pia sio rahisi mpaka umpige kwenye
paji la uso ni uzembe mkubwa sana. Lakini mimi nataka nikutazamishe nini
kilitokea kwa uchache, Daudi alisema lugha hii ambayo ndio ilibadilisha
muelekeo wa vita alisema “Mimi nakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu
wa Israeli uliowatukana.” 1 Samweli 17:45 lugha hii si lugha ya kawaida
tunaiita lugha ya uchonganishi kati ya Mungu wa Daudi na miungu ya Goliathi
hivyo baada ya kusema hivyo Daudi aliipisha ile vita Mungu apigane yeye
mwenyewe na kama Daudi angeshindwa basi Mungu angeaibika sana hivyo Mungu
ikabidi aingie kazini kupigana na miungu ya Goliathi, kwa mantiki hiyo sisi
tunaona lile jiwe ni dogo lakini uhakika nilionao ni huu lile jiwe kwenye vita
vya kiungu halikuwa la kawaida ndio mana hata miungu ya Goliathi ilishindwa
kumsaidia mtu wake kukwepa lile jiwe dogo, lakini sisi kwa macho yetu tunaona
ni jiwe dogo sana lakini pia Daudi mwenyewe tunamuona ni mdogo sana lakini
uasilia ni kuwa baada ya Mungu kukabidhiwa ile vita alitumia ule ule udogo wa Daudi
na silaha duni tuzionazo kupambana na jitu kubwa lenye silaha za kutosha. Kwa
mtazamo huo sasa utaanza kuelewa udhaifu si kitu cha kupuuzia ndio mana moja ya
agenda ya Roho Mtakatifu kwenye maisha yetu ni “KUTUSAIDIA UDHAIFU WETU” mpaka
Roho Mtakatifu aingie kazini kwa ajili ya udhaifu wetu kamwe udhaifu sio kitu
cha kudharau mana ndio miongoni mwa kazi za Roho Mtakatifu, ukiudharau udhaifu
maana yake umedharau kazi ya Roho Mtakatifu, anakuwa anakosa nafasi kwa mtu
kudhihirisha kilichoko nyuma ya udhaifu kama tutakavyojifunza. Si unakumbuka
ule wimbo unaosema “alipo Roho mambo yote yanawezekana” moja ya kipengele
ambacho kinawezekana akiwepo Roho ni kipengele ambacho sisi ni dhaifu. Sasa
twende hivi…
*“Na alipoulizwa na Mafarisayo,
Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hajui kwa
kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, Tazama,
UFALME WA MUNGU UMO NDANI YENU.” Luka 17:20-21.* Ukisoma hii mistari unaona
shauku kubwa ya Mafarisayo ni kujua siku ambayo ufalme wa Mungu utakuja, lakini
majibu ya Yesu yamekuwa ya kuvutia sana kiasi kwamba inakupa kujifunza vitu
vingi sana, embu nikuulize maswali kidogo, Hivi unaelewaje nikisema utawala wa
Tanzania uko ndani yako? Au mtu akaja kutoka uingereza na tunajua serikali ya
uingereza ni ya kifalme je ni rahisi kuingia akili kusema kuwa ufalme wa
Uingereza uko ndani ya huyo mtu aliyetoka Uingereza? Hizo sio lugha
zinazoeleweka vizuri na nina uhakika hata Mafarisayo hawakuelewa nini Yesu amemaanisha,
kwasababu moja ya tafsiri ya ufalme ni eneo lenye mipaka halali ambalo
linaongozwa na mfalme kama ndio muamuzi wa mwisho, kwa lugha hiyo tukisema
ufalme wa Mungu sasa tumaanishe liko eneo ambalo Mungu hutawala kama mfalme na
yeye ndiyo mwamuzi wa mwisho kwenye hiyo serikali. Swali langu kwenye maelezo
ya Yesu ni hili? Huo ufalme unawezaje kuja kukaa ndani ya mtu? Nikupe dondooo
chache za kukusaidia kutafakari hilo swali, kuna maneno matatu ambayo
yanaelezea ufalme kama ifuatavyo…
1. Ufalme wa Mungu
2. Ufalme wa mbinguni
3. Ufalme(limetajwa hivyo hivyo pasipo kuainishwa kwamba ni
aina gani ya ufalme)_*
Huu ni msingi mkuu wa somo.
Hivyo tuzidi kuweka mambo vizuri ili upate vitu vya kukusaidia
Haya maneno yanatofautiana
sana kimatumizi, sasa napenda nikuletee maana chache nilizozipata wakati
najifunza.
Ufalme wa Mungu ni asili ya tabia ya Mungu
Ufalme wa mbinguni ni eneo ambalo ni asili ya ufalme wa
Mungu, lakini pia huwakilisha mifumo yote ya kiutawala inayohusu ufalme wa
Mungu.
Ufalme maana yake ni utamaduni wa ufalme unavyotawala na
kumiliki duniani.
Hizo maana chache napenda ziwe msingi wa wewe kujifunza
zaidi sasa lengo letu ni hiyo maana ya kwanza ya Ufalme wa Mungu kwa tafsiri ya
kwamba “asili ya tabia ya Mungu” kwa maana hiyo sasa Yesu alichokuwa
anakizungumzia sio aina ya serikali bali asili ya mwenye serikali mana mwenye
serikali akiwepo kuna mambo mengine ni rahisi sana kuwepo, sasa hawa Mafarisayo
hawakuelewa kwasababu mtazamo wao kivipaumbele haukuwa ukifanana na Yesu
kwasababu kitu cha kwanza Yesu alichokuwa anashughurika nacho ni kurejesha kwa
upya asili ya tabia ya Mungu ndani ya mwanadamu. Ndio mana anawaambia hiyo
asili ya tabia ya Mungu tayari iko ndani yenu.
Sasa hapa ndipo nataka tuanze kujifunza somo letu, swali
langu kwa Yesu ni hili, alitazamaje au anamtazamaje mwanadamu ambaye ni dhaifu
na kuamua kuweka asili ya tabia ya Mungu ndani ya mwanadamu ambaye ni dhaifu?
