MINDSET
UTANGULIZI.
Shalom
marafiki wa Yesu, Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa nafasi hii ya kipekee ya
kupata wasaa wa kutumika katika madhabahu hii, niwashukuru viongozi wa huduma
hii kwa mara nyingine tena kutuletea mfululizo wa semina hizi.
Kwa
wale wageni karibuni na kabla sijaanza basi nitaomba tena uongozi utume ile
miongozo kwa faida yetu na wale wageni tujikumbushe.Tafadhali andaa mahala pa
kuandika. Na jiandae kwa darasa.
Naitwa
Victor Jerome, kitaaluma ni mhandisi wa mifumo ya habari na teknolojia ya
mtandanio yani information systems and network engineering.Nje ya hapo ni
certified life coach, na mentor, muasisi wa huduma ya *teen for teen mentorship
program*
Huduma
inayojihusisha na kuwasaidia vijana kujitambua na kuishi maisha wanayoyatamani na
kutimiza ndoto zao za maisha, nimejikita hasa katika masomo ya kujitambua,
mindset, purpose,na goal setting.
Pia
ni mshereheshaji na mwandazi wa shughuli na ninajulikana pia kama mc mtumishi,
Kwa
sasa naishi mkoani moshi na ninafanya kazi na shirika la egpaf kama temporary
data clerk na kituoa changu cha kazi ni hospitali ya rufaa ya kcmc, Sijaoa na
sina sijachumbia bado🤣🤣.
Nitakuwa
nanyi kwa wiki nzima kwa ajili ya somo la mindset.Mwaka jana tulikuwa na kichwa
cha somo kilichokuwa kinasema *RETUNE YOUR MINDSET*
tulijaribu
kufafanua mindset ni nini na inafanyajr kazi, lakini ili tuweze kufikia mahali
pa kuelewa kiundani ili tuweze kujibadilisha mindset zetu na fikra zetu
niliamua kuanza nyuma kwenye somo la *identity*
Hvyo
tutarudi nyuma kidogo kujikumbushia halafu tuendelee mbele juu ya mindset
Zoezi:
1.
Write down who you think you are (dont think,just write)
Andika
unafikiri wewe ni nani? _ (Usifikirie,andika tu)
2.
Who do you admire most (would like to be them) _ni nani/kina nani unamkubali sana_(ungependa kuwa kama wao)
3.
What attracts you to the who #2, why do you admire them _kipi kinakuvutia
kwao?, Kwa nini unawakubali_
Tufanye
zoezi hili kwa haraka na andika pia majibu yako kwenye daftari lako
Wanasema
kuwa kuna siku kuu mbili katika maisha yako duniani,Siku uliyozaliwa na siku
uliyojua/utakayojua kwa nini ulizaliwa,Watu wengi hatujitambui sisi ni kina
nani, tuna nini ndani yetu na tuna uwezo gani
Mpaka
pale ambapo utatambua wewe ni nani na una uwezo gani ndipo utakapoweza kuishi
maisha yako kwa ukamilifu
Wengi
wetu haoa tumewataja watu *tunaotamani kuwa kama wao*
Hakuna
aliyerekebisha swali langu akalijibu kwa namna tofauti.
Wengi
kwa kukosa kujitambua tumejikuta tunaishi maisha ya kioo...
Kioo
kazi yake kubwa ni ku *copy* kitu cha upande wa pili na kukionesha kama
kilivyo,kioo daima hakiwezi kuumba kitu chake au kubuni kitu chake, lazima kila
siku kifanye kilichofanywa na mtu mwingine
Je
wewe unatamani kuwa wewe au unatamani kuwa kama nani?
Je
unaishi kama wewe au unaishi kama fulani?
Usipo
ishi u mimi wako au usipo ishi kama wewe maisha yako hayajakamilika, apostle
shemeji melayeki alifundisha hapa somo
la kusudi la maisha,
Mimi
huwa napenda kutumia mfano wa nafasi za kazi.
Katika
taasisi au kampuni panapo onekana hitaji au pengo fulani kampuni au taasisi
huamua kuajiri mtu mwenye sifa na vigezo vya kufanya kazi ile,ndipo mtu huyo
huajiriwa ili akazibe pengo lile lililopo,
Mtu
huyu lazima awe mwenye sifa na vigezo vya kuziba nafasi ile au pengo lile.
Sasa
Mungu aliona hitaji fulani haoa dunaini, akakuumba wewe na kukutuma uje kuziba
pengo lile au nafasi ile hapa duniani, haukuja kwa bahati mbaya, ulikuja na
kusudi maalumu au kazi maalumu hapa duniani uje kuitimiza.
