MSAMAHA
Bwana Yesu asifiwe
Naitwa Goodluck Ernest. Ni
mume wa mke mmoja mwanamke na set mbili za mapacha. Mungu ni mwema wote
naendelea kuwadownload toka rohoni ingawa mama yao ameshafika. Namalizia malizia
mambo kadhaa ili awe mke rasmi.
Ninamshukuru Mungu kwa nafasi
hii ya kuweza kujifunza tena kuhusu Msamaha.
Namwamini Mungu kuna makusudi kabisa ya yeye kuruhusu tujifunze Msamaha
Karibu Roho Mtakatifu
utufundishe wewe mwenyewe. Damu yako Yesu inenayo mema ikanene mema juu ya
roho, nafsi na miili yetu tunapojifunza kutoka madhabahuni pako. Katika Jina la
Yesu tunajiachia mikononi mwako tukikuamini kwa ajili ya kipindi hiki, AMEN
Natamani kusikia kutoka kwenu
kwa mara nyingine tena MSAMAHA NI NINI? Nitaendelea nitakapopata mwitikio wa
angalau watano
[6/7, 7:45 PM] +255 716 388 067: Msamaha ni kuachilia kile
kilichokuhudhi au kikosea kitoka moyoni mwako
[6/7, 8:03 PM] +255 655 749 326: Msamaha ni tendo la
kumwachilia Yule aliye kukosea
Inawezekana ikawa bure au ikawa na gharama
[6/7, 8:15 PM] +255 783 862 862: Msamaha nihali ya mtu
mmoja kuachilia au kujutia kosa au tendo alilolifanya dhidi ya mwingine...
[6/7, 8:22 PM] +255 657 360 555: Msamaha ni hali ya
kuachilia uchungu ulioijeruhi nafsi yako kwa kukosewa na mtu iwe kwa kukusudia
au la, msamaha ni hali pia yakuachulia kutokuliweka moyoni na pia
kusahau.kabisa,kusamehe pia ni hali yakijishusha kwa kumaanisha na kuleta
upatanisho katika nafsi zilizokoasana,upatanisho unaofanyika kwa kuondoa
tofauti nakurudisha upendo wa awali bila kuacha kovu, mwisho msamaha ni hali
yakutambua kosa na kujuta kwa yule uliyemkosea ni hali yakuomba upatanisho kwa
yule uliyemkosea
Nafurahi kwa majibu mazuri na
sahihi kabisa, Nashukuru sana. Tumejibu kwa
usahihi.Wengi wamekuwa wakisema
wamesamehe ama wamesamehewa lakini kiukweli hawajui kwa uhakika hasa ni kitu
gani kimetokea
Natamani leo turudie tena
kujifunza kwa mara nyingine kwamba MSAMAHA NI NINI.
Mara zote Msamaha
unapozungumziwa kuna mambo kadhaa uwe na uhakika yataguswa:
-UCHUNGU
-MAUMIVU
-HASIRA
-GHADHABU
-KISASI
Jeraha jingine lolote
linapompata mtu huwa tunafahamu linaleta MAJERAHA ambayo husababisha UCHUNGU
ambao utaachilia MAUMIVU makali kwa yule aliyejeruhiwa.
Ndivyo ilivyo pia kwa Msamaha na Kutosamehe. Moyo
unapojeruhika yule aliyejeruhiwa haraka sana ndani yake hupata JERAHA
linalopelekea kwenye UCHUNGU na hatimaye kuendelea kutembea katika MAUMIVU
makali.
Kumbe basi moyo huwa unaweza:
~KUUMIZWA
~KUJERUHIWA
~KUPATA UCHUNGU
Kwa hiyo unapokuja Msamaha
uwe na uhakika unakuja kushughulika na MAJERAHA, UCHUNGU na MAUMIVU yaliyoenda
kuugusa moyo.
Kwa hiyo;
Msamaha ni:
*Kukoma na kuacha kuhisi hasira juu yako mwenyewe.*
Msamaha ni:
*kutokulipiza kisasi japokuwa una haki ya kulipiza kisasi.*
Msamaha ni:
*Kurudisha na kumwachia Mungu haki ya kulipa kisasi.*
Msamaha ni:
*kuyakatalia maumivu haki ya kumiliki na kutawala maisha
yako.*
Msamaha ni:
*kuamua kuzirejesha nguvu zako na kuchukua tena umiliki wa
maisha yako toka kwa yule aliyekukukosea.*
Msamaha ni:
*Kufikia mwisho wa kuyabeba katika moyo wako maumivu,
uchungu, hasira, ghadhabu, chuki na kisasi na kuviachilia viondoke.*
Msamaha ni:
*Kuacha kuishi katika maumivu na uchungu wa makosa
uliyotendewa.*
Msamaha ni:
*Kuacha kuishi kwenye matumaini kwamba kilichotokea kinaweza
kubadilika na kuwa vinginevyo.*
Msamaha ni:
*Kujiweka huru na kutumia nguvu yako iliyokuwa ikitumika hapo
awali katika maumivu, uchungu, kuitumia nguvu hiyo kuponya na kuvitibu vidonda
vilivyo sababishwa na makosa uliyotendewa.*
Msamaha ni:
*Kumruhusu
aliyekuumiza aondoke yeye pamoja na maumivu, uchungu, chuki na hasira
aliyokusababishia.*
Msamaha ni:
*Kuupenda moyo wako kuliko uharibifu unaoletwa na maumivu na
uchungu wa kukosewa.*
Msamaha ni:
*Kukubali yaliyopita kama yalivyo na kuamua kuutumia wakati
huu kutengeneza na kuboresha kesho yako, kuyafanya maisha yako yajayo kuwa bora
zaidi.*
Msamaha ni:
*Kumweka huru mfungwa na kuja kugundua mfungwa huyo ni wewe
mwenyewe.*
Msamaha ni:
*Uamuzi wa kutotaka haki bali kuonyesha rehema.*
Kwa hiyo unaweza kuendelea
na kuendelea katika maana za msamaha na kufikia mwisho mzuri. Lakini naomba
niishie hapa kwa kuanzia.
Ninakaribisha mjadala na
aina yoyote ya ufafanuzi katika kuzijadili maana zote za msamaha tulizozitazama
leo, iwe ni Mimi ama zile zilizoletwa na rafiki zangu waliochangia mwanzo
Mungu awabariki sana na
usiku mwema!!
[6/8, 2:23 AM] +255 764 392 747: Je unawezaje kumsamehe
kabisa mtu ambae mf n mume wako afu anachepuka, yaan mnaishi wote lkn tabia za
kuchepuka plus maudhi mengine km kukupiga, au kununa, kukutolea maneno ya
kebehi na dharau, kutokulala nyumbn au
kurudi usiku wa manane nk. na hizi tabia
ndo zinazid kila inapokuja siku mpya, je mtu wa namna hii nawezaje kuishi nae
kwa maana hizo za msamaha?