Mana sitegemei kabisa ununue gari lenye thamani kubwa sana na kwenda kulilaza
kwenye zizi la ng’ombe!! Huo ni mfano ijapo sio mzuri sana. Lakini
ninachomaanisha asili ya tabia ya Mungu jinsi ilivyo iweje iwekwe kwa mwanadamu
aliyedhaifu? Kuna agenda ya msingi sana hapa lazima tuione mana kama hakuna
agenda ya msingi basi somo lisingekuwepo. *“Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na
nguvu.” 2 koritho 12:10*
Kwa huu mstari kuna mambo mawili ya msingi ya kulinganishwa
(i) Niwapo dhaifu
(ii)Nilipo na Nguvu.
Inasema nilipo dhaifu ndipo nilipo na nguvu kwa minajili hiyo
mahali anapokuwa dhaifu ndio hapo hapo anakuwa na nguvu swali langu ni hili
*iweje mahali alipo dhaifu pawe na nguvu wakati panatambulika kama mahali
dhaifu?* Hili swali huwezi pata majibu yake kama hujajifunza mitazamo miwili
mmoja mtazamo wa Mungu na wapili ni mtazamo wa shetani ambao tutajifunza hapo
chini…
Tutajifunze vitu vifuatavyo
mpaka mwisho wa darasa letu…
1. Mtazamo wa Mungu juu ya mwanadamu.
2. Mtazamo wa shetani juu ya mwanadamu.
3. Asili ya udhaifu.
4. Siri zilizofichika kwenye udhaifu.
5. Namna ya kutumia udhaifu wako kutengeneza aina bora ya
maisha.(Namna ya kuongeza uthamani wa maisha yetu jinsi tulivyo.)
Hivyo ndo vitu napenda tujifunze hatua kwa hatua na tutaona
thamani kubwa iliyofichwa ndani yake. Kwa hiyo kuna vipengele atafundisha Bro.
Jr. Dugilo.
Tuanze leo mtazamo mmoja tu
naoni ni Mtazamo wa Mungu.
*1. MTAZAMO WA MUNGU KWA
MWANADAMU.*
*“Mungu akaumba mtu
kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na Mwanamke aliwaumba.”
Mwanzo 1: 27.**
Mungu alimuumbwa mtu kwa namna hiyo hapo akiwa hana mwili
huu wa nyama, kwa hiyo kama kwa mfano wa Mungu, mtu anafanana na Mungu kwa
maana hiyo kuna vitu viko kwa Mungu na kwa huyu mtu pia viko, kwa kufuata hiyo
lugha ya mfano wa Mungu. Lakini pia ukisoma huu mstari unasema *“Nitakushukuru
kwa kuwa NIMEUMBWA kwa jinsi ya ajabu ya kutisha…Mifupa yangu haikusitirika
kwako, Nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi;” Zaburi 139:14-15.* Hayo
ni maneno ya Daudi akiusifia uumbaji wa Mungu jinsi ulivyo kwake namna
anavyojitazama, utaona anasema neno zuri sana “ *Nilipoumbwa kwa ustadi”,*
licha ya kuwa tuna mwili uliotoka mavumbini lakini ustadi mkubwa sana ulitumika
kutuumba sisi sasa tumalizie huu mstari *“Mungu akaona kila kitu alichokifanya,
na Tazama, ni chema sana.” Mwanzo 1:30* . Kwa mstari huu wa mwisho hakuna kitu
ambacho alikiona kina mapungufu iwe kwa mwanadamu au kwa kiumbe yeyote yule
hapa duniani. Kwa lugha rahisi kwa kipindi hicho chote Mungu hakuwa na neno
linaloitwa “ *UDHAIFU* ” kwasababu kila kiungo na kila kiumbe kilikuwa na
thamani sawa sawa na *kusudi* lake. Baada ya Mtu kuumbwa kwa namna hiyo, Mungu
aliweka mahitaji mawili kwa mwanadamu na tutaona sababu za kuwekwa hayo
mahitaji mawili.
Hitaji la kwanza *01: Mwanadamu alikuwa anauhitaji uwepo wa
Mungu ili aweze kufanya kazi za Mungu za kila siku.*
Hitaji la pili *02: Mwanadamu alikuwa anamuhitaji Mungu
mwenyewe kwa ajili ya kutawala kwa kufuata maelekzo yatokanayo na agenda na
mapenzi yake Mungu.*
NB:- Kuna tofauti kati ya uwepo wa Mungu na Mungu mwenyewe,
tafsiri mojawapo ya uwepo wa Mungu ni mahali ambapo nguvu za Mungu zipo lakini
kuna mazingira mengine Mungu yeye mwenyewe yuko mahali hapo. Mfano wake Adamu
aliwekwa bustanini Edeni mahali kwenye uwepo wa Mungu sawasawa na tafsiri ya
neno “ *EDENI* ” lakini pia Mungu alikuwa na utaratibu wa kushuka jioni
(alasiri) kumtembelea Adamu. Kwa mfano huo hayo ndio mahitaji ya msingi sana
ambayo mwanadamu aliumbwa kuyategemea kwa ajili ya maisha yake ya kila siku.
Kwa hiyo mwanadamu akiwa na vitu vyote pasipo hayo mahitaji mawili hawezi
kuishi vile alivyokusudiwa kuishi.
Mungu aliweka hayo mahitaji kwasababu alijua kwakuwa
mwanadamu amemuumba na kumpa mamlaka kamili ya kumiliki dunia, lakini pia huyu
mwanadamu anafanana naye sawa sawa na Mwanzo 3:22, Mungu akaona ili kuwepo na
aina nzuri ya utawala katika ufalme wake ilibidi mwanadamu awe tegemezi kwa
Mungu. Hivyo hayo mahitaji mwanadamu hawezi kuyakwepo.
Ngata Hadson: Ahsante sana kwa leo tuachie
hapo na kesho tutajifunza mtazamo wa shetani kwa mwanadamu. Halafu ndo tutajua
asili ya udhaifu ilipoanzia. Kwa hapo unaona nguvu iliyoko kwenye hayo mahitaji
mawili. Mungu ametubariki sana.