Kama
hujajitambua na kuishi kuendana na namna ulivyopaswa kuja kuwa hapa duniani maana
yake ni kwamba bado hujaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Kwa
maana nyingine pia ni kuwa mwanadamu hajakamilika, na kwa sababu hyo ndio maana
tunaishi katika jamii ili kukamilishana.
Ndio
maana kuna uwepo wa karama mbalimbali na talanta mbalimbali ili kuhudumiana na
kukamilishana.
Hvyo
basi mimi mwalimu nisiposimama katika nafasi yangu kuna watu upande wa pili
maisha yao yataharibika kwa sababu sijajitambua na kusimama kama mwalimu,
Vivyo
hvyo kwa mwinjilisti,mchungaji, na watu wa kada mbalimbali
Usipo
jitambua na kuishi kama wewe ulivyoumbwa unakuwa hujakamilika na pia
unawagarimu wengine kwa sababu hujasimama kwenye nafasi yako.
Ningetamani
kila mtu atoe jibu kama ameelewa na kama amekwama mahali tumekane sawa,
utangulizi huu ni muhimu sana ili huko mbele tuwe pamoja
Walau
tupate tathmin fupi ya jana...nani anaweza kunipa summary ya utangulizi wa jana
Basi
naombeni tuendelee
*Mimi
ni nani*
Je
ni vipi kati ya hivi hapa vinatambulisha kuwa wewe ni nani
- Kazi
- Kabila
- Tabia
- Mwenendo
Experience
- Knowledge
- Mazingira
- Elimu
Wengi
wetu jana tulijitambulisha kwa kutumia vitu hvyo hapo juu
Lakini
sio jana tu mara nyingi huwa tukiulizwa *wewe ni nani* jibu letu huzunguka
ndani ya vitu tajwa hapo juu na vingine vingi
Sasa
je ukiwa unamiliki mojawapo ya vitu hivi na unaelezea hali ya umiliki/ownership
huwa unasemaje
- Saa
- Gari
- Nyumba
- Akili
Tuchangamke
kujibu basi ili tuendelee mbele,Au niulize kwa maana nyingine
Umewahi
tamka maneno haya...
a) Saa
yangu.....
b) Akili
yangu
c) Moyo
wangu
d) Nafsi
yangu
Mimi
ni *ROHO* nina *NAFSI* na ninaishi kwenye *MWILI*
Na
ndio maana tunatamka nafsi yangu, yangu nani, mimi, mimi nani, roho.
Na
ndio maana mtu anapoaga dunia tunasema mwili wa marehemu fulani, maana yake ni
nini,fulani ametutoka hayupo,kilichobaki ni mwili wake, kilichotoka ndani ya
mwili ni nini, ni roho, na ndio maana tunasema Roho ndio itiayo uzima,mwili
haufai kitu, maana yake kuwa wewe. Ni Roho, uliyopo ndani ya mwili,
Binadamu
wengi tumefungwa utambulisho wetu katika makabila yetu, historia zetu, matokeo
yetu, ufahamu wetu, experience yetu, na mazingira yetu tuliyokulia au kutokea
Tumekubali
watu watupachike identities mbalimbali kutokana na mitazamo yao, nasi
tumezipokea na kutembea nazo kila mahali tumekuwa tukijitambua hivyo ama
kujitambulisha hvyo kutokana na mitazamo ya watu,
Kama
wewe ni Roho, na ulikuja duniani kwa kusudi maalumu kwa nini unaruhusu watu
wakupangie uwe nani, wakuambie uwezo wako hapa duniani ni upi , kwa nini
unaruhusu watu wakuchoree mstari chini kuwa mipaka yako ni hapa wewe huwezi
kufanya hiki au kile, kwa nini unakubali kuchukua identity za watu wengine na
kuishi nazo kama zako .
Wakati
wewe ni Roho na una uwezo mkubwa kuliko hao wanaokuzunguka wanavyokupangia uwe
1.Ni
mambo mangapi umetamani kuyafanya hadi leo na hujafanya?
2.
Je nini kinakuzuia
3.
Je kinachokuzuia ni ukweli au ni mitazamo tu ya watu?
Mara
ngapi umeacha kufanya mambo kwa sababu tu umeambiwa na watu huwezi
hiki...umeona wapi mtu wa kabila hili akafanya hiki
Ukoo
wetu hakujawahi kuwa na aliyefanya hiki wewe ni nani hata ufanye ufanikiwe.