Gudluck Ernest: *Tunaendelea...*
Jana tuliona maana tofauti
tofauti za Msamaha. Wengi tumekwama hapo kwa kuwa ni wachache sana wamekuwa
wanajua hasa huu msamaha ni kitu gani.
[6/8, 9:16 PM] Gudluck Ernest: Ni kweli umeme unaweza
kukupiga shoti endapo hutautumia vizuri. Lakini siyo kwa sababu umekupiga shoti
basi umeme ni mbaya, la. Umeme ni mzuri. Suala ni matumizi yasiyo sahihi. Na
ndivyo ilivyo kwenye Msamaha. Wengi wamepigwa shoti za Msamaha kwa sababu
hawajui msamaha ni nini kwa usahihi na kupelekea matumizi yasiyo sahihi.
[6/8, 9:24 PM] Gudluck Ernest: Ni muhimu sana kurejea mara
kwa mara kujiuliza Msamaha ni nini. Usiwe na haraka kuondoka hapo. Jiulize na
elewa kwa usahihi. Ushindi wote upo hapo, Hallelujah!
[6/8, 9:26 PM] Gudluck Ernest: Kabla sijaendelea na cha leo
kuna swali kuhusu maana za Msamaha?
[6/8, 9:32 PM] Gudluck Ernest: *Moyo:*
[6/8, 9:35 PM] Gudluck Ernest: Mwanadamu ameombewa moyo
ambao hauwezi kubeba maumivu. Naam Mungu amemuumbia mwanadamu moyo ambao haupo
tayari kubeba uchungu na maumivu.
[6/8, 9:44 PM] Gudluck Ernest: Kwa hiyo, unapoumizwa na
tumeona mtu anapojeruhika moja kwa moja maumivu, uchungu, na mengine yote yale
hukimbilia kwenye moyo. Maana yake ni kwamba uchungu na maumivu hayo huweka
kambi katika moyo, moyo ambao Mungu hakuuumba kuvibeba. Uwe na uhakika kwamba
kwa sababu moyo hauwezi kuvibeba basi kuna madhara yatatokea tu.
[6/8, 9:52 PM] Gudluck Ernest: Ndiyo maana Mungu amesema
wazi katika Mithali 4:23 *"Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."* Mungu anakujua na anajua aina
ya moyo aliouumba. Anataka uchukue jukumu la kuulinda.
Anajua yapo madhara ambayo moyo ukiguswa na ukajeruhika basi
uzima wako upo hatarini
[6/8, 10:06 PM] Gudluck Ernest: Ushahidi zaidi unaonekana
katika maandiko mbalimbali kwa mfano Mithali 14:30a *"Moyo ulio mzima ni
uhai wa mwili."* Umeona! Uhai wa mwili wako unategemea sana uzima ulio katika mwili wako. Kitu chochote kisicho
kizuri kinapougusa moyo wako na kutishia uzima wake uwe na uhakika utakuwa
kwenye hatari. Mwili wako utakuwa hatarini tu. Ndiyo maana ni muhimu kuulinda
ili kuwa salama. Na namna moja bora zaidi ya kuulinda moyo wako ni kwa
*KUSAMEHE.*
[6/8, 10:06 PM] Gudluck Ernest: _*"Uhai wa mwili wako
unategemea sana uzima ulio katika moyo wako."*_
[6/8, 10:09 PM] Gudluck Ernest: Ngoja tuanze kuingia ndani
zaidi.
[6/8, 10:12 PM] Gudluck Ernest: Mambo muhimu kuyajua kuhusu
Msamaha:
[6/8, 10:22 PM] Gudluck Ernest: *1. Msamaha ni kwa ajili
yako wewe uliyekosewa*
Msamaha unakuhusu kwanza wewe uliyekosewa. Madhara ama
matokeo ya makosa yanapotendeka humpata moja kwa moja yule aliyekosewa.
[6/8, 10:28 PM] Gudluck Ernest: Si wengi sana wanaojua hili
ya kwamba wanapokosewa, wao waliokosewa ndiyo waliobaki na madhara na matokeo
hasi ya makosa yaliyofanyika.
[6/8, 10:36 PM] Gudluck Ernest: Na ni rahisi mno kujua.
Jiulize wewe mwenyewe unapokosewa ni nini kinachotokea? Unajisikia uchungu?
Unajisikia hasira? Unajisikia maumivu? Unaweza kuendelea kujiuliza na
kujiuliza. Na nina uhakika utapata majibu kwamba ndivyo unavyojisikia na
pengine kujisikia vibaya zaidi. Naam. Huo ndiyo ukweli unaowapata wengi
wanapokosewa.
[6/8, 10:50 PM] Gudluck Ernest: Sasa kama hivi vyote
vinaugusa moyo wa yule aliyekosewa uwe na uhakika yale madhara yaliyo na
kawaida kwenda kuharibu moyo na hatimaye kudhuru vingine vyote katika maisha
basi hakika vitampata yule aliyekosewa bila ya kujali wala kujiuliza chochote
kumuhusu mkosaji. Haitakuonea huruma. Na ndiyo maana Msamaha ni kwa ajili yako
wewe uliyekosewa. Ni kwa ajili yako. Unaachilia kwa faida yako wewe mwenyewe
kwanza. Unamuondoa aliyekukosea moyoni mwako kwa ajili ya usalama na uzima wako.
[6/8, 10:59 PM] Gudluck Ernest: Ndiyo maana Mungu akaonyesha
mfano yeye mwenyewe. Isaya 43:25 inasema *"Mimi naam Mimi ndimi niyafutaye
makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe."* Mungu ambaye ndiye mwanzilishi wa
Msamaha hutusamehe *si* kwa ajili yetu. Mungu hutusamehe kila siku kwa ajili
yake mwenyewe. Ndiyo wakosaji ni sisi. Naam aliyekosewa ni Yeye Mungu lakini
*anayesamehe* ni Yeye Mungu. Na kamwe usisahau hili, ANASAMEHE KWA AJILI YAKE
MWENYEWE.
[6/8, 11:01 PM] Gudluck Ernest: Kama Mungu anasamehe kwa ajili
yake mwenyewe itakuwa ni ajabu mno wewe kufanya kinyume. *Na kwa taarifa yako
hata ukifanya kinyume ni kwa hasara yako wewe mwenyewe.*
[6/8, 11:07 PM] Gudluck Ernest: Unapozungumzia
*"kuumizwa"* uwe na uhakika anazungumziwa yule *aliyekosewa.* Na
ninajua kwa hakika hakuna namna utaumizwa na ikaishia tu bila maumivu na
uchungu kwa yule aliyekosewa, aliyeumizwa. Hivyo katika kuulinda moyo wako wewe
uliyekosewa na kuumizwa basi NI LAZIMA KUSAMEHE.