Ahsante sana jana tulikuwa na
utangulizi mrefu sana na pia tuliona kipengele cha kwanza MTAZAMO WA MUNGU KWA
MWANADAMU.
sasa twende hatua kadhaa
mbele
Naomba baada ya somo ndo watu
wacomment iwe kwa swali au kwa lolote lililoko ndani ya somo.
2.MTAZAMO WA SHETANI KWA
MWANADAMU.
Kwakuwa shetani alikuwepo wakati mwanadamu anaumbwa na
aliona mwanadamu alivyobarikiwa na jinsi mwanadamu jinsi alivyomkamilifu,
shetani akawaza moja ya njia nzuri ya kumpata mwanadamu ni kusababisha
anayakosa mahitaji mawili hayo tuliyoyasoma. Kwasababu kwa kukosa hayo mahitaji
mawili vitu hivi vitatokea…
Asili ya tabia ya Mungu(Ufalme wa MUNGU) utaondoka,
Uwepo wa Mungu kama hitaji hatolipata
Lakini pia Mungu mwenyewe hatokuwa na mahusiano na
Mwanadamu.
Kwa hiyo mtazamo wake kwa mwanadamu ni huu mwanadamu ni
mkamilifu kwa kila kitu isipokuwa tu akikosa hayo mahitaji mawili tu anakuwa
sio mkamilifu kwa namna yoyote. Na pia shetani anajua kuwa uhitaji wa kiungo
chochote cha mwanadamu nao pia unahitaji uwepo wa Mungu, hivyo uwepo wa Mungu
hukamilisha kila kitu kwa mwanadamu.
Kabla ya dhambi rank hii ya
uongozi ilikuwepo. Na kabla ya mwanadamu kuumbwa.
1.Mungu
2. Malaika mkuu(Lusifa)
Kutokana na hitifaki hiyo
shetani aka asi mbinguni, moja ya wazo la Mungu ni kumuumbwa mtu ambaye atakuwa
hayupo chini ya shetani kimamlaka ya kiungozi hivyo ikabidi mwanadamu awe mkuu
kuliko malaika ili shetani awe chini ya mwanadamu
Ndio tafsiri ya sisi kuwa
mfano na sura ya Mungu, sisi ni level za Mungu kwa hiyo kuweza kumiliki hapa
duniani ilimbidi shetani amfanye mwanadamu atende kosa kama lake lililomfanya
yeye kuondolewa kwenye nafasi yake ya mara ya kwanza
Baada ya kuumbwa mwanadamu
uongozi ulikuwa hivi
Mungu
Mwanadamu
Malaika wakawa ni watenda kazi
Sasa angalia asili ya UDHAIFU
ilipokuja
Kwa Mungu hakukuwa na Neno
Udhaifu, na udhaifu umekuja baada ya dhambi kuwepo mana tulikuwa tunakamilishwa
na mahitaji mawili tuliyosema hapo mwanzo. Hivyo basi moja ya sababu ya uwepo
wa udhaifu ni kutokuwepo kwa mahitaji mawili tuliyoyasema hii tunaipata katika
Warumi 8:26 inasema "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu..."
Sasa usifike kule hatujui
kuomba, hiyo ni aina ya udhaifu lakini nataka uone hivi
Hatukuumbwa tuwe tunaomba kama
hivi tunavyoomba leo, kuomba huku kumekuja kuwa mbadala wa aina ya kwanza ya
mawasiliano
Tuliumbwa tuwe tunaongea na
Mungu akija duniani kila mara hivyo kutokuja kwake baada ya dhambi ndio udhaifu
ulipoanzia ndio mana unaona mbadala wake ikabidi Roho aingilie kati kuubeba
udhaifu ili tuwasiliane na Mungu kwa ubora ule ule wa mara ya kwanza na kuzidi.
Moja ya kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa sio kuchukua udhaifu wetu kwasababu hatukuwa na hiyo agenda kipindi kile lakini Roho aliibeba hiyo agenda ili kurahisisha uimarishwaji wa ufalme wa Mungu kama alivyokusudia.
Sasa tazama hiviii
*ASILI YA UDHAIFU.*
Kama tulivyoona mwanzo kuwa palipo udhaifu kuna nguvu, sasa
tuzungumzie kutoka kwenye kilichoko nyuma ya udhaifu ambacho ndo tunaita nguvu.
Nguvu iliyoko kwenye udhaifu ndio inatafsiri aina ya udhaifu wenyewe, kwa hapa
tunapata aina mbili za nguvu...
1. Nguvu ya utegemezi kutoka kwa Mungu.
Kama nilivyosema mwanzo tuliumbwa kuwa na mahitaji mawili ya
msingi kumtegemea Mungu na uwepo wake hivyo nguvu hiyo inatoa aina ya kwanza ya
udhaifu. Na huu udhaifu huonekana kwa lengo la kuudhihirisha ukuu wa Mungu kwa
Mwanadamu. Hapa ndipo tunasema *“Uweza wa Mungu hutimilika katika udhaifu”*
mahali tunapofika na kuona hatuwezi kinachobaki ni kutegemea msaada kutoka kwa
Mungu, ndio mana Mungu hutumia sana viumbe dhaifu, au viungo dhaifu kujitukuza
kwa sababu viko tayari kutegemea nguvu za Mungu kwa ajili ya udhihirisho wa
kile kilichokusudiwa na Mungu.