Mara
Ngapi tumeishi kwenye historia za kabila letu,koo zetu,familia
zetu,tumeziruhusu zitute genezee utambukisho na zituambie nini tunaweza na nini
hatuwezi
Hvyo
ni haja ya moyo wangu kuwa utambue kuwa wewe ni nani na una uwezo gani ndani
yako na uanze sasa kuamua kutaka kutoka hapo ulipo na kupiga hatua
zaidi...ukisha tambua kwamba identity uliyojipa mwanzo au uliyokuwa umepewa na
watu sio sahihi ndipi somo la mindset litakapoweza kukuingia na kuweza
kukubadilisha mitazamo yako, self belief yako na kukuwezesha sasa uweze kuishi
kwa mtazamo chanya, kuongeza imani na kujiamini na kubadilisha mtindo wako wa
maisha na kukusaidia kuweza kufika unapotamani kufika na kuanza kuishi u *mimi*
wako katika ukamilifu wake
Karibuni
kwa maswali na michango zaidi
Wazo 1:
Kwa hiyo mwalimu hili👆🏾👆🏾 ndo
jibu zuri la kumjibu mtu akikuuliza wewe ni nani??
Kuna
mtu na mtu, kuna mtu ukimjibu hivi atakuelewa, kuna mtu ukimjibu hivi mtakesha
naye hapo mpaka kesho
Tutakapoendelea
mbele muda ukiruhusu tutasoma call and assignment utapata mwanga zaidi
Mbna
Yesu alisema 'ROHO YANGU naikabidhi......."???
Swali
kutoka group lingine....
Mwenye
jibu hapo:-
Asanteni
kwa leo...bado npo online kwa michango na maswali.
Kesho
tutapiitia belief system na kuingia kwenye somo la mindset
*Swali:* *How can we Discover our
Potential ???????*
1. Watu hufuata nini kwako?
2.
Ni kitu gani unapenda kukifanya bila kusukumwa, na bila kuambiwa, na unakifanya
kwa furaha hata kama hutosifiwa, hutolipwa, hutopata umaarufu au kupongezwa
4.
Kitu gani ukikiona hakiko sawa unasikia maumivu ndani yako na hutokuwa na amani
hadi ukirekebishe?
I
think its because YESU NI MUNGU .....
Na MUNGU NI ROHO
Aliona
wakati roho inatoka.... Kabla haijatoka ...... Akamwambia Mungu Baba ... Roho
Yangu ...
Tulivoumbwa
kwa sura na mfano Wa Mungu.... Tumepewa Roho .... Ila roho zetu ni milki ya
Mungu .... Ndo maana hata hukijiua unakuwa umeua koz hauna dhamana nayo
Jibu
la swali la mwanzo kabisa tamko la Yesu
msalabani
Niombe
radhi kwa leo, nilibanwa kidogo na pia, tutaendelea kesho mapema tu
Namshukuru
Mungu kwa ajili ya nafasi ya kukutana hapa tena kuendelea kushirikishana
machache kwa ajili ya kupanua fikra na kuongeza maarifa.
Tutaendelea
leo kidogo juu ya mada tuliyoianza sitoenda mbali sana kwani nipo safarini
Mniombee nifike salama
Tumeanza
kuona kuwa tatizo la wengi kushindwa kuishi aina ya maisha wanayoyatamani, au
kuishi u mimi wao unaanzia kwenye kuishi identity ambayo sio yako na kukubali
kuziishi identity ulizopewa na watu wanaokuzunguka
Kwa
hyo mabadiliko makubwa ya sisi kuanza kuishi kile ambacho tunakitamani yanaanza
kwanza kwa kujitambua ba kuanza kutembea kwenye identity yako halisi
Sasa
tuingie sehemu inayofata.
*Mindset*
Mindset
kwa kiswahili ni fikra, au mfumo wa utambuzi wa mambo, unaoongoza mienendo ya
mtu, tabia, na hata kungamua hatma ya maisha ya mtu
Mimdset
ya mwanadamu au fikra za mwanadamu zimeundika katika mfumo wa kama wa kompyuta
inavyofanya kazi
Fikra
za mwanadamu zinafanya kazi katika mtindo ufuatao
1.
Kupokea taarifa
2. Kuhifadhi taarifa
3.
Kuchakata taarifa
4.
Kutoa matokea ya taarifa
*kupokea
taarifa*
Mindset
ya binadamu inakula... Na chakula chake kikui ni taarifa, Mindset/fikra/akili
ya mwanadamu inakula kupitia milango miwili/midomo miwili.