[6/8, 11:11 PM] Gudluck Ernest: Mhusika namba moja wa Msamaha
ni wewe uliyekosewa. Naam wa kwanza kupokea faida za msamaha ni yule
aliyekosewa. *MSAMAHA NI KWA AJILI YAKO WEWE ULIYEKOSEWA.*
[6/8, 11:15 PM] Gudluck Ernest: Nasikia ndani yangu kuweka
pause hapa. Unaweza kuuliza swali lolote kuhusiana na nilichofundisha leo
[6/11, 10:39 PM] Gudluck Ernest: Mara ya mwisho katika
darasa hili, nilianza kuzungumza kuhusu mambo muhimu unayopaswa kuyafahamu
kuhusu Msamaha. Na ni kweli tukajifunza kwamba kumbe *Msamaha ni kwa ajili yako
mwenyewe.* Wengi tumekuwa tukidhani Msamaha huwa unamfaidisha yule anayeupokea
kuliko anayeutoa. Lakini ukweli ni kwamba Msamaha ni kwa ajili yako wewe
unayeutoa. Ni kwa faida yako. Ni kwa uzima wako. Ni kwa afya yako. Hiyo ni
uamuzi wako kuchukua ama kuiacha. Uchaguzi wowote utakaoufanya uwe na uhakika
ni wewe utakayebeba matokeo yake. Period!
[6/11, 10:51 PM] Gudluck Ernest: Sasa kabla sijaendelea na
jambo jingine la muhimu kuhusu Msamaha naomba niweke wazi suala hili:
_*"Maadam Wewe
unaishi duniani na pia unaishi na wanadamu basi uwe na uhakika kuna siku
utakosewa tu."*_ Ni suala la muda na mahali. Lazima siku moja utakosewa na
kuumizwa na wanadamu hawa. Na wanadamu hawa ni pamoja na Wewe mwenyewe.
Ni jambo ambalo halitegemei na wewe ni mwema kiasi gani ama
unajilinda kwa umakini kiasi gani usiumizwe nakuhakikishia kuna siku wanadamu
kama si mwanadamu mmoja atakuumiza. Ipo hivyo tu yaani. Hata mimi nimeikuta tu.
Ipoooo. Salama yako ni kujifunza Kusamehe kila siku. Kwa sababu hilo ndilo
unaloweza kulifanya pale wanadamu hawa wanapokuumiza. Usisahau hili. Ni muhimu
sana!!
[6/11, 10:58 PM] Gudluck Ernest: *2. MSAMAHA NI GHARAMA*
Hili ni jambo jingine muhimu sana kufahamu. Msamaha wowote
ni gharama kubwa sana kuutoa na hata kuupokea. Wengi hudhani kusamehe ni jambo
rahisi yan unaweza kutoa tu kirahisi. Si kweli. Msamaha ni gharama. Inagharimu
kusamehe.
[6/11, 11:07 PM] Gudluck Ernest: Mara zote unapotaka
kusamehe ni lazima utakutana na gharama inayokupasa kuilipa. Kuna wakati
itakugharimu heshima yako ili umsamehe mtu. Kuna wakati utadharaulika kwa
sababu tu umeamua kusamehe. Kuna wakati utasamehe huku unalia machozi una
maumivu makali.
Ndiyo kusamehe ni gharama. Kuna mwingine utamsamehe na
wakati huo huo hajali na anaendelea hata kukusema vibaya. Lakini unasamehe.
Kuna mwingine unamsamehe na wala hajali kabisa kuwa amefanya kitu gani
kukujeruhi. Msamaha ni gharama.
Kuna wakati utasamehe na wakati huo huo unaendelea kulipia
makosa ya yule aliyekukosea. Lakini bado utasamehe tu kwa sababu Msamaha ni
gharama.
[6/11, 11:17 PM] Gudluck Ernest: Wengi hatujui hili. Lakini
kutojua hakufanyi iwe vinginevyo. Msamaha ni gharama. Ngoja tumtazame
mwanzilishi wa Msamaha:
Ilimgharimu Mungu kumtoa mwanae wa pekee Yesu ili kuweza
kumsamehe mwanadamu. Ilikuwa ni gharama kubwa kiasi gani?
Ilimgharimu Yesu maisha yake ili mimi na wewe tusamehewe.
*Maisha Maisha Maisha.* Hivi hiyo ni gharama ndogo? Hapana. Ni gharama kubwa
mno. Gharama kwa ajili tu ya Msamaha. Halafu wewe unadhani kusamehe ni rahisi,
hapanaaaa. Ni gharama. Ni gharama.
Fikiria utukufu wote aliokuwa nao Yesu lakini ilimgharimu
kuacha kila kitu kwa ajili ya Msamaha. Yaani heshima yote aliyokuwa nayo lakini
akakubali kulipa gharama ya aibu kwa ajili ya kusamehe.
*Msamaha ni gharama.*
[6/11, 11:27 PM] Gudluck Ernest: Unajionea huruma eti
amenikosea kosa kubwa sana siwezi kumsamehe. Aisee Mungu akusaidie tu. Kama
Yesu aliyemuumba mwanadamu Yeye mwenyewe na mwanadamu huyo huyo akamkosea na
hakuishia hapo akamtundika msalabani kwa aibu na dharau na maumivu makubwa
lakini bado akamsamehe, ndugu nakuhakikishia bado hujafikia gharama aliyoilipa
Yesu. SAMEHE. NI GHARAMA ambayo NI LAZIMA UILIPE. Hakuna siku itakuwa rahisi
kusamehe. Huo hautakuwa Msamaha. Msamaha ni gharama.
[6/11, 11:27 PM] Gudluck Ernest: Unajionea huruma eti
amenikosea kosa kubwa sana siwezi kumsamehe. Aisee Mungu akusaidie tu. Kama
Yesu aliyemuumba mwanadamu Yeye mwenyewe na mwanadamu huyo huyo akamkosea na
hakuishia hapo akamtundika msalabani kwa aibu na dharau na maumivu makubwa
lakini bado akamsamehe, ndugu nakuhakikishia bado hujafikia gharama aliyoilipa
Yesu. SAMEHE. NI GHARAMA ambayo NI LAZIMA UILIPE. Hakuna siku itakuwa rahisi
kusamehe. Huo hautakuwa Msamaha. Msamaha ni gharama.
[6/11, 11:47 PM] Gudluck Ernest: *3. MSAMAHA NI MAAMUZI SI
HISIA*
Jambo jingine muhimu kulifahamu ni hili hakuna siku
utasamehe kwa kuwa umejisikia kusamehe. Haipo hiyo siku. Na sababu ni kuwa
kusamehe ni maamuuzi ya dhati unayoamua kutoka ndani yako.
Ngoja nikuambie ukweli huu, unapokosewa ama kuumizwa
kinachofuata ni maumivu. Maumivu ndiyo yaletayo maana hasa ya kujeruhika. Kwa
hiyo ni uongo kusema kwamba wakati umeumizwa utajisikia ile hisia nzuri kiasi
cha kuweza kusamehe, hapana.
Ni kujidanganya kwamba utaweza kusamehe kwa kusubiri hisia
ya kusamehe ije ndani yako. Nakuhakikishia haitakuja hata kwa bahati mbaya.