*2. Utoshelevu kutoka
kwa shetani.*
Mwanadamu alivyoasi, mbegu ya uasi ikawa ndani yake ikidai
mazingira ya kujidhihirisha, Baada ya dhambi, shetani alipata nafasi ya kuwa
mtoaji wa mahitaji yale mawili kwa mwanadamu, hivyo mwanadamu kutokujua aina ya
utoshelevu wake inapotoka huishia kutoshelezwa na shetani na Matokeo yake ni
udhihirisho wa vitu vya shetani katika maisha yake hapa utakutana na magonjwa
na aina ya udhaifu ambao chanzo chake si Mungu. Mfano mtu ni mzinzi huo udhaifu
haujatokana na Mungu. Ijapo Mungu anao uwe udhaifu pia kudhihirisha Nguvu zake
mana ni Mungu pekee ndiye anayestahili kutoa mahitaji mawili makuu kwa
mwanadamu. Hivyo uwezo huo wa Mungu huwezi kumsaidia mwanadamu kuvuka kwenye
kila aina ya udhaifu wa namna hii ya pili.
Ilikuwa hivi….
Kwa maelezo hayo ya mwanzo bila shaka unaweza fahamu udhaifu
umeanzia wapi, baada ya mwanadamu kutenda dhambi mahitaji hayo tuliyoyasema
hakuweza kuyapata tunaona kwenye huu mstari “ *Kwa hiyo BWANA Mungu akamtoa
katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi
akamfukuza huyo mtu…” Mwanzo 3:23-24* Kwa tafsiri ya neno “ *edeni* ” ndo
unajua kuwa kufukuzwa bustanini ni moja ya ishara mbaya sana kwao kwasababu
watakosa uwepo wa Mungu, lakini pia watamkosa Mungu ambaye alikuwa akishuka
mara kwa mara jioni kuwatembelea maana yake kama alikuja hakuwaona siku hiyo
waliyotenda dhambi, na yeye anajua kabisa amewafukuza mahali ambapo alikuwa
anakuja mara kwa mara bila shaka hawezi kwenda tena kwa ajili yao bali kwa
ajili ya shughuri zake pengine. Hivyo mahitaji mawili yakawa ni makali sana
kwasababu shetani ndio akataka akae kwa ajili ya kuwapa kile walichokikosa
baada ya Mungu kuwaondoa bustanini. Hapo ndipo udhaifu ukaanza kuonekana
kwasababu uwepo wa Mungu ukimfunika mtu hakuna anayetambulika kwa jinsi ya
mwili bali kwakuwa sisi ni mfano na sura ya Mungu basi nasi ni roho kwa kuwa
Mungu ni roho, hivyo katika roho tunajikuta wote tuko mbele za Mungu. Lakini
uwepo wa Mungu ukiondoka hapo ndo utaona aliyemzinzi anaweza kuendelea na
uzinzi wake, ukisoma habari za Miriumu,
Haruni na Musa utaona hii kesi baada ya Miriumu kumsema Musa mbele za Haruni,
hasira ya Mungu ikawaka juu yao akapata ukoma lakini cha ajabu ukoma
haukuonekana mpaka ule uwepo wa Mungu ulipoondoka. Ndivyo kazi ya uwepo wa
Mungu kujaza mahali palipo pa nyonge.
Hivyo udhaifu kuonekana ni ishara ya kitu fulani, ndio mana Yesu
anapenda kutumia udhaifu kujidhihirisha mana anajua akiacha udhaifu ufanye kazi
wenyewe hakuna kitu kinaweza fanyika. Lakini pia mwanadamu mahali ambapo hana
udhaifu kiburi kile cha kuwa yeye ni mungu wa dunia hii humuingia ndio mana
Mungu aliweka yale mahitaji kumsaidia kuishi huku Umungu ndani yake
usimkorofishe na Mungu aliyemuumba. Hujawai kuona watu wakifikia hali fulani
kihuduma kuna kiburi, au majivuno huinuka n.k. kuonekana kwa udhaifu huo ujue
uwepo wa Mungu na wenyewe hauwezi kukaa mahali hapo muda si mrefu utamuona huyo
mtu ni mtupu.
[6/22, 8:39 PM] Ngata Hadson: Bila shaka hapo umeona jinsi
udhaifu ulivyoanza kutambulika, iko mifano mingi sana, ukiondoa hiyo ya Miriumu
na Haruni, lakini embu fikiri hivi...moja ya agenda ya Yesu kuja hapa duniani
ni kushughurika na kila udhaifu ikiwepo na ule wa Kutokujua kuomba kwa jinsi
itupasavyo, ndio mana alivyoondoka akatuachia Roho Mtakatifu
[6/22, 8:41 PM] Ngata Hadson: Unakuja tena kuona Katika kila
udhaifu iwe kuahindwa kufanya jambo fulani Biblia ikasema "Tunayaweza
mambo yote katika Yeye atutiaye nguvu"
maana yake udhaifu utakapokuzuia kufanya jambo fulani iko NGUVU YA MUNGU
ya kukuvusha wakati wengine wanashangaa bahari ya shamu kumbe Musa alikumbuka
kukabeba kale kafimbo, wakati Sauli
anashindwa kuongoza ile vita dhidi ya Goliath yuko jamaa Daudi na kombeo lake
anakuja kupiga mambo na watu wanashinda
Hii sasa nakupa ili uone, kila udhaifu huwa na sababu yake kimatumizi, mfano Shetani anaweza kuruhusu udhaifu wako ukufanye kumtumikia yeye kwa nguvu zote na pia Mungu anaweza kufanya hivyo pia.
NB+ Shetani kwenye udhaifu anafanya kazi kwa spidi kubwa
sana kuliko kwenye ubora wa mtu. Angalia wakristo wengi udhaifu wanajisingizia
ni upi halafu angalia wengi wamekamatwa hapo hapo.
Shetani amewapa watu nafasi ya
kuona udhaifu umewekwa kwasababu hatukuumbwa wakamilifu. (NO) Tuliumbwa wakamilifu na ukamilifu wetu ni
KRISTO.
BE BLESSED leo naomba tuishie hapo, kesho nitamalizia kipengele cha mwisho halafu nitamkaribisha Mwl na Bro Jr. Dugilo aendelee na kipengele vinavyofuatwa
Mungu wa Bwama wetu Yesu Kristo ahsante kwa neema hii, ninakuomba unitakase kwa damu ya Yesu tena uniweke kamili kutumika vile ulivyokusudia leo katika hali zote jina lako litukuzwe sasa na hata milele. Mbariki kila mtumishi wako ambaye anafatilia somo hili kwa jina la Yesu amen.