*Macho*
*Masikio*
Taarifa
zinaingia kwako kupitia unachoona/tazama kwa macho yako,
Na
pia kwa unachosikiliza kwa masikio yako.
*kuhifadhi
taarifa*
Taarifa
zinazopokelewa mara kwa mara zinahifadhiwa katika fikra zako au katika mindset
yako au katika akili yako, vitu hivi vinavyohifadhiwa kwako vinatumika kama kumbukizi
rejea kwa haraka na ndizo zinazoongoza fikra zako katika kufanya maamuzi
mbalimbali mara kwa mara
Kwa
wale tuliopitia kidogo kompyuta tumesoma kuhusu ram na rom
Ram
inahifadhi taarifa kwa muda mfupi, Na ram inahifadhi taarifa za muda mredu
ambazo mara nyingi hazifutiki kirahisi, Akili ya mwanadamu ina consious na sub
consious mind.
Sasa
hizi consioua na sub consious mind zinafanya kazi kama ram na rom,
Moja
hutumika kuhifadhi taarifa zile ambazo wewe umeziona kama sio z muhimu sana au
ni taarifa mpya sana kwako,
Sasa
pale taarifa hizi zinapoingia mara kwa mara katika ubongo wako zinahamishiwa
sehemu ya pili ambayo ni sehemu sasa ya kudumu
Sasa
hapa ndo wengi tunakosea.....
Wengi
taarifa tulizojana kwenye sehemu ya kudumu ni zile taarifa ambazo sio za msingi
wala za kutusaidia lolotw katika maisha yetu, Mentor wangu huwa anapenda kusema
*Maarifa
uliyonayo huamua kiasi cha pesa ulichonacho*
Maana yake ukijiona huna pesa ya kutosha maana
yake ni kuwa huna maarifa ya kutosha yanayoweza kukutengenezea pesa, Sijui
umenielewa mpaka hapo
*kuchakata
taarifa*(processing information)
Aina
ya mahindi unayopeleka mashine yachakatwe huamua aina ya unga utakaoupata,
ukipeleka mahindi yaliyooza utapata unga usiofaa kula au ambao lishe yake ni
duni,
*Sasa
aina ya taarifa unazoruhusu ziingie kwako ndizo zinazokuwa processed na kutoa
matokea huku nje*
Sasa
taarifa nzuri ni hii:-
jinsi
ulivyo sahv ni matokea ya taarifa unazoruhusu ziingie kwako na zimechakatwa na
mindset yako na kutoa matokeo ya jinsi ulivyo_
*Kutoa
matokeo*
Hapa
najua mmeshanielewa, Kuna swali mpaka hapo
Swali.
1.
Ungeambiwa ubadilishe vitu vitatu kuhusu wewe ungebadilisha nini
2. Kwa nini unataka kubadilisha vitu hvyo kuhusu
wewe
*Andika
kwenye daftari lako majibu kisha piga picha nitumie inbox, Mwisho kesho saa
kumi na mbili jiono
Swali...
Kama
mind ya mtu inafanya kazi kama komputa na komputa ina namna inavyoweza kufuta
taarifa ziliongia either kwenye RAM au ROM
Je
mind pia ina namna inavyoweza kufuta taarifa zilizoingia either kwny conscious
au subconscious
Ndio... Ndo maana kwa wale wa mwaka jana hii
mada nliipa jina *retune ur mindset*
Ntaeleza
baadae hapo mwisho,Lakini njia rahisi kuliko zote ni kuanza kubadili chanzo cha
taarifa, Kama uli jiwrka katika mazingira ya kupata taarifa ambazo hazikusaidii
kukua, kimwili, kiroho na kiakili(maarifa) badili mazingira haya
Kubadili
vyanzo vya taarifa ....sahihi kabisa.Tunaishi kwny ulimwengu tunaokutana na
watu Mara Kwa Mara na watu wenye hulka tifauti na tabia tofauti
Sehemu
zetu za kazi ndio zaidi
Je
ufanyeje ili kuepuka vyanzo vya taarifa,maana kila Mara watu huzungumza na ni
rahisi zaidi kuwasikia wakizungumza. Jambo linapofika kwako mara ya kwanza,
ubongo unalihifadhi katika sehemu ya mwanzo ambayo ni kama ram, ukianza
kulifikiria kwa kina, au kulijadili, au kulichambua kiundani linahamishwa sasa.
