JE PESA NDO KILA KITU??

JE PESA NDO KILA KITU??
LOAN &HIS SISTER 2014 RUGWE BOYS SCHOOL

Ndani ya Mawazo ya Leo tunaenda kujiuliza au kujadili au kuhoji topic hiyo ya juu, tuanze kwa kuulizana hivi,
Kama ndio au hapana toa hoja, kama kuna namna nyingine hebu tuelezee.

Naomba nikufahamishe kwanza vitu hivi vitatu vinavyoshikilia pilika pilika za hapa duniani ,migogoro inayotokea kila kona za dunia. Ukifuatilia kwa kina unakuta chanzo ni
 #Kupendwa (Upendo,mapenzi) kuna kesi na migogoro mingi inayo repotiwa una kuta ni mikasa ya kukosekana kwa upendo au wivu wa kimapenzi, watu wanafuta na kujishughulisha na shughuli mbalimbali zenye masilahi na zisizo na masilahi kwa kusudi la kutafuta kupendwa au kuonekana ni mzuri au maarufu.
# Imani.  Imani ni kitu cha kipekee sana ambacho kinaendesha maisha ya watu kwa lugha nyingine tunaweza sema hivyo, kwa nini lakini?? Katika kitabu cha Waebrania kinaonesha chanzo cha Imani ni nini, kwanza Imani ni kuwa na uhakika wa jambo kulipata,kulipokea au kukutokea kabla hujaliona au kulihisi, kwa mantiki hii lazima uwe makini na kitu unachosikiliza au unachokula kwa kupitia milango ya fahamu kwa lengo la kukufikishia taarifa au information, huwezi kuwa tofauti na kile ulichokipokea ,mwanadamu una mwili,nafsi na Roho vyote vitakuwa salama kulingana na taarifa unazozipata na kuzipa nafasi ya kuziamini. Kwa nini maandiko matakatifu yanasistiza sana kuulinda moyo kuliko vitu vyote ulivindavyo?? .Jua kwamba moyo ukiharibika  ndo basi. Unaweza endelea kujiuliza maswali mengi zaidi.

#Fedha (pesa,hela au mali) zingine tunaweza kuziweka hapa. Je pesa ni kila kitu?? Maandiko matakatifu yanakiri kuwa " pesa ni jawabu la mambo yote) ,Hapa tukipata majibu haya unaweza kuwa na mtazamo mpana zaidi juu ya sentensi ya juu hapo. Ni nani alisema pesa ni jawabu la mambo yote? Alikuwa katika mkutadha wa hali gani?  Kwa nini hadi ilifikia kusema hivyo?? ,hayo ni maswali ya kujiuliza tu, twende sasa katika mazingira yetu kuangalia nguvu iliyopo kwenye pesa.Mtu mwenye pesa anaheshimiwa kila mahali. Mtu mwenye Mali za kutosha anaweza kupata aina mbalimbali za mahitaji yake ya nje au ya kimwili yaani fahari zote za duniani, pesa ina uwezo hata wa kupindisha haki au kweli.
Lakini pesa haiwezi kutatua maswala ya rohoni, mambo ambayo hayaonekani(nguvu za ki uungu, nguvu za giza) mambo ya kiimani, Ingawa ni dhahili utahitaji pesa kukua kiroho kwa wakati mwingine.

Kitu ambacho nataka tuelewe ni kwamba wakati upo hai hapa duniani yakupasa ujitambue vizuri kusudi la wewe kuwepo.Mungu alituumba wanadamu wengi kiasi hiki kwa ajili ya kusaidiana, au kukamilishana, Hakuna mtu anayeweza na kuwa na kila kitu, itamubidi kila mwanadamu amuhitaji mwenzio kukipata anachokitafuta au anachostahili. Kukosa pesa au kupata pesa isiwe shida katika maisha yako, ukipata neema ya kuwa na Mali za kutosha, kumbuka kuishi maisha yenye manufaa kwa sasa na kwa baadaye.

Kwa hiyo kuna vitu inakupasa uvielewe vizuri wewe kama wewe ili uweze kusimama vizuri kwenye nafasi yako.

Sasa tunaweza kufamu na kuendelea kujifunza juu ya pesa, na mengineo
1.Mwanzilishi wa hela ni nani, au ilianzaje?
2. Je ni nani aliyefikia kiwango cha juu cha kiuchumi, kila kitu shwari kwake?
3.Namna gani unaweza kufikia kilele cha Uhuru wa kifedha??

Napenda nimalizie kwa namna hii ingawa kuna maswali mengine hapo juu sijatoa majibu yake. Ili uweze kumudu vizuri vitu vyote hivyo katika maisha yako bila mkanganyiko inakubidi uwe na ufahamu mzuri au sahihi kuhusu Mungu juu ya maisha yako. Kuna maeneo utapita si kwa sababu ya ujuzi wako au elimu yako ,patahitaji upendeleo wa Kimungu kukuvusha, kuna maeneo patahitaji vyeti vyako ila kuna maeneo patahitaji uvumilivu wako,, uaminifu wako, na mambo mengine mengine yafananayo na hayo. Natakayeweza kukufahamisha utofauti wa utumiaji nyakati hizo ni Mungu ambaye anamfahamu kila mmoja kutoka A hadi Z.Hakuna tunachoweza kumficha Mungu katika maisha yetu.

Comments

Popular posts from this blog

KULIISHI KUSUDI LA KUUBWA.

UAMINIFU