Ahsante sana, mpaka sasa tumeshaviangalia vipengele kadhaa, leo napenda kumalizia kipengele cha mwisho kwa upande wangu ili kesho mwalimu wetu afundishe nae kipengele chake mana kina vitu vikubwa sana na vya kushiba mana tumeanza vipengele vidogo vidogo kwenda vikubwa
Siku ya nyuma tulisema leo tutaangalia siri zilizojificha kwenye udhaifu
Nitakutajia na kufafanua baadhi kwa uchache na urahisi kabisa.
3*SIRI ZILIZOFICHWA KWENYE UDHAIFU.*
“ *Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, MIMI SI MSEMAJI, tokea
zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana MIMI SI MWEPESI WA
KUSEMA, na ULIMI WANGU NI MZITO. BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa
cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi?...Basi sasa,
enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.”
Kutoka 4:10-12.* Nimevutiwa sana na mazungumzo kati ya Mungu na Musa, yamejaa
vitu vya ajabu sana, baadhi ya ninavyotaka kujifunza ni udhaifu wa Musa wa kuwa
na *“ULIMI MZITO”* hiyo ni taswira aliyonayo Musa kuwa yeye ana ulimi mzito
sana, lakini taswira aliyonayo Mungu ni hii watu ambao sio waongeaji ni
watendaji sana, hivyo sasa uangalie hivi…Mungu anavyowaza kwenye udhaifu wa
Musa na suluhisho lake, Musa aliona uzito wa ulimi wake ndio tatizo Mungu
akamwambia *“nitakufunisha utakalo linena”* si rahisi mimi nikikwambia ulimi
wangu mzito eti uniambie utanifundisha nitakalo linena sasa nitalinenaje wakati
ulimi wangu mzito, kwa hiyo hata ukinifundisha sitaweza mpaka unifundishe namna
ya kuongea huku nikiwa na ulimi mzito, mtazamo wa Mungu sio ulimi kuwa mzito lakini
cha kuongea ndio kitu cha msingi kwa hiyo katika udhaifu wa Musa kilichokuwa
kimefichwa ni uwekwaji wa kitu cha Mungu, mana Musa angetambua kuwa ulimi wake
unaweza kusema bila shida “ *ASINGEHITAJI KUFUNDISHWA CHA KUSEMA”* licha ya
udhaifu huo huo Mungu akakubari kukaa kwenye kinywa dhaifu maana yangu ni hii
uwepo wa udhaifu wa kinywa cha Mungu ilikuwa ni njia nzuri sana ya kukubali
kufundishwa cha kusema kuliko kama asingekuwa na ulimi mzito. Soma huu
mwingine…
*“Nawe utasema naye,
na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na
pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya. Naye takuwa msemaji
wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe utkuwa mfano wa
Mungu kwake. Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo utzifanya zile
ishara.” Kutoka 4:16-17*
[6/23, 8:19 PM] Ngata Hadson: Musa baada ya kupewa Haruni
kuwa ndio msemaji wake, unaona bado Mungu anasisitiza kuwa nitakuwa na vinywa
vyenu hata kama Haruni ulimi wake sio mzito, kinachotakiwa sio wepesi au uzito
wa ulimi bali kinachotakiwa ni uwepo wangu kwenye hicho mnachokisema. Hapo sasa
Mungu akafanya maajabu ikabidi Haruni awe kinywa cha Musa halafu Musa awe mfano
wa Mungu kwa Haruni maana yake alivyotoka kwenda kwa Farao hakwenda Musa bali mfano
wa Mungu ulikuwa umeenda kwa farao, hivyo Farao alikuwa anapambana na sio Mungu
aliye mbinguni bali Mungu aliyeduniani ambaye ndiye Musa mwenye kinywa kizito.
Musa hakuwa na majeshi lakini kwasababu anamuwakilisha Mungu, ikabidi majeshi
yake yawe vyura, chawa, nyoka n.k kwa mantiki hiyo sasa sidhani kama kuna
udhaifu wowote kwenye maisha yako utaudharau mana umebeba kitu cha ajabu sana
ambacho kikitumika mataifa yatashangaa.
Ukienda kujifunza maswala ya vita, biashara n.k utagundua
kuwa mafanikio ya mtu mwingine ujue ni udhaifu wa mwingine alioufanyia kazi.
Ndio mana kampuni kubwa zinajari sana sanduku la maoni mana ndiko udhaifu wao
unapoandikwa hivyo wanapata muda wa kujifunza na kufanyia kazi huo udhaifu
ulioandikwa na wateja wao. Kwenye majeshi utaona ili ushinde vita ni muhimu
kujua unayepigana naye ubora wake uko wapi na udhaifu wake uko wapi, swali la
msingi kwa nini udhaifu uwe ni muhimu sana kwa ushindi wa upande fulani?
Nadhani umewai kusoma hadithi ya sungura na kobe walivyokuwa
kwenye mashindano, nikupe mitazamo yao.
*Sungura*
Kwa kuwa anajua kukimbia sana na ni mjanja kuliko kobe
akachukulia hiyo sifa na kumdharau kobe udhaifu wake wa kutokimbia sana,
akajificha kabla hata hajafika mwisho wa mbio.
*Kobe* .
Alijua kabisa kwa kuwa mwendo wake ni mdogo basi inambidi
asifanye uzembe wa kucheza, kulala, wala kushangaa, alijikuta mshindi kwasababu
alidhamiria kushinda licha ya udhaifu wake juu ya sungura.
Nini nataka uone…?
Ile kuna watu wameanza mbio mbele yako haimaanishi ndio
washindi, kwasababu mwisho wa mbio ndo ushindi upo sio mwanzo wa mbio. Hivyo
haijalishi una udhaifu gani umakini wako kwenye huo udhaifu utakusaidia sana.