Mfano
umepita barabarani ukamuona mwanamke amevaa hovyo, ukamuangali ukaendelea na
shughuli zako,Hili linaishia hapa, ukifika mbele ukaanza kumuongelea sasa
linaenda kiseviwa kwenye rom linakuwa la kudumu,
Ukimya
huwa una maana mwalimu kaeleweka sana, au hajaeleweka kabisa au hakuna
anayemsikiliza,
Nyie
mpo kundi lipi
Swali:
Kati ya mwili,roho na nafsi kipi kimeanza kuwapo duniani?au kipi kinaanza
kuumbwa ili binadamu afanyike mwenye kukamilika pumzi?
*Rejea
kitabu cha Mwanzo*
Swali
dogo juu ya hilo la kwanza ni
Je
maamuzi ya kutenda jambo yana mtiririko gani ukihusisha mwili,nafsi na roho? .Je
ni kipi huanza kuona huzuni binadamu afanyipo dhambi?
Je
ni kipi chenye utambuzi, Niombe walimu wa neno,wachungaji na wainjililisti tusaidiane majibu ya maswali
Karibuni
watumishi kwa majibu
Wazo
2: Roho ya mtu ndiyo iliyotangulia kuumbwa kwenye Mwanzo 1,
halafu
Mwanzo 2, ndipo mwili wake ukaumbwa......
Ninavyofikiri
mimi suala la maamuzi kwa sababu lipo kwenye nafsi, huwa inategemea kama
maamuzi yanafanyika ni kwa upande wa kimwili au ni ya upande wa kiroho.....
Kama
mjuavyo kwamba mwanadamu anaishi kwenye ulimwengu mbili kwa wakati mmoja, sasa
kwenye NAFSI kuna (Nia, Hisia,na Maamuzi).....
Kwa
hiyo kama ukikusudia kufanya jambo la kimwili sharti iwe hivi...
Nafsi
= Mwili = roho
Ila
ukitaka kufanya jambo la kiroho lazima iwe hivi....
Nafsi
= roho = mwili
Kwa
mfano, kwenye maombi lazima uanzie kwenye nafasi, uje kwenye roho halafu
mwili....
Yesu
akasema *roho ii radhi lakini mwili ni dhaifu* maana yale ameshaamua kwa nafsi
yake kuomba, roho ipo tayari lakini mwili unaleta uzito......kukamilisha
maamuzi yake.....
Majibu
toka group no 1
Kipengele
cha pili kuhusu nini kinachohuzunika ukitenda dhambi......
Jibu
ni *roho yako*
Kwenye
roho ya mtu kuna mambo makubwa matatu ibada,
dhamiri na utambuzi
Sasa
dhamiri ndiyo huwa inapata shida ukitenda ndambi na ndiyo inakuishitaki mbele
za Mungu na kwa watu..... Roho iliumbwa, Mwili ukaumbwa, Pumzi ikapulizwa mtu
akawa nafsi hai
Kuhusu
kipi kuanza kuwepo duniani....hapa sijaelewa mwalimu
Ila
mwili asili yake mavumbi
Roho
asili yake ni sura na mfano wa Mungu
Nafsi
asili yake ni pumzi ya Mungu
Mwili .....nafsi....roho
Mwili
unapokea vya mwili na kupeleka kwenye nafsi,Roho hupokea vya rohoni na
kuvipeleka kwenye nafsi
Mwili
huitaji kutawala ukishindana na roho kuitwala nafsi yenye willpower
:
Kuhusu nini kilitangulia kuumbwa kati ya roho na mwili maandiko yako wazi ngoja
nikuoneshe hapa....
Mwanzo
1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;
wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote
pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo
1: 27 - Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Hapo
Mungu alikuwa ameshawaumba kabisa roho zao tena mwanamke na mwanamume.....
Halafu
sasa ndipo akaja akauginyanga mwili wake kwa mavumbi ya nchi.......
Mwanzo
2 : 7 - Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi
ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Hapo
sasa ndipo kaumba mwili wa mwanadamu na akaipulizia ile roho ndani ya ule mwili
ndipo mtu akanyanyuka.......
Ndiyo
maana wakati anamtoa Mwanamke kutoka ubavuni mwa Adamu hakuumba tena roho kwa
sababu alikuwa ameshaumba roho ya mwanamke na mwanamume kama tulivyoona hapo
mwanzo 1:27
Ukitaka
kuelewa kanuni hii vizuri angalia Mungu alichomwambia Yeremia kwamba kabla
sijakuumba katika tumbo nalikujua....Maana yake kabla hujatungwa kwenye mwili
roho yako nilishaiumba tayari.....
