Kitabu cha Nguvu ya Kuzaliwa(Intro..)
Nguvu ya Kuzaliwa
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA UNAPOFANYA MAAMUZI .
1. Hakikisha una ufahamu wa kutosha na uliosahihi wa jambo unalotaka kulifanyia maamuzi, eg, kama unataka kufanya biashara au unataka kuwekeza fanya utafiti wa kutosha, uliza taarifa na upate habari zitakazoweza kukusaidia kufanya maamuzi hayo, usikurupuke kuamua kwa haraka ingawa yapo maamuzi ya kuamua kwa haraka kutegemeana na mazingira na wakati 2. Unahitaji hekima ya kukuongoza kufanya maamuzi hayo na namna ya kuyasema au kuyawasilisha, unaweza ukawa na maamuzi mazuri kabisa lakini ukishindwa kujua the how au namna ya kuyafanya au kuyasema au kuyachukulia hatua utafanya vibaya-1 Falme 12:1-7,12-18 3. Maamuzi mazuri yanahitaji muda wa kujipanga eg Rehoboam alihitaji siku 3, hii inakupa fursa ya kujiridhisha juu maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri na kuyaombea maamuzi hayo, 4. Ipo nafasi ya maombi kwa maamuzi yaliyo na matokeo mazuri, maombi kwa Mungu,muombe Mungu ili akusaidie kuyathibitisha maamuzi yako, mkabidhi Bwana njia zako ili ayathibitishe mawazo yako,kumbuka maamuzi yanatoka ndani ya mawazo au fikra zako, Zaburi 19:14 5. Kama una amini Mungu anayathamini maisha yako basi ujue pia kuwa anajali maamuzi yako kwahiyo fahamu kuwa ipo nafasi ya Mungu katika maamuzi yako, usiingie kwenye mtego wa kuamua peke yako, ni bora usiende vitani kama huna hakika Mungu yuko nawe, tambua nafasi ya Neno lake, 1 Falme 11:26-39, Mithali 16:1-4 6. Maamuzi ni msimamo wa ndani au commitment, unapofanya maamuzi usifikiri unafanya jambo jepesi au rahisi, matokeo ya maamuzi unayofanya yanaweza kukuharibia kabisa maisha yako au yakakuletea matokeo mazuri ya maisha yako, usikurupuke, maamuzi ni vita na ndio
Comments
Post a Comment