Kufanya vizuri sana kwenye hicho unachokifanya
[6/23, 8:29 PM] Ngata Hadson: Ukichunguza kwa umakini maeneo
ambayo mtu ana udhaifu hutumika sana na shetani kumpiga vita sana, Shetani
hawezi kupoteza muda wake mwingi kuutafuta udhaifu wa mtu kama huo udhaifu
hauna umuhimu kwake, ndivyo ilivyo kwa Yesu hawezi kushughurikia udhaifu wa
watu wake kama huo udhaifu hauna faida kwenye ufalme wake. *Swali langu la
msingi ni hili kwanini shetani aone hayo maeneo kwake ni ya muhimu na kuna kitu
gani kilichojificha nyuma ya udhaifu wa kila mtu?* Hizo ndo agenda zetu za
msingi.
*1. Mahali ulipo
dhaifu ndipo penye utukufu wa Mungu.*
Moja ya jambo kuu na la msingi ambalo watu wengi wanalisahau
ni sehemu ambazo Mungu utukufu wake ni rahisi kujidhihirisha, moja ya hizo
sehemu ni zile zenye udhaifu, swali kwanini? Mara zote akili za mwanadamu zipo
kutumika katika uwezo wake wote pasipokuhitaji msaada hivyo akili inapochoka
huitaji msaada kwa haraka sana kuliko kawaida hivyo mahali palipo dhaifu akili
huitaji msaada ndipo utukufu wa Mungu hujidhihirisha. Soma huu mstari..
*“Kwa kuwa hakuna
kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye
alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kutenda dhambi.” Ebrania
4:15* kwa akili za kawaida Yesu asingejishughurisha na udhaifu wetu kama anajua
kuwa udhaifu hautampa utukufu mkubwa. Hivyo usiudharau udhaifu ulipo bali
utumie udhaifu huo vizuri. Mara nyingi wanaodharaulika ndio huwa mashujaa.
*“Mungu hutumia viumbe dhaifu kujitukuza”*
*2. Mahali ulipo
dhaifu ndipo asili ya nguvu za Mungu hudhihirika.*
“ *Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” 2 koritho
12:10* Umewai jiuliza swali hili iweje Paulo asemae alipo dhaifu ndipo alipo na
nguvu, uhalisia sio kweli, kwasababu kama wewe ni dhaifu ni dhaifu tu lakini
siri iliyoko hapo ni kuwa udhaifu unapokuwepo kuna nguvu nyingine huonekana
ambayo hiyo nguvu inakufanya kuonekana ni mwenye nguvu na nguvu hizo sio zako
bali Mungu mwenyewe mana tayari wewe ni dhaifu. Kwa hiyo ninapokuwa dhaifu
mahali, kinachoonekana kwasababu mimi nimebeba sura na mfano wa Mungu, Mungu
hudhihirisha nguvu zake mahali nilipo dhaifu. Moja ya jambo napenda uliweke
akilini ni hili *“Mungu hufanya mambo makubwa sana kututumia sisi sio kwasababu
ya sisi bali kwasababu ya sura yake na mfano wake aliouwekeza ndani yetu,*
*kuliko yeye kuaibika mbele za watu kwasababu ya udhaifu wetu yuko tayari kutumia
nguvu zake wakati tunapokuwa tumechoka.”* Nadhani unamkumbuka Musa na Haruni na
Huri walipokuwa mlimani, Musa akiwa amechoka majamaa wanamshikilia mikono ili
ushindi upatikane vitani alipokuwa Yoshua. Hiyo ndo siri ya msingi sana.
Ni rahisi kuwa mnyenyekevu hasa ukiguswa sehemu yenye
udhaifu wako.
Hii ni ya kawaida wewe unafahamu si mara zote wanaohitaji
msaada wanakuwa katika hali nzuri, mara nyingi kwenye kipengele cha udhaifu ni
rahisi mwanadamu kuhitaji msaada, tena kwa unyenyekevu mkubwa sana.
*3. Udhaifu hutumika
kama mlango wa kuingizia silaha za kifalme upande wa giza.*
Udhaifu hutumika kama mlango wa kuingizia silaha za kivita
za kifalme hivyo kwakuwa Mungu anaishi ndani yetu uwe na uhakika udhaifu wetu
kwa Mungu ni fursa kubwa na ya ajabu sana kupigana vita na kushinda. Bila shaka
unamkumbuka Daudi, soma sasa huu mstari… “ *nami nitamshambulia wakati
atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu;…” 2
Samweli 17:2)* umeona moja ya silaha ni hofu ambayo itaingizwa wakati mtu
amechoka amekuwa dhaifu. Usijidharau mahali ulipo dhaifu.
*4. Udhaifu humpa mtu
kufikiri kujihami hivyo humfanya kuwa salama muda mwingi.*
“ *Wibari ni watu dhaifu; lakini hujifanyia nyumba katika
miamba.” Mithali 30: 26.* Wibari ni aina ya wanyama wadhaifu lakini kwa kutumia
udhaifu wao huamua kujenga nyumba zao kwenye miamba kwa ajili ya usalama wao
ndivyo ilivyo kwa watu.
*5. Uweza wa Mungu
hutimilika katika udhaifu.*
“ *Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu
hutimilika katika udhaifu,…” 2 korintho 12:9*
Katika udhaifu wetu UWEZA WA MUNGU hutimilika na unafahamu
uweza wa Mungu ukitimilika. Vifuatavyo hutokea
Ubora huonekana.
Ukuu wa Mungu hauwezi kudhihirishwa kama aliyeubeba hajataka
kuudhihirisha hivyo udhaifu pia ni chombo kizuri kudhihirisha ubora wa Mungu
kupitia mtu, nadhani unamkumbuka Musa kile kisingizio cha kuwa na ulimi mzito
na unajua mambo makuu aliyoyafanya licha ya kuwa alivyokuwa.
i. Taswira ya udhaifu hubadilika.