Unasamehe kwa kufanya maamuzi ya dhati kabisa kwamba nasamehe. Unaamua.
Unaamua. Siyo kujisikilizia.
[6/11, 11:55 PM] Gudluck Ernest: Fikiria Yesu yupo msalabani
katikati ya maumivu makali na makubwa halafu awe na hisia nzuri hivi ya
kusamehe. Yaani Yesu ajisikie kusamehe oooh si ajabu mpango wa wokovu ungeishia
pale. Kusingekuwa na Msamaha. Lakini ashukuriwe Yesu ambaye *ALIAMUA KUSAMEHE.*
Alifanya Maamuzi. Kwa sababu *Kusamehe ni Maamuzi si hisia.*
[6/12, 12:45 AM] Gudluck Ernest: *MUHIMU:*
Sina uhakika ni group gani kati ya haya tuliyonayo katika
RYM lakini yupo mtu ambaye Roho Mtakatifu anasema umuamini kwa hilo
ulilotendewa na kuacha maumivu makubwa ndani yako. Anasema imetosha kuendelea
kushikilia. Anajua ni ngumuu kiasi gani kwako. Lakini anataka umuamini Yeye.
Kuachilia ni hatua ya kwanza muhimu mno ya kumuamini. Na Yeye Roho Mtakatifu
atashughulika na hatua nyingine zilizobaki.
[6/12, 12:46 AM] Gudluck Ernest: Katika Jina la Yesu
natangaza uhuru wako sasa
[6/12, 8:35 PM] Gudluck Ernest: Tunaendelea na mambo muhimu
kuyajua kuhusu Msamaha
[6/12, 8:44 PM] Gudluck Ernest: *4. MSAMAHA HUTOLEWA BURE
KWA YULE ANAYEUPOKEA*
Wakati mwingine imeonekana kuna gharama anayopaswa kuilipa
yule aliyekosea ili aweze kupata msamaha. Hilo siyo sahihi kabisa. Msamaha hutolewaa
bure kwa yule anayeupokea
[6/12, 8:51 PM] Gudluck Ernest: Ni makosa kutaka kuuza
Msamaha. Msamaha huachiliwa bure kwake yule aliyekosea. Ndiyo msamaha ni
gharama kweli. Lakini hakuna gharama atakayolipa yule aliyekosea na gharama
hiyo ikatosha kununua msamaha huo. Ndiyo maana msamaha wa kweli hutolewa bure
bila kusubiri kununuliwa na mkosaji.
[6/12, 9:09 PM] Gudluck Ernest: Kuna watu hutaka mkosaji
alipie. Na yapo malipo ya aina nyingi ambayo aliyekosewa hutamani mkosaji alipe
ili kuweza kumsamehe. Mwingine atataka mkosaji aumie ama aaibike ndipo
amsamehe. Mwingine mpaka mkosaji aje alie na kuomba msamaha. Mwingine atataka
amseme kwanza mkosaji na baadae ndiyo amsamehe. Yapo malipo ya namna mbalimbali
zaidi ya haya.
Lakini hilo ni kinyume kabisa na ukweli kuhusu msamaha.
Tujifunze kwa mwanzilishi wa msamaha, MUNGU. Msamaha alioutoa na kuachilia
ulikuwa ni bure kabisa. Hakuna gharama aliyoingia mwanadamu ili kuupata msamaha
huu. Mungu alianzisha mchakato wa msamaha na kuutoa msamaha kabla ya mwanadamu
kufanya chochote kuulipia. Ni bure kabisa.
[6/12, 9:16 PM] Gudluck Ernest: *5. MSAMAHA HAUCHAGUI*
Mara nyingine imetokea mtu anayetaka kusamehe akaanza
kuchagua ni nani wa kumsamehe na nani wa kutomsamehe. Hili nalo ni tatizo. Tena
ni tatizo hasa kwa kuwa haijawahi kutokea Msamaha ukawa unachagua wa kusamehe
na wa kutosamehe. Haipo na wala haitakuwepo milele.
[6/12, 9:39 PM] Gudluck Ernest: Fikiria Yesu angekuja
kusamehe wakristo tu.? Mungu hakuwahi kufanya biashara kichaa kiasi hicho.
Msamaha aliouachia ulitolewa kwa wanadamu wote. Haukuchagua kundi fulani hivi,
hapana. Hata kama kuna ambao wamejimilikisha ukweli umeendelea kubaki kuwa
msamaha aliouachia Mungu umeachiliwa kwa watu wote. Sasa kama Mungu ameachilia
msamaha bila kubagua nani na nani itashangaza wewe kuanza kuchagua nani wa
kumsamehe na nani wa kutosamehe
[6/12, 9:47 PM] Gudluck Ernest: *6. MKOSAJI HAKUSTAHILI
KUUPATA*
Kuna wakati mtu anakukosea hadi unajiuliza hivi kweli
nimsamehe huyu ndugu.? Niwe mkweli mimi imewahi kutokea. Yaani unaona kwa namna
ulivyokosewa ama kutendewa unaona ukimsamehe huyo ndugu ni kama umempa kitu
ambacho hastahili kabisa.
[6/12, 10:05 PM] Gudluck Ernest: Mara nyingi makosa
yanapotokea na ukatazama, unaweza kuona kama vile yule aliyekosea hastahili
kusamehewa. Huwa inatokea kabisa.
Lakini yule aliyekosea tena kosa baya kabisa ndiye
anayestahili kusamehewa. Msamaha ni kwa ajili ya yule mkosaji tena aliyekosea
haswaa. Msamaha huachiliwa kwa yule ambaye katika hali ya kawaida unaweza
kudhani mkosaji hastahili kuupata
[6/12, 10:08 PM] Gudluck Ernest: *_Anayekosea tena kwa
kiwango kibaya sana ndiye huyo anayestahili na kuuhitaji zaidi Msamaha._*
[6/12, 10:16 PM] Gudluck Ernest: Kesho nitazungumzia kuhusu
*"Nimekusamehe lakini sitakusahau."*
[6/12, 10:17 PM] Gudluck Ernest: Naomba kama kuna maswali
yanayohusiana na niliyofundisha hadi sasa.
[6/13, 7:09 AM] Gudluck Ernest: Kuna ndugu alinitumia
maswali inbox. Lakini kwa bahati mbaya nimeyapoteza. Nakuomba unisamehe na
unisaidie kuyapata tena.. Naomba unitumie tena inbox na unapotuma kwangu naomba
umtumie na Madam Anitha pia. Jioni nitajitahidi kuyajibu.
Blessings!
[6/15, 8:49 PM] Gudluck Ernest: Tunaendelea na mambo muhimu
kuhusu Msamaha
[6/15, 9:05 PM] Gudluck Ernest: *7. KUSAMEHE SI KUSAHAU*
Imekuwepo dhana ya kwamba kusamehe ni kusahau kile ambacho
kimefanyika na kukuumiza. Hii ni moja ya dhana ngumu sana na zenye mjadala
mpana. Unawezaje kusamehe na kusahau? Je hilo lipo kweli?