Yeremia
1 : 5 - Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni,
nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Nasubiria
majibu ya assignment yangu, Zoezi langu sijapata majibu yenu
Naomba
kurudi nyuma kidogo kwenye identity.....
Nilizungumza
kuwa wengi wetu tumevishwa identities kutokana na mambo tuliyopitia, maisha
tuliyokulia, malezi na mambo mengine mengi,
ü Ufahamu/ujuzi
ü Uzoefu
ü Imani
ü Mfumo
wa uthamani
ü Chaguzi
Halafu
inarudi tena mwanzo
Sasa
narudi kwenye mindset kwa kutumia mfumo huo hapo juu na ntaongelea sana vitu
vitatu ntaviita *EKE* yaani
*ENVIRONMENT*
*KNOWLEDGE*
*EXPERIENCE*
KWA
KISWAHILI
*_MAZINGIRA_*
*_UJUZI/UFAHAMU_*
*_UZOEFU_*
Hapa
naomba muwe makini kidogo
*Belief
system*/ _mfumo wa imani_
Mfumo
wa imani wa mtu au belief system ya mtu ni mfumo uliojengeka ndani yake
unaomuongoza kufanya maamuzi ya kila siku na chaguzi za kila siku katika maisha
yake
Mfumo
huu umeundwa kwa muda mrefu naa ndio mfumo unaoongoza kwa kiasi kikubwa ama
chote kabisa namna mindset inavyofanya kazi
Mfumo
wa imani ndani ya mindset ya mtu unaundwa ama kutengenezwa kwa kupitia vitu
vitatu yaani *EKE*
kuna
watu kuna vitu tunaamini kwa kuwa tumekulia katika *environment* au _mazingira_
yaliyotujengea kuona hvyo vitu mara kwa mara na hvyo kuishia kuamini kwamba ni
vinakuwa hvyo hata kama sio sahihi
Kuna
watu kuna vitu tunaviamini kwa kuwa tu vimetutokea katika maisha yetu tumevi
*experience* na tukafikia kuamini kuwa lazima iwe hvi kwa sababu ndicho kitu
tunakiamini katika mindset yetu haraka haraka
Mfumo
wa imani kuna vitu tumejenga kuamini au kuvitengenezea hyo belief system kwa
sababu tu tumepata kufundishwa, ama kuelezwa mara kwa mara kiasi kwamba
tumefikia mahala tukajenga imani flani juu ya hvyo vitu
Mifano.
Kuna
watu wanaamini kuwa mwanamke jiwe moja haliinjiki chungu, hvyo mwanamke mafiga
matatu.....
Sasa
huyu mtu amekulia katika mazingira ya namna hii ameona wanawake wote wenzake
wanaomzunguka wana michepuko, sasa huyu anajenga imani kuwa jambo hili ni
sahihi na ni la lazima kulifanya na anajikuta naye anaishi maisha ya kuwa na
wanaume watatu au wawili kwa sababu belief system yakr imetengenezwa kuamini
kwamba hiki ni kitu sahihi
Mfano
wa pili
Wapo
wadada wanaamini tu kwamba kwenda kumtembelea mwanaume/mvulana nyumbani kwake
lazima atakutaka kimwili, belief system yakr inamtuma hivi kwa sababu labda ame
experience kitu hiko au amepata ufahamu huo kutoka kwa marafiki
wanaomzunguka...
Mwanamke
mwenye belief system hii hutamuona hata siku moja anakubali kwenda kumtembelea
mvulana anayeishi peke yake kwa sababu tu anachokiamini ni kuwa lazima atatakwa
kimwili au mwanaume huyo amemuitia kukutana naye kimwili,
Na
mwingine utakuta ameenda amejiandaa kabisa ana kanga😐, mafuta,chanua,
na nguo ya ziada kuwa basi endapo liitatokea la kutokea basi ana nguo za
kubadili...
Wapo
wanawake/wanaume wanaamini hakuna mwanaume/mwanamke mwaminifu kwa sababu tu ame
experience kukutana na watu wasio wakweli au waaminifu katika mahusiano
waliyopitia...
Au
hakuna mahusiano bila labda kukutana kimwili kwa sababu tu ame experience kitu
hiko au kasimuliwa na marafiki zake...
Mwingine
hata hajaexperience but maarifa aliyonayo kutokana na taarifa anazozipata kwa
marafiki zake zimemjengea imani hyo
Jiulize
vingi unavyoviamini ndani ya belief system yako ni *facts* au *opinions*,
*truth* au *myth*
*EKE*
Imetutengenezea mfumo wa imani ndani ya fikra zetu ambazo zimeathiri namna
tunavyothamini vitu na ambazo pia imeathiri namna tunavyofanya maamuzi katika
maisha yetu.