Nguvu za Mungu zikidhihirishwa nafasi ya udhaifu kuonekana
inakuwa tena hakuna, nani alijua kuwa kile kishindo kilikuwa ni cha wale
wakoma, piga picha jeshi zima la maadui walikimbia kisa kusikia kile kishindo,
na hawakuwa na muda kuchunguza kuwa kishindo kilikuwa ni cha nini walichojua ni
kimoja kuwa majesho mengi yanakuja kumbe vijamaa vine vyenye ukoma, udhaifu ule
Mungu aliutumia kama Fursa hivyo basi waliokuwa wanaenda sio wakoma tena bali
ni nguvu za Mungu wa majeshi. Bila shaka sitaki kuudharau udhaifu wangu hivi
hivi nilivyo nitafanya mambo makubwa ya kushangaza dunia.
*II. Upekee wa mtu
huonekana kutokana na udhaifu wake.*
Nani angeamini kuwa Mungu wa Daudi anaweza tumia silaha duni
kumshinda Goliathi kama asinguruhusu mavazi ya sauli yasimtoshe Daudi. Mungu
alitaka pia tujue likija kwenye swala la upekee wa ufanyaji kazi wa mtumishi
wake anaweza kutumia vitu dhaifu kufanya kitu cha kipekee na cha kutisha.
Hakuna tena kwenye Biblia aliyetumia silaha kama zile za Daudi. Upekee huo.
Hata leo unaweza Fanya hivyo pia kuweka upekee kwenye jambo lolote lile.
*III. Kukuzwa na kutukuzwa huonekana kwasababu ya
kitu cha tofauti ambacho Mungu amekiachilia kitimilike kwa mtu.*
[6/23, 8:32 PM] Ngata Hadson: Waow Mungu ahsante kwasababu
nimekimalizia kipengele hichi kwa namna hii. Ahsante sana kwa kuendelea kuwa
tayari kujifunza Mungu akubariki. Kwa leo naomba tuishie hapo. Kesho
tutaendelea hatua nyingine na Mwalimu.
Mungu awatunze na kuwahudumia kwa utoshelevu kutoka kwake.
Mwl Dugilo:
Namshukuru Mungu kwa hii nafasi niliopata ya kushirikisha kidogo kuusu
KUONGEZA THAMANI KATIKA MAISHA.
Leo sitofundisha ila kuweka msingi
ambao kesho nitakuja kujenga juu Yake
Nianze hivi.
Katika maisha kila binadamu kuna
mahali anataka kufika, inaweza tusifanane tunapotaka kufika au kufikia either
iwe kielimu, kumahusiano, kiuchumi au kihuduma ila kuna mahali tunataka kufika, Tatizo ni kwamba ingawa tunayo hiyo
sense ya kuzidi na kufika mahali lakini si kila mtu anajua hasa nini anataka na
wapi anataka kufika
Ndio maana kuna mtu anaweza fikiri anaitaji fedha dhaidi au elimu zaidi na anaenda anaongeza ila mwisho wa siku anakuta hakuna utoshelevu
Ni kwanini mtu awe na hiyo sense ya kuongezeka au kwa maana nyingine kuongeza thamani ya maisha yake?
Ni kwanini ijapokuwa watu wanaangaika kuongeza thamani lakini mwishowe wanaishia kupoteza thamani?
Nini hasa kinatakiwa kifanyike kati ya wewe ulivyo na unaetakiwa kuwa?
Kwanini watu wengi wako confused (wamechanganyikiwa) hawajui nini chakufanya?
Haya maswali ndio nitakuwa nayajibu hapo kesho nitakapokuwa naendelea....
Na kitu kingine nitakigusia kesho ni
tofauti ya UDHAIFU na UBOVU wa mtu, na namna ya Kudeal na kila kimoja wapo na
nini mtazamo wa Mungu juu kila kimoja wapo
Kwa leo naomba niishie hapa ila nishauri endelea kuombea ili Mungu anipe kile ambacho kitatuvusha sote na kutupa nafasi mpya na kuongezeka
Niliahidi jana kuwa leo nitakuja
kuendelea na kujibu maswali ambayo niliweka hapo juu
Basi karibu tujifunze, Hapo nyuma nilisema kila mtu
anayosense ya kuongezeka au kutaka kuwa
bora zaidi, swali ni kwanini?
Ukisoma mwanzo 1;26-31
Utagundua aina ya watu Mungu alio waumba walikuwa na kitu kinaitwa
UTOSHELEVU,
Ukifuatilia utagundua huo utoshelevu ulijengwa kwenye mambo
manne makuu.
1/ usahihi wa eneo walilokuwa (edeni)
2. Usahihi wa kazi waliokuwa wanafanya (kutunza edeni,
purpose)
3.usahihi wa uwepo (fellowship na Mungu)
4. Usahihi wa utaratibu waliokuwa wanaoparate chini
yake(Neno la Mungu...msile tunda la mti wa kati kati)
Hayo ndio mambo manne makuu ambayo utayaona katika bustani
ya edeni kabla ya dhambi ambayo yalimfanya adam na eva kuwa na utoshelevu.
Sasa ukifuatilia utagundua baada ya
dhambi, kila kitu kati ya hivyo hapo vinne walipoteza, na mwisho wake
utoshelevu ukapotea wakaanza kuitaji.
Sasa kukosa utoshelevu ni very tricky feeling mara nyingi
utahisi kuna kitu ambacho unaitaji na unaweza usijue ni nini unachoitaji ndio
maana adamu uitaji wake wa kwanza ulikuwa nguo japo hilo sio chanzo cha
utoshelevu wake na kimsingi alicho hitaji sio hiko kwasababu alichopoteza sio
nguo,
Tatizo ni hili kuwa watu wengi hawana utoshelevu ndani na
mwisho wa siku wanaanza kutafuta vitu ili kutuliza ile hali wanaoisikia ndani
lakin baada ya kupata bado wanagundua kuna la dhaidi.