[6/15, 9:23 PM] Gudluck Ernest: Ngoja niseme ukweli kwamba
kuna mambo yamewahi kunitokea na toka yametokea hadi leo sijasahau. Yamebaki
kuwa kumbukumbu kwenye maisha yangu. Lakini ukiniuliza kama nimesamehe
nitakujibu nimesamehe.
[6/15, 9:32 PM] Gudluck Ernest: Ukweli ni kwamba kuna mambo
yanapotokea huacha alama za kudumu zisizofutika. Kuna makosa yatakapotendeka
yataleta majeraha ambayo hatimae yataacha makovu ya kudumu ambayo yatabaki
kukumbusha kuna jeraha limewahi kutokea hapo
[6/15, 9:38 PM] Gudluck Ernest: Kuna wakati mtu atakukosea
na kukujeruhi na kuacha alama itakayokuwa ni ya kudumu ambayo hata ufanyaje
huwezi kusahau.. Huo ni ukweli ambao huna budi kuujua na kukubaliana nao.
*"Kuna mambo yakitokea na kukujeruhi yataacha alama za kudumu kwenye
maisha yako na utayakumbuka bila kujali unajitahidi kiasi gani
kuyasahau."*
[6/15, 9:51 PM] Gudluck Ernest: Hembu fikiria huyu dada
alibakwa na akapata mimba na baada ya miaka mingi akaweza kuendelea na maisha
yake akasamehe. Swali ni je atasahau yule mtoto amepatikana vipi? Yaani kwa
sababu tu amesamehe basi anasahau kabisa kwamba hakubakwa na akapatikana mtoto?
[6/15, 10:33 PM] Gudluck Ernest: Mama huyu amekuwa akipigwa
na mume wake mlevi na siku moja hadi akang'olewa meno kwa kipigo. Je kila
anapokuwa anajitazama kwenye kioo anapofanya make up zake na kuona mapengo yake
atajisahaulisha kwamba hajui yametokea wapi?
[6/15, 10:43 PM] Gudluck Ernest: Narudia tena kuna
mambo ni ngumu mno kuyasahau yanapotokea
kwenye maisha yako. Yapo mengine ambayo ni kweli unaweza kuyasahau. Lakini yapo
mengine ni ngumu kusahau. Na kama unakumbuka tulipotoka *hakuna msamaha wa
baadhi ya makosa.* Sasa kwa makosa ambayo yamefanyika na kuacha alama
inayotufanya tukumbuke tunafanyaje?
[6/15, 11:02 PM] Gudluck Ernest: Sasa ukirejea tulipotoka
utakumbuka msamaha ni *kuachilia* na si kusahau. Kwa baadhi ya mambo si suala
la kusahau bali ni suala la unapokumbuka kitu gani kinatokea ndani yako.
Unasikia uchungu? Hasira? Maumivu?Unajisikiaje? Jinsi unavyojisikia ndiyo
itaamua umesamehe ama hujasamehe. Kama utasikia naweza kuziita hisia hasi yaan
hasira, uchungu na yanayofanana na hayo basi hujasamehe. Lakini ukumbukapo na
ukajikuta husikii hayo basi umesamehe na
havina madhara kwako. Kumbe unaweza ukasamehe na ukaendelea kukumbuka kwa
sababu *Kusamehe si kusahau.*
[6/15, 11:12 PM] Gudluck Ernest: Na mara nyingi kadri
unavyojitahidi kusahau ndivyo unavyokumbuka zaidi😄 naamini wengi wetu
tunaweza kuwa mashahidi wa hili. Na tumeshindwa kusamehe kwa sababu
tumejisikiaa hatia kwa kushindwa kusahau. Msamaha si kusahau. Acha kujitahidi
kusahau. Jifunze namna gani unaweza kuachilia maumivu na kumuachilia yule
aliyekukosea. Ukifanikiwa kuweza kuachilia uchungu na maumivu uwe na uhakika
utakuwa salama pale utakapokumbuka
[6/15, 11:22 PM] Gudluck Ernest: Inawezekana kabisa
kujidanganya kwa muda mfupi kuwa umefanya jitihada kubwa kusahau. Ndani yako
waweza kujifariji kabisa kwamba
umesahau. Ha! Subiri siku unasikia jina lake linatajwa ama unaonana nae
ndipo utakaposhangaa kifua chako kikijaa na kufura hasira ambayo hata wewe
mwenyewe hujui ilipotokea. Hujasamehe wewe
[6/15, 11:27 PM] Gudluck Ernest: Lakini inapotokea kwa
sababu yoyote ile ukakumbuka ama kumuona aliyekukosea na moyo wako ukaendelea
kuchangamka, haukuvurugika, unashangilia na amani yako ipo pale pale basi huo
ndiyo unaitwa msamaha.
[6/15, 11:30 PM] Gudluck Ernest: Kwa hiyo kusamehe si
kusahau. Acha kujiumiza kwa kutaka kusahau. Shughulika na namna ya kuweza
kuachilia hamu ya visasi, kutaka haki, kuwa na uchungu n.k ili moyo wako uwe
huru halafu mengine ni historia.
[6/15, 11:32 PM] Gudluck Ernest: *"Waweza kuendelea
kukumbuka bila maumivu naam ukiwa umesamehe."*
[6/15, 11:33 PM] Gudluck Ernest: Lakini pia sidharau umuhimu
wa kusahau. Ukiweza kusahau basi ni vyema zaidi.
[6/15, 11:38 PM] Gudluck Ernest: Mwenye swali linalohusiana
na kusahau karibu
[6/16, 9:30 PM] Gudluck Ernest: Tumekuwa tukijifunza kwa
siku kadhaa juu ya mambo muhimu kuhusu Msamaha. Tumeyaita mambo muhimu kwa
sababu ndiyo msingi wa Msamaha. Na namwamini Roho Mtakatifu kuwa mambo haya
yamekuwa baraka kwa wengi. Jambo moja nina uhakika nalo ni hili kuna jambo jema
linafanyika katika maisha ya watu humu ndani. Haijawa bure. Hilo nina uhakika
kabisa. Na ninaendelea kuamini kwa ujasiri kabisa wapo wengine watakaoendelea
kutengenezwa kwa upya tunapoendelea na somo hili.
[6/16, 9:30 PM] Gudluck Ernest: Sasa leo naongeza mambo
mengine muhimu kuhusu Msamaha.
[6/16, 10:10 PM] Gudluck Ernest: *8. MSAMAHA SI KUREJESHA
TENA MAHUSIANO*
Mara nyingi watu walipokoseana na wakaombana msamaha labda
na kweli wakapeana huo msamaha jambo lingine likaibuka nalo ni hili kurejesha
ama kutorejesha mahusiano ya hapo kabla. Leo ngoja tujifunze hili..
[6/16, 10:17 PM] Gudluck Ernest: Ni kweli hata mimi
ningetamani mno mara baada ya kumsamehe yule aliyenikosea basi nirejeshe ule
uhusiano uliokuwepo hapo mwanzo. Lakini siyo lazima kurejesha uhusiano na kila
mtu uliyekosana naye.