Hvyo
kwa yule aliyeuliza swali je naweza kufuta taarifa ambazo sio sahihi ndani
yangu kama ambavyo tunafura cd au ram au rom sasa jibu sahihi lipo hapa yani
kubadilisha belief system ya mtu
Ni
ngumu kumbadilisha mtu au kumshauri mtu ambaye belief system yake inamueleza
vitu ambavyo sio sahihi au ni negative....
Yeye
atakusikiliza tu lakini maamuzi yake siku zote yanajengwa ndani ya ile belief
system yakr
Natamani
msisome hapa kama hadithiya kufikirika na kusadikika bali msome kwa kujifunza
na kuchanganua mambo na tujadili kwa kina na kwa pamoja
EKE
ndiko taarifa nyingi tunakopatia
Hvyo
pia kuanza kubadilisha taarifa unazoruhusu ziingie katika ubongo wako na kwenda
kuhifadhiwa na kutengenezwa katika mindset yako ni kubadilisha EKE yako.
Unataka
kuwa nani, je unachotaka kuwa na EKE yako ina support.
Mazingira.
Yanayokuzunguka, mazingira unayopenda kukaa, wanaokuzunguka mambo unayofanya
mara kwa mara yanachangiaje wewe kuwa unayetamani kuwa?
Je
ufahamu ulionao unakusaidia kuwa unayetamani kuwa, unakusaidia kuishi umimi
wako
Nakaribisha
maswali kuhusu haya machache ya leo
Tumejifunza
nini mpaka sasa.....
Tushirikishane
kwa ufupi watu wawili watatu
*RETUNE
YOUR MINDSET*
Unapokuwa
umefungulia masafa flani au frequency fulani matangazo utakayosikiliza ni yale
yanayotangazwa katika frequency zile... Ukiwa unataka kusikiliza matangazo ya
radio fulani ambayo labda inatangaza kwenye 88.5 basi utakachosikilia ni iile
kinachotangazwa kwenye station yenye masafa hayo,Kama kinachotangazwa katika
masafa ya 88.5 sicho unachotaka kusikiliza basi yakupasa ku retune(kufungulia
masafa mengine) yanayotangaza kile anbacho unataka kusikiliza.
Huwezi
ukawa unataka kusikiliza kipindi cha maombi tuseme redioni saa saba kamili wewe
ukafungulia radio ambayo inatangaza kipindi cha michezo saa saba kamili.
Hvyo
lazima uhakikishe unachotaka kusikiliza
kipo katika masafa yale unayofungulia au unayoyasikiliza.
Kama
unaposikiliza sipo basi badiki stesheni.
Sasa
dhima hii ya retune ur mindset ninachokimaanisha kuwa mpaka sasa uneshajua
ubongo wako unakula kwa njia mbili kuona na kusikia. Na chakula chake kikuu ni
taarifa ambazo ndani yake kuna vitu vingi ikiwemo maarifa, na mambo yasiyo ya
kujenga,
Na
tukasena kuwa njia ya kuanza kuformat mindset yako ya kwanza kabisa ni kuanza
kubadilisha chanzo chako cha taarifa
Sasa
naomba niongelee kipengele kimoja cha mwili kwa nini nasema ubadilisje masafa
ya taarifa
*RAS*RECTICULAR
ACTIVATING SYSTEM_
Huu
ni mfumi wa fahamu katika ubongo unaofanya kazi kama filter au kama sumaku
katika ubongo wako,
Mfumo
huu umeunganishwa na zile sehemu mbili za mindset yako yani consious na sub
concious mind.
RAS
inafanya kazi kwa mfumo ufuatao.
Taarifa
ulizozihifadhi katika mindset yako kwa muda mrefu ndizo zinatumika kama
reference.....
Sasa
baada ya hivi vitu kuwa vimeseviwa ndani yako...
RAS
inafanya shughuli kuu mbili zifuatazo.
Kuchuja.
Kwanza
ras inachuja taarifa zote zinazokuja kwako ambazo haziendani na vitu
vilivyohifadhiwa
Cha
pili itafanya kazi kama sumaku...
Itavuta
taarifa zote zinazoendana na kilichojaa ndani yako na ndicho inachokiatract
huko nje na kukileta kwako
Ukitaka
kujua ras inafanyake kazi kwako
Nakupa
mfano mrahisi.