Wako watu wanaona ili apate utoshelevu anaitaji shule zaidi,
mwingine ndoa, mwingine pesa zaidi n.k lakin baada ya kupata bado wanagundua
there is more ili utoshelevu uje
Sasa hapa ndio dhana ya kuongeza THAMANI ilopo,
Kuna mambo kadhaa ya kuyajua katika kuongeza thamni
1.Hauwezi kuongeza thamani kama unayo, maana yake muongeza
thamni huwa hana
2.huwezi kuongeza thamani kama hujui ni nini huna na nini
unaitaji ili kujenga thamani
3. Kuongeza thamani sio mara zote kutakupa kuwa unaetakiwa
kuwa,
4.kuongeza thamani ni mchakato na sio event/tukio, ambao
unagharama kupunguza, kuongeza na kutunza vitu
5. Lazima ujiulize hiyo thamani itakupa unachokiitaji?
Sasa kutokea swali la 5 hapo juu linajibu swali ambalo niliuliza jana kwanini watu wengine katika mchakato wa kuongeza thamani wanajukuta wanashuka thaman?
Je Kile unachokitafuta ukikipata kitakuwa sawa na kile
unachokiitaji?
Katika kitabu cha mwanzo Adamu na eva walijificha kwasababu
ya aibu swali je baada ya kushona majani(kuongeza thamani yao) walipata
utoshelevu?
Na je baada ya Mungu kuwashonea ngozi walipata utoshelevu?
Jibu ni hapana,, kwasababu walichoitaji ili kuongeza kama
thamani ili wapate ustoshelevu haikuwa katika walichokuwa wanatafuta (mavazi)
ila ilikuwa katika yale mambo manne tuliojifunza kule juu.
Ili upate utoshelevu nini unaitaj? Je unadhani ukipewa vyote
ulivyo navyo katika list ya maitaji yako utapata utoshelevu? Je thamani yako
itakufikisha pahali pa kusikia unakila kitu?
Sasa inapotokea umepata unachokiitaji alafu bado unahisi kuna la dhihada huwa unajisikiaje?
Je baada ya kuoa/kuolewa alafu ukagundua kuwa hakuna
ulichokidhania utapata utajisikiaje?
Kuna watu wako confused kwadababu wamejaribu kila kitu
possible wanachoweza kujaribu katika kuongeza thamani ila bado mwisho wa siku
utoshelevu haukuja.
Hii ni kwasababu utoshelevu haujajengwa katika VITU ambavyo
watu wanatafuta..
Kwamaana rahisi dawa ya utoshelevu sio vitu,
Adamu alikuwa na utoshelevu japo hakuwa na gari, wala
nyumba, wala mavazi..
Ndio maana biblia ikashauri TAFUTENI KWANZA UFALME (yale
mambo manne) then hayo mengine mtadhidishiwa ...sasa tatizo watu wanaanza
kutafuta yale ya dhihada ili kujaza gap la UFALME WA MUNGU katika mioyo yao
kitu ambacho sio sahihi,
I dont care unatafuta nini, kama yale mambo manne
niliyoyataja pale juu hauna huwezi pata utoshrlevu...
Unaweza pandisha thamani kulingana na standard za dunia ila
utoshelevu wa moyo wako hautokuja..
Kuna tofauti kati ya kujitosheleza katika ulichotaka au takiwa kuwa nacho na kutosheka katika kile unachoitajika.
Kama ili upate kazi unaiyoitaka unaitaji PhD ukiipata hiyo
PhD utakuwa umejitoshelrza kwa ajili ya hiyo kazi na sio utoshelevu wa ndani ya
moyo wako
Kwasababu hiyo nashauri kama unaitaji utishelevu tafuta
kwanza yale mambo manne ambayo adam na eva walipewa pale edeni.
Nimalizzie kwa kuzungunzia UDHAIFU kama sehemu ya vitu ambavyo vinawasumbua wengi hasa inapokuja katika swala la kuongeza thamani yako kama mtu.
Moja kati ya kitu naamini watu wengi wanacho ni udhaifu na
nipende kusema haya
1.udhaifu sio dhambi
Kwa maana rahisi ni kwamba ile kwamba umekuwa na udhaifu
haina maana wewe ni mdhambi
Udhaifu sio tatizo ila tatizo ni focus ya mtu mwenye
udhaifu...amefocus kwenye nini? Udhaifu au nguvu alizo nazo.
Mwanadamu hawezi jiboresha au kuboresha udhaifu wa mwingine
ndio.maana ukaitwa udhaifu,
Kunatofauti kubwa kwati ya kushindwa kwasababu ya udhaifu na
kushindwa kwasababu ya kutojua namna ya kuweza kufanya..
Udhaifu ni moja ya vitu ambavyo Mungu anavitumia
kudhihirisha nguvu zake kwa maana rahisi udhahifu ndio mahali ambapo kuna a/c
ya nguvu za Mungu (i can say that)
Kinachotusumbua sio kwasababu tuna udhaifu ila ni kwasababu
hatujajua kwanini Mungu /aliruhusu tuwe na hizo weakness.
Jambo la muhimu ni kwamba UDHAIFU ulionao ni Mungu pekee
anaweza deal nao ndio maana Mungu anatutia moyo kuachana na kufocus kwenye udhaifu. Kwasababu that is not your business
Wakati Musa anajaribu kumueleza Mungu juu ya udhaifu wake
Mungu hakumuondolea ila alimpa njia nyingine
Kwanini udhaifu
1. Fursa ya Mungu kuachilia nguvu zajke na kujitukuza
2. Njia ya kukunyenyekeza.
Usiuchukie udhaifu na wala usiangaike na udhaifu focus na
nguvu ambayo Mungu ameweka kwako. Na hapo ndio utazaa matunda..
NOTE
Si kila unachokiita udhaifu kinaweza kuwa udhaifu kuwa
makini vingine ni tabia yako au kutojitahidi au kujidhibiti n.k
Naomba niwekee mkazo hili...nimezungumzia sana utoshelevu kwasababu ndi sababu ya msingi na ya kwanza ya kwanini uongeze thamani, sasa kama ukiweza kupata utoshelevu KUPITIA UFALME WA MUNGU kwanza hizo qualities nyingine UTAZIPATA NA ZITAKUWA NA MAANA KWAKO...
Mungu awabariki kwa leo naomba
niishie hapa.
Comments
Post a Comment