[6/16, 10:23 PM] Gudluck Ernest: Kuna wakati baada ya kupata
kwa usalama wako ni vyema na sahihi kabisa kutoendelea na uhusiano na yule
ndugu hata kama umemsamehe. Ndiyo utamsamehe na bado ni lazima uweke umbali
naye kwa usalama wako.
[6/16, 10:32 PM] Gudluck Ernest: Kusamehe si kurejesha
uhusiano. Ni kweli kuna wakati msamaha utakuwa ni hatua muhimu kuweza kurejeza
uhusiano kwa upya. Lakini si mara zote msamaha unapoachiliwa basi ni lazima
uhusiano huo urejee kama mwanzo. Ngoja nitoe mfano kidogo
[6/16, 10:59 PM] Gudluck Ernest: Kuna huyu mama ambaye mume
wake alimkosea baada ya kulala na mfanyakazi wake wa ndani. Na baada ya mchakato wa muda mrefu mama
akaweza kusamehe kabisa. Na akaachilia kabisa moyoni mwake. Lakini kusema ukweli
si salama sana eti kwa kuwa amesamehe basi ni lazima arejeshe uhusiano na yule
msichana. Anaweza kumsamehe na bado akafungasha mizigo ya yule binti kumuondoa
pale nyumbani. Ndiyo. Ni salama zaidi kumtoa pale. Haina maana kwamba kwa
sababu amemtoa nyumbani basi hajasamehe.
[6/16, 11:08 PM] Gudluck Ernest: Unaweza kuchukua na mifano
mingine mingi kwenye mazingira yafananayo na hayo. Ukweli ni kwamba wengi
huchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja wakidhani ni jambo moja ama yakiwa
yana maana moja. Kuna kitu kinaitwa *Msamaha (Forgiveness)* na
*Usuluhishi/Upatanishi (Reconciliation).* Haya ni mambo mawili tofauti kabisa.
Kinachohusiana na mahusiano kati ya mawili haya ni la pili yaani Reconciliation
(Upatanisho)
[6/16, 11:14 PM] Gudluck Ernest: Ngoja tutazame kwa
mwanzilishi wa Msamaha. Msamaha uliachiliwa pale msalabani. Lakini Upatanisho
uliohitajika kwa ajili ya kurejesha mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu
ulifanyika mara baada ya Yesu kufufuka. Upatanisho na urejesho wa uhusiano huo
ulifanyika kwa Yesu kupeleka damu yake mbele za Mungu baada ya kufufuka. Lakini
msamaha ulikuwa tayari umeachiliwa tangu Yesu akiwa msalabani.
[6/16, 11:25 PM] Gudluck Ernest: Ukweli ni kwamba huwezi
kuwa na Upatanisho ama Usuluhishi bila ya Msamaha. Lakini yawezekana kabisa
kuwa na Msamaha bila Usuluhishi.
Najua haya ni maarifa mengine mapya kwa wengine. Tuendelee
kujifunza.
Rejea tulipotoka kuhusu Msamaha ni nini. Msamaha ni
kuachilia na kuyatoa maumivu na uchungu juu ya kile ulichotendewa. Msamaha
wenyewe kama wenyewe hauna lengo kuhusija na mahusiano moja kwa moja. Msamaha
una lengo la kuhusika na moyo wako. Upatanisho ndiyo wenye lengo la kuhusika na
yale mahusiano. Ndiyo maana kuna wakati mwingine ukishaweza kuhusika na
kuuponya moyo wako inatosha. Si lazima kulazimisha kurejesha uhusiano. Kama
uhusiano hauwezi kukupa amani ya moyo si dhambi kutorejeza. Hey, ni jukumu lako
kuulinda moyo wako si mtu mwingine. Kuna wakati kutorejesha uhusiano huo ni
namna sahihi ya kuulinda moyo wako FANYA HIVYO.
[6/17, 12:04 AM] Gudluck Ernest: Unajua kuna wengine utaweza
kuwasamehe lakini wasijue gharama ulizoingia kuweza kumsamehe. Maana yake
pamoja na kwamba unatakiwa kuuishi Msamaha kila siku lakini usiruhusu kuumizwa
kirahisi. Kama unaweza kujilinda usiumizwe na kama njia ya kujilinda ni kwa
kutorudisha uhusiano hiyo ni sahihi kabisa. Ni sahihi. Kuna wakati utasamehe
(rejea kusoma tena kwamba msamaha ni nini) na mtu huyo asiwe sehemu ya maisha
yako, ukawa huna mahusiano naye. Inawezekana kabisa
[6/17, 12:17 AM] Gudluck Ernest: Msamaha si kurudisha
mahusiano. Usisahau hili kamwe. Ni kweli kuna wakati msamaha utasaidia
kuyarejesha mahusiano. Lakini kuna wakati msamaha ndiyo utakuonyesha njia ya
amani ya kuondokea na kutokea kwenye uhusiano huo.
[6/17, 1:59 AM] Gudluck Ernest: Wewe mtu amekuibia mara ya
kwanza kwenye biashara ukamsamehe na kurudisha uhusiano kama mwanzo. Mara ya
pili na ya tatu ameendelea kukupa hasara na ukamsamehe. Sawa. Lakini ukiendelea
kumweka kwenye uhusiano wa kibiashara huo huo kisa unajua na unaweza kusamehe aisee
upo kwenye hatari. Unatakiwa kusamehe na badili uhusiano. Mruhusu uondoke.
Kumbuka hata kama umeweza kusamehe kuna gharama utakuwa umeingia. Hivyo
jilinde. Tunza amani ya moyo wako. Ina maana gani kuwa na uhusiano ambao
unaendelea kujeruhi nafsi yako in the name of msamaha.? Hey huo ni ujinga.
Jilinde! Ni jukumu lako na hakuna mwingine ajuaye maumivu na majeraha
uliyoyapata. Na kama uhusiano huo endapo utaurejeza unaweza kukuweka
kwenye hatari ya kukurudishia maumivu
hayo uhusiano huo hauna maana. Achana nao. Wewe samehe kisha weka mikono na
ondoka mbali nae!
[6/18, 5:42 PM] Gudluck Ernest: Tumepata neema ya kujifunza
kwa siku kadhaa juu ya mambo muhimu kuyafahamu kuhusu Msamaha. Yawezekana leo
ama kesho tukajifunza mengine machache na kuangalia uwezekano wa kuhamia kwenye
jambo jingine.
[6/18, 6:00 PM] Gudluck Ernest: *9. MSAMAHA HAUSUBIRI
KUOMBWA SAMAHANI*
Kabla sijajifunza vizuri kuhusu Msamaha nilikuwa naamini
msamaha hutolewa mara baada ya mkosaji kuomba msamaha naam kusema samahani.
Hili si jambo sahihi.