Ni
wangapi wameona matangazo ya hizi semina na haya magroup?
Na
ni wangapi waliyapita kama hawajaona.. Kwa nini wewe hili lilivuta macho yako
ukapata interest ya kulisoma?
Nyingine
ni je umefollow watu gani, fb, insta, na ni vipindi gani vya redio vinakuvutia
kusikiliza au vya tv kutazama,
Ni
watu wa namna gani wamekuzunguka. Ni
stori za namna gani zinakuvutia kusikiliza...
La
mwisho mambo mangapi yametokea hapa nchini leo tayari umepata info...
Na
mangapi umeambiwa yametokea hata wiki mbili zimepita na hata hukujua umekuja
kujua masiku yamepita.
Si
kuna mtu mtaani kwenu kikitokea kitu mnajua kwake ndo info zote zinapatikana...
Je
watu kwako huja kutafta taarifa gani.. ambaazo wanajua kwako hawawezi kuzikosa?
Hvyo
basi ni muhimu kuanza kubadilisha taarifa kwa haraka ndani yako na kuondoka
zile ambazo unaona hazichangii kukujenga, Lakini pia muhimu kuliko yote ni hili
Tumezungumza
kuhusu EKE.
Sasa
unapobadilisha EKE yako inabadilisja belief system yako.
Belief
system yako inabadilisja mawazo yako na mawazo yanabadilisha mindset yako
Mindset
yako itabadilisha matendo yako ya kila siku
na yatazaa tabia ambapo tabia hujengwa na matendo ya kujirudia rudia.. Tabia
huzaa characyer au mwenendo na mwenendo hubadili hatma ya maisha yako
Kwa
hyo ukitaka leo kubadili maisha yako au hatma ya maisha yako anza kule mwanzo
kabisa kwenye ,Environment, knowledge,experience
Hivi
vitakutengenezea belief system mpya, itatengeneza mawazo mapya na tabia mpya,
kuzaa mwenendo mpya na mwisho kubadili hatma ya maisha yako
Sasa tunanadilishaje....
Je
unataka kuwa nani, au wewe ni nani..
Kwanza
1.
Jua wewe ni nani na una nguvu gani(tumia kanuni ya swot)
2.
Pili jifunze kuishi kwa malengo
3.
Badili chanzo cha taatifa
Sio
kila kipindi ni cha kusikiliza au kutazama, jifunze kuchuja taarifa jipimie
kiasi cha redio unachosikiliza au tv unazotazama.
Tafta
cd za mafundisho, semina, audio clips
Sasa
tunanadilishaje....
Je
unataka kuwa nani, au wewe ni nani...
Kwanza
1.
Jua wewe ni nani na una nguvu gani(tumia kanuni ya swot)
2.
Pili jifunze kuishi kwa malengo
3.
Badili chanzo cha taatifa
Sio
kila kipindi ni cha kusikiliza au kutazama, jifunze kuchuja taarifa jipimie
kiasi cha redio unachosikiliza au tv unazotazama.
Tafuta
cd za mafundisho, semina, audio clips
4.
Tafuta mentor( kuna mentors wa aina tofauti tofauti)
5.
Soma vitabu, vya kiroho, vya maarifa based na kusudi lako na ndoto zako
6.
Tafta marafiki wa kukujenga, waliofanikiwa kupita wewe ili ujifunze kwao na
ambao wako chini yako utakao wanyanyua pia.
Tengeneza
network yako, kumbuka *your network is ur networth*
7.
Hudhuria semina, mafungo, makongamano, warsha mbalimbali za kiroho, za personal
development na za kukujenga based na ndoto zako, kusudi lako na malengo yako ya
maisha.
8.
Jiunge kwenye mastermind groups.
9. Tengeneza routine ya maisha yako na kuwa na
tabia ya kuiishi kesho yako leo, yani iandae ratiba yako ya kesho leo.
10.
Amua kuwa wewe na jiamini kuwa unaweza.
Mwisho.
Nichukue
nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kutumika kwa wiki hii
nzima....naamini kabisa yupo mtu ambaye nimezungumza naye na ataenda kubadilika
baada ya somo hili kwa ufupi.
Niwakaribishe
kwa ushauri, mijadala, kushirikishana na kuongezeana maarifa zaidi.
Pia
ntakuwa na darasa binafsi litakaloanza wiki ijayo tutakalosoma mada nne yanii
Identity
Mindset
Call
and assignment
Na
goal setting techniques.
Mwl.
Victor Jerome:Teen for Teen mentorship program
Comments
Post a Comment