[6/18, 6:26 PM] Gudluck Ernest: Kama umekuwa ukifuatilia
vizuri tangu mwanzo utagundua msamaha mapema kabisa una maana na umuhimu mkubwa
sana kwanza kwa yule aliyekosewa. Kwa hiyo kama unafahamu kwamba Msamaha ni kwa
ajili yako na ukafahamu hasara za
kutosamehe nakuhakikishia hutasubiri uombwe msamaha ndiyo usamehe.
[6/19, 8:22 PM] Gudluck Ernest: Sawa. Nilikuwa nimeanza
kuzungumza kwamba *Msamaha huwa hausubiri kuombwa samahani.* Na nitalizungumzia
hilo leo.
[6/19, 9:02 PM] Gudluck Ernest: Msamaha huwa hausubiri
mkosaji kusema samahani ndipo utolewe. Hii nayo ni moja ya dhana ambazo
zimeleta shida mno linapokuja suala la kusamehe.
Ni jambo la hatari mno kusubiri mtu aliyekukosea aje
kukuambia samahani ndipo usamehe. Ni hatari kwa sababu kadhaa. Moja ni hatari
kwa sababu unasamehe kwa kuwa umeona na unajua kwa hakika ya kwamba kuendelea
kumbeba yule aliyekukosea ndani ya moyo wako ni hatari. Unachagua kusamehe kwa
kuwa ni salama kwa maisha yako ya mwilini na rohoni. Husamehi kwa sababu
ameweza kuja kukuomba msamaha. Unasamehe si kwa sababu amekuja kuomba msamaha
la. Unasamehe kwa sababu unaupenda moyo wako kuliko maumivu, hasira na uchungu
aliyokusababishia.
[6/19, 9:08 PM] Gudluck Ernest: Ngoja nikuambie ukweli kuna
watu wengine watakukosea na kamwe hawatarudi hata mara moja kukuomba msamaha.
Ndiyo inakuwa imetoka hivyo. Swali ni je utaendelea kuwashikilia kwa sababu tu
hawajarudi kukuomba msamaha?
[6/19, 9:13 PM] Gudluck Ernest: Ndiyo kuna wengine
watakukosea na wasijue wamekukosea. Maana yake hakuna namna huyu mtu atakuja
kuomba msamaha, atakujaje na hajui kama amekukosea?
[6/19, 9:18 PM] Gudluck Ernest: Ni sawa na wale wengine
ambao watakukosea na wakajua wamekukosea lakini wanaogopa kuja kukuomba
msamaha. Utaendelea kujiumiza na kujiharibu huku hujui ni lini mtu wa namna hii
atapata lini ujasiri wa kuja kukuomba msamaha?
[6/19, 9:29 PM] Gudluck Ernest: Wapo pia ambao
watakaokukosea na wakajua wamekukosea lakini isipatikane nafasi ya kuombana
msamaha. Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha hili. Kwa mfano mtu
amekukosea na akaondoka pale ulipo labda ameondoka mkoa ama nchi na sasa hakuna
mawasiliano kati yenu na hilo likasababisha msiweze kuombana msamaha. Katika
mazingira kama hayo utaendelea kumsubiri mtu usiyejua atarudi lini na vipi kuja
kuomba msamaha?
[6/19, 9:39 PM] Gudluck Ernest: Kwani hujawahi kusikia wale
wengine ambao wameendelea kuwashikilia na kuamua kutowasamehe waliowakosea
lakini hao wakosaji wenyewe wala hata hawapo hai, wamekufa. Imagine. Hawapo
hai. Swali watasubiri wafufuke ndiyo waombwe msamaha na kusamehe?
[6/19, 9:44 PM] Gudluck Ernest: Usisubiri mtu akuambie
samahani ndiyo usamehe. Usisubiri. Samehe hata bila ya kuombwa msamaha kwa
sababu ni kwa faida yako.
[6/19, 9:49 PM] Gudluck Ernest: Nataka nikuambie kwa uhakika
ya kwamba kuna wakati watu watakukosea na wala hata wasijali kabisa habari ya
kuja kukuomba msamaha. Yaan wala hawana habari na wewe. Tena wanaweza kuwa
ndiyo wanakucheka kabisa. Halafu wewe unajipa moyo kwamba atarudi kukuomba
samahani ohoooo *HARUDI HUYOOO.*
[6/19, 9:57 PM] Gudluck Ernest: Una jukumu na wajibu wa
kulinda moyo wako. Ni wajibu wako kutunza amani na furaha yako. Na hiyo
yawezekana kwa kusamehe. Kusubiri mkosaji arudi kukuomba samahani ni kumpa
wajibu huo mkosaji. Unawezaje kumpa mtu mwingine dhamana ya moyo wako? Hiyo si
sawa. Huu ni wajibu wako. Ipo ndani ya uwezo wako. Mungu amekuamini na moyo
wako na siyo mtu mwingine. Acha uzembe
[6/19, 10:33 PM] Gudluck Ernest: *SWALI:*
Mwalimu,naamini tunapotaja msamaha tunazungumzia kwa Mungu
na wanadamu... Sasa..
_Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo._
*Luka 23:34a*
1. Hii inakaaje? Kama Yesu anasema WASAMEHE KWAKUWA HAWAJUI
WATENDALO..! Wakiwa wanajua je? Bado wanastahili msamaha?
2. Mkono huo huo ulioshika hilo swali kuna jingine.. Kama
ninazini na nna tubu.. Halafu badae kidogo nazini tena.. Na tena na tena na
tena... Na kutubu hivyo hivyo...na tena na tena na tena.... HII INAKUBALIKA?
Nasamehewa?
3. La mwisho..
Kuna watu HATUWEZI KUFANYA DHAMBI siku ambayo tunaenda
kanisani... Au kabla ya kwenda kanisani.. Lakini tunaweza tukitoka kanisani.
Eti tuna Hofu ya Mungu tunadai... Yani naweza zini nikiwa mbali na kanisa au
mbali na siku ya kwenda kanisani mfano jumatano...lakini jumamosi siwezi
kwakuwa asubuhi yake kuna session ya kanisani.. Au nikitoka kanisani ndio
naweza.
Na baada ya muda nasikia amani kabisa... Hapo amani naitoa
wapi wakati sijaomba toba na kusamehewa?
Je,ninapoomba msamaha katika hili naupata? Hasa kwa dhambi
ambazo nadhamiria kabisa na kujiandaa mwezi mzima au wiki zima kuzitenda?
Asante.
[6/20, 8:20 PM] Gudluck Ernest: Natoa nafasi ya maswali leo
[6/20, 8:28 PM] +255 713 292 216: Mwalimu :swali langu
nikuhusu msamaha eti unakuta MTU kakukosea umemwambia ukweli anakununia hata
ukimsalimia hajibu halafu muda wote unamsikia
anasali ndani kwake je?? Huyu MTU yuko kundi gani?hapo???
[6/20, 8:57 PM] Gudluck Ernest: *Jibu swali#1:*
Kama umenifuatilia vizuri tangu tumeanza kujifunza utagundua
unaposamehe husamehi kwanza kwa ajili ya yule aliyekukosea bali kwanza kabisa unasamehe
kwa ajili yako mwenyewe. Naam unasamehe kwa kuwa unajua kuendelea kumbeba
moyoni yule aliyekukosea na kuendelea kubeba uchungu na maumivu ndani yako juu
ya yale uliyokosewa ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako. Ni kwa hasara
yako kuendelea kutomsamehe aliyekukosea.
Kwa hiyo husamehi kwa kuwa aliyekosea anajua makosa yake.
Kuna wakati utasamehe hata kama aliyekosea hafahamu kama amekosea. Rejea somo
la jana, kuna watakaokukosea na wasijue wamekukosea. Sasa utaacha kusamehe na
kuendelea kumshikilia mpaka atakapojua amekosea? La. Ni lazima umuachilie sasa
kwa sababu huna gurantee kwamba atakuja kujua na hata akijua atakubali kurudi
kuomba msamaha. Mkosaji kujua ama kutojua amekosea haifanyi msamaha uwe halali
ama kutokuuwa halali.
Binafsi naendelea kujifunza bado kuhusu msamaha na sijafika
mwisho. Kwa hapa nilipofika naweza kusema Yesu alipokuwa akisema kuhusu
kuwasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo ni alikuwa akionyesha huruma
(compassion). Alikuwa anautazama msamaha na namna hawa wanadamu wanavyofanya na
akamtazama Mungu akaona huruma. Akaona upendo juu ya wanadamu hawa na ndipo
akawa akiyasema maneno yale. Nafikiri si kwamba maneno yale ndo yangefanya ama
kutofanya msamaha uwepo. Tayari mchakato wa msamaha ulishaanza na Mungu hakuwa
akisamehe kwa sababu Yesu amesema hawajui walitendalo. Mungu amesamehe kwa
sababu Yesu amelipa gharama ya dhambi ya mwanadamu kwa kusulubishwa msalabani
naam kwa sababu damu ya Yesu msalabani. Si kwa sababu ya maneno ya Yesu
wasamehe kwa sababu hawajui walitendalo. Angeweza kutoyasema maneno hayo na
bado Mungu angewasamehe tu as long as Yesu angeendelea na safari ya msamaha
hadi mwisho.
[6/20, 9:30 PM] Gudluck Ernest: *Jibu swali #2:*
Mungu husamehe dhambi zote bila kujali imetokea mara ngapi.
Hawezi kumuambia mwanadamu samehe saba mara sabini na kumtwisha jukumu hilo
halafu Yeye Mungu mwenyewe hawezi. Haipo hivyo. Mungu ni Baba. Na kama ambavyo
baba mwingine anavyoweza kuendelea kumsamehe mwanae anapokosea hata pamoja na
mara nyingine kumuadhibu bado mtoto akaendelea kumpokea kama mwanae ndivyo
ilivyo kwa Mungu. Atakusamehe.
Lakini pamoja na ukweli huo kuna ukweli mwingine je
utaendelea kukosea kwa sababu unasamehewa? Hapana. Huko ni kuchezea neema.
Paulo anauliza tuendelee kutenda dhambi kwa sababu neema ipo? Una uhakika gani
utapata nafasi nyingine ya kutubu? Lakini pia je unajua maana ya kutubu?Kutubu
ni kugeuka. Mungu anapokupa neema ya kutubu anategemea ugeuke. Sasa
unapoendelea kurudia kwa makusudi basi hujageuka. P
Zaidi ipo gharama ambayo kila unapotenda dhambi. Haiendi
hivi hivi bure tu. Kuna gharama. Kwa hiyo uwe na uhakika kuendelea kwako
kukosea na kurudia na kurudia kuna vitu vinaharibika kwako inakugharimu kitu.
Na hata baada ya kusamehewa baadae kuna gharama utaingia kuweza kuvirejesha.
[6/20, 9:32 PM] Gudluck Ernest: Na ninapoendelea kujibu
nawakaribisha wengine kuongezea katika majibu ninayotoa
[6/20, 9:47 PM] Gudluck Ernest: *Jibu swali #3:*
Dhambi haina siku maalum ya kufanya pamoja na kwamba ni
ukweli kwamba Mungu husamehe dhambi zote. Na ni ukweli pia kwamba Mungu
husamehe dhambi zote ambazo mwanadamu atakosea. Lakini hupaswi kuendelea
kukosea kwa makusudi. Ni hatari kubwa.
[6/20, 10:23 PM] Gudluck Ernest: Mwalimu :swali langu
nikuhusu msamaha eti unakuta MTU kakukosea umemwambia ukweli anakununia hata
ukimsalimia hajibu halafu muda wote
unamsikia anasali ndani kwake je?? Huyu MTU yuko kundi gani?hapo???
[6/20, 10:23 PM] Gudluck Ernest: *Jibu:*
Msamaha ni kwa ajili yako. Unasamehe kwa ajili ya moyo wako.
Sawa amekukosea na ukaenda kumwambia ukweli je ulipomwambia ndiyo ilikupa
ahueni? Ngoja niongee ukweli mchungu mtamu, kumwambia ama kumueleza ukweli yule
aliyekukosea juu ya kosa alilofanya bila wewe kuamua kuachilia haina maana
yoyote. Haikusaidii chochote. Sasa ameshajua ukweli halafu?
Wengi tumekwama hapa. Kusamehe ni kuachilia na si kumwambia
mtu ukweli. Unaweza kumwambia ukweli na ukawa hujasamehe na matokeo yake ukala
hasara. Hiyo ni moja.
Mbili yake ni hii kama umeshasamehe na upo huru kinakusumbua
kitu gani kujibiwa ama kutojibiwa kwa salamu yako? Sawa amenuna kwa hiyo?
Anasali ama hasali inakuumiza nini? Ukishajua yupo kundi gani inakusaidia nini?
Mara nyingi hizi ni dalili za kwamba bado yupo ndani yako naam bado ana nafasi.
Unaposema umesamehe ni lazima ukubali kuachilia kila kitu na
uviachie kweli kweli. Kinachotokea baada ya wewe kuachilia na kusamehe
hakipaswi kuwa na athari hasi kwako. Yanayotokea ama kufanywa na mkosaji baada
ya kusamehe hakikuhusu sana. Ishi maisha yako
[6/21, 1:20 PM] Gudluck Ernest: *Maswali:*
1.Je mtu ana uwezo kumwondolea mtu mwingine dhambi
2.Je mtu akinikosea nikimsamehe atakuwa amesamehewa na Mungu
pia?
3.Je ninapookoka ninakuwa nimesamehewa dhambi zote yaani
zilizopita,za sasa na zijazo?....
[6/21, 1:21 PM] Gudluck Ernest: Hahahahahah swali #1 na #3
ni maswali tricky mno. Ni kati ya maswali yanayosababisha idadi ya madhehebu ya
kikristo kuongezeka kila siku. Wanathiolojia waliomo humu ndani wanaweza
kunielewa
Comments
Post